Usimpe mtu connection ya kazi ni Bora uiuze kwa gharama

Usimpe mtu connection ya kazi ni Bora uiuze kwa gharama

Kaka hii inanihusu kabisa ... Nina ushuhuda kuna mtu yupo bongo alikuwa akinisumbua sana anatafuta kazi nikamtafutia mahali fulani hapo bongo ...huyo bosi ikabidi aniuzie hiyo nafasi kwa 1.5M japo hii jamaa aliyekuwa ananisumbua hakujua kuwa nimetoa ila nilifanya hivyo kwaajili ya family friend relation toka tuko watoto sana.. jamaa kafika huko Job miezi miwili mitatu anadai aongezewe pakee la sivyo anaacha kazi ...net pay yake kwa mwezi ilikuwa 1M ukiondoa makato ya PAYEE na Mifuko ya Jamii baada ya usumbufu wa muda wa wiki kadhaa Bosi wake akampa option mbili 1. kuendelea na kazi au 2. aandike barua ya kuacha kazi kwa hiari yake jamaa akachagua kuacha kazi kwa hiari yake kwa kuwa bosi kagoma kumuongeza mshahara .. yaani kwa aibu jamaa hajanipa taarifa mpaka huyo bosi wake alipokuja kunichana akaniambia kufanya kazi na watanzania inabidi uwe katili kidogo nijitahidi nisiwe soft sana ile kauli ilinikera sana ila nimejifunza... Tanzania sitakuja kumwamini kijana yoyote kwenye mambo ya connection.. 90% ya vijana shida wamezizoea wapambane tu na umaskini wao kichwani japo wana vyeti mikononi...
Niunganishe hapo, hiyo 1.5m nakurudishia yote
 
Mkuu huwa unasema ukweli mchungu na ni ukweli ulio wazi naunga mkono hoja

Nje na mada kidogo mkuu Taikon wa fasihi Kuna kundi limeibuka kutoka kaskazini mwa Tanzania hapa JF hasa Arusha wakidai kuhujumiwa na serikali kwamba pesa zinazo patikana mkoa wa Arusha ndo zinajenga Dar,Dodoma nk mbaya zaidi wanafikia hatua ya kusema wanahitaji kujitenga na kutengeneza taifa la United State of Arusha kwa kuiunganisha Arusha na Moshi sababu ya wewe mkuu umekuwa unatoa elimu nzuri Sana kupitia uwezo wako katika fasihi na ujunzi wa lugha sanifu ya kiswahili naomba ukipata muda andika jambo kuhusu hili maana mbegu isha anza kumea ya ukanda.
Huo ni uwendawazimu, wapuuzwe hao wakaskazini
 
Kuliko kusimanga na kufanywa mtumwa baada ya kusaidia watu basi tuuzieni hizo connection za kazi
 
Kuna mda kama ukikubari thamani yako na ya ukoo wako ishuke basi kazi boss mwenye kibri itakua ni partner wako maishani.
 
Kuna watu ukiwasaidia wakifanikiwa wanajifanya kama sio wewe vile uliwapigia pande.
 
Kaka hii inanihusu kabisa ... Nina ushuhuda kuna mtu yupo bongo alikuwa akinisumbua sana anatafuta kazi nikamtafutia mahali fulani hapo bongo ...huyo bosi ikabidi aniuzie hiyo nafasi kwa 1.5M japo hii jamaa aliyekuwa ananisumbua hakujua kuwa nimetoa ila nilifanya hivyo kwaajili ya family friend relation toka tuko watoto sana.. jamaa kafika huko Job miezi miwili mitatu anadai aongezewe pakee la sivyo anaacha kazi ...net pay yake kwa mwezi ilikuwa 1M ukiondoa makato ya PAYEE na Mifuko ya Jamii baada ya usumbufu wa muda wa wiki kadhaa Bosi wake akampa option mbili 1. kuendelea na kazi au 2. aandike barua ya kuacha kazi kwa hiari yake jamaa akachagua kuacha kazi kwa hiari yake kwa kuwa bosi kagoma kumuongeza mshahara .. yaani kwa aibu jamaa hajanipa taarifa mpaka huyo bosi wake alipokuja kunichana akaniambia kufanya kazi na watanzania inabidi uwe katili kidogo nijitahidi nisiwe soft sana ile kauli ilinikera sana ila nimejifunza... Tanzania sitakuja kumwamini kijana yoyote kwenye mambo ya connection.. 90% ya vijana shida wamezizoea wapambane tu na umaskini wao kichwani japo wana vyeti mikononi...
Mcanada me nisaidie connection ya Canada pls
 
Naweza nikakubaliana na wewe sana sana maana nimeshakutana na scenario zooote ulizoeleza hapo mkuu.Zote zinanihusu mwenyewe

Nikitulia nitazielezea zoteeeee..Ilankwa 90% uko sahihi
 
Nina laki 5 naitaji kazi ya uhakika na mkataba wa miaka 3 au kudumu..kama unayo njoo tuyakenge
 
Kwema Wakuu!

Namna Bora ya ku-deal na vijana wa sasa ambao Asilimia 90% ni Vijana wa hovyo ni kuwa na roho ngumu tuu. Kama unahitaji mahusiano mazuri yenye furaha na vijana hawa na hautaki kuumia basi nakushauri kuwa na roho ngumu.

Kama sio mtoto wako uliyemzaa basi usimpe connection ya kazi, au usimpe mchongo wa pesa. Ni akheri umuuzie hiyo connection.
Kwa wale wasiojua ni kuwa siku hizi kupata kazi ni mpaka uwe na pesa, hiyo ni biashara inayoendelea mjini. Na haijaanza Leo wala jana. Hilo watoto wa mjini wanalifahamu vizuri tuu.

Kuuza connection ya kazi ni Sawa na kuuza ramani ya nyumba. Hakuna kitu cha Bure. Mwambie mtu Kama unataka kazi nipe kiasi kadhaa nikupe kazi.
Mfano; kazi hii Mshahara wake Kwa mwezi ni Tsh Milioni moja hivyo ili nikupe hii kazi nipe 1M nikupe connection, hataki muache apite kushoto.

Au kijana anahangaika anatafuta kibarua chochote anakulilia shida, wewe usimuonee huruma machozi yake au anavyolalama. Mwambie kuna kazi ya laki tano, nipe laki tano nikupe connection ukafanye kazi. Masuala ya burebure mwambie huna.

Unajua KAZI Kama haujaitolea jasho kuitafuta huwezi kuithamini.

Uza kazi
Uza michongo
Uza ramani ya maadili
Hakuna kutoa burebure. Utanishukuru na hata unayempa hiyo connection atakushukuru.

Kijana ukimpa kazi anadhani uliipata kirahisi. Hiyo ndio mindset ya Vijana wengi ilivyo.
Kwanza kijana akikuambia umtafutie kazi ukamkubalia Kwa akili yake ameshachora Aina ya kazi na Mshahara ambao anautaka. Hivyo kitendo cha kumuambia umepata kazi roho yake itafurahi lakini utakapomuambia kazi gani na Mshahara wake wengi hunyong'onyea.
Na wengi wanaweza kukubali kishingo upande.
Elewa kuwa wakati huyo kijana unayemtafutia kazi hiyo akinyong'onyea Kwa kutoridhishwa na kazi na Mshahara huo, kuna kijana mwingine ambaye hamna mahusiano ya karibu anayekuambia umpe kazi hiyo na yupo tayari kukupa hata PESA Kwa ajili ya kazi hiyo.
Wewe Kwa vile unampenda nduguyo unaacha pesa unampa kazi alafu baada ya mwezi Kuisha anakuambia au unasikia ameacha kazi.
Hiyo inaitwa Shukrani ya Punda

Hajui anapoacha kazi anavunja uaminifu wako na boss wa hiyo Ofisi au Kampuni.
Yeye hajui na hataki kujua na anahaki ya kufanya hivyo Kwa sababu kila binadamu yupo Kwa ajili yake mwenyewe. Wewe ndio ulikosea kumpa kazi na connection mtu ambaye hanamsaada wowote na wewe. Ni Bora ungemuuzia hiyo kazi ili hata akiacha kazi basi uwe umepata chochote.

Haya unakuta mtu hajasoma lakini anchagua kazi, anataka kazi ya ofisini au Hotelini. Unamuambia hizo kazi zinahitaji vyeti yaani waliosomea, anajisikia vibaya.
Sasa unahitaji kazi nzuri na haujasoma unaakili Kweli?
KAZI nzuri zinahitaji walau elimu ya Diploma au Shahada.

Haya imetokea KAZI ya ofisini au hotelini umeunganishiwa lakini unaambiwa Kwa vile wewe haujasomea hayo mambo na hauna taaluma hiyo utalipwa nusu ya Mshahara wa waliosomea. Ati unajisikia vibaya.
Elimu inaongeza value ya mtu mahali pa kazi.
Hata kama utafanya majukumu yaleyale kama afanyavyo mwenye elimu lakini kamwe hamuwezi kulingana.

Kwa hasira unaacha kazi, unamgharimu aliyekutafutia na kuonekana anaakili za kipuuzi kama zako.

Taikon huwaga nashauri, hakikisha mtu anagharamia Kwa jasho na damu kupata nafasi unayoenda kumpa. Hiyo inajenga nidhamu na heshima ya kazi.
Lakini ukimpa kirahisi rahisi naye atafanya na kuacha kirahisi rahisi.

Hata Mungu ndivyo afanyavyo, hawezi kukupa kitu kirahisi rahisi ili ukidharau na kukiona hakina thamani.

Kijana akikuambia umtafutie kazi labda Kwa vile anakuona upo katika nafasi Fulani au Kampuni Fulani mwambie hakuna nafasi na huna huo muda wa kutafutia watu kazi.
Ila Kama itatokea utamuambia. Ikitokea mwambie akupe pesa kiasi Fulani umuunganishe, kama Hana mwambie huna msaada wowote kwake.
Uza kwingine.

Hivyo ndivyo Dunia ya sasa ilipofikia, na hivyo ndivyo tunapaswa kuishi.
Elewa mambo haya,
Wewe sio mungu wao, na wewe sio Baba Yao uliyewazaa hivyo hakuna popote utakapolaumiwa.

Watu tujifunze kujipigania, tujifunze kupambana wenyewe bila kumtegemea yeyote.

Ogopa watu wanaolialia wakiomba msaada. Ni hatari Sana.
Ogopa watu wenye lawama. Hao ndio hatari zaidi.

Mfano mzuri ni kijana Jackson majaliwa, alijitoa mhanga kuokoa Maisha ya watu wengine kwenye Ndege, sio Taaluma yake kuokoa watu lakini alifanya tuu bila kutegemea chochote, lakini hiyo ndio gharama aliyolipia na anachokipata ni sehemu ya malipo.
Unamtafutia mtu kazi mtu anayelala nyumbani anaangalia Series za kikorea au anayecheza PS unategemea nini?
Ni Bora umpe Bodaboda au anayeuza machungwa ambaye amekuomba.
Hawa vijana wanaochagua kazi ni wakuwakimbia au kuwafanyia biashara tuu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Najaribu kuangalia motive behind ya hii tabia yako ,,,
Ni hela huna au unanjaa au nn nn

Ebu ni kwambie mtu ukimuuzia kazi hawezi kuithamini atakua mwizi humo ashafanya hiyo n biashara na yy! Akipata kazi atatafuta namna ya kupiga anajua atanunua kazi nyingine
 
Naweza nikakubaliana na wewe sana sana maana nimeshakutana na scenario zooote ulizoeleza hapo mkuu.Zote zinanihusu mwenyewe

Nikitulia nitazielezea zoteeeee..Ilankwa 90% uko sahihi

Bado hujatulia Mkûu ushushe uzoefu
 
Najaribu kuangalia motive behind ya hii tabia yako ,,,
Ni hela huna au unanjaa au nn nn

Ebu ni kwambie mtu ukimuuzia kazi hawezi kuithamini atakua mwizi humo ashafanya hiyo n biashara na yy! Akipata kazi atatafuta namna ya kupiga anajua atanunua kazi nyingine

Hiyo haitakuwa juu yako itakuwa juu yake.

Weñye uzoefu wa kutoa connection bure wanajua nasema kitu gàni.
Siku ukibarikiwa Ukawa na Nafasi ya kujua connection zilipo utaelewa nazungumzia nini KW Sasa Huwezi kuelewa Kwa sababu nawe unatafuta hizô connections
 
Sikubaliani na wewe kwenye mengine lakini hili bro 💯.
1. Kuna mbwa nilimtafutia kazi nilipokua nafanya kazi, wakati anaomba kazi alikua anatamani anipigie magoti. We bwanaee, alipopata Ile kazi na kumjua bosi ilikua balaa hadi mwenyewe nikaacha kazi. Lakini shetani Hana rafiki, bosi alimsikiliza huku jamaa kanunua harrier na baadaye wakapelekana mahakamani.
2. Kuna mshkaji wa utotoni, msomi mzuri tu, Kuna kipindi Hana kazi hata Mia Hana, ananyanyaswa na mkewe Kama mbwa, nokamhurumia nikampa connection. Hutaamini Kuna siku tumekutana naye akiwa na mkewe, tukakaa mahali tulivu, bili ilipokuja alisemma kila mtu alipie alichotumia. Kalipa alivyokula na mkewe. Mimi nikajilipia. Mbwa yule sitaki hata kumuona.
 
Ndio maana wahenga wanakuambia tenda Wema nenda zako ukiamua kubaki Basi Baki at your own risk.

Binadamu NI kiumbe WA ajabu Sana.
 
Back
Top Bottom