Usimuamini sana mtoto wa kike, kwenye mahusiano kuwa na kiasi

Usimuamini sana mtoto wa kike, kwenye mahusiano kuwa na kiasi

Kama unatumia Anroid ukienda google playstore kuna app inaitwa WHATS WEB CHAT....

Unaidownload halafu ukipata simu ya huyo wifi yangu unaingia whatsapp kune settings kuna sehemu ya whatsapp web.

Then kune simu yako utafungua hiyo app WHATS WEB CHAT...utascan sasa QR code ya inayoonekana hapo kune whatsapp web(kune simu ya wifi etu)....
Mi ningepata hata ya sms Jana nimeangaika Google mpaka simu ili surrender ikazima chaji kumi na robo alfajiri naomba nipatiwe hii elimu
 
Hahaha nacheka kichina huha.

Kauli za faraja hizo,Na mabinti wapenda pesa haswa hawa katika himaya yangu wataisoma namba zaidi.

"Maisha ni mchanganyiko wa taabu nyingi sana zilizoambatana na chembe chembe ndogo sana za raha"
Huu msemo.. Alishawahi kuusemaa mwalimu wangu wa physics.... Ni ww nini?
 
MUENDELEZO.....

Muda mfupi baada ya kufanikiwa kudukua simu yake akawa amerejea na vocha. Nikarekebisha tatizo la simu yake na kuingiza ile vocha kisha nikamuungia data pekee bila dakika wala sms.

Nilifanya ivyo makusudi ili kama atakua na nia ya kuwasiliana na mtu ni lazima atumie whatsapp ambayo mimi nitakua naona kila kitu. Otherwise anunue vocha nyingine ajiunge kitu ambacho nilijua asingefanya kwa wakati ule.
Nilidisconnect wifi kisha nikampatia simu yake, huku data nikiiacha on.

Tuliendelea na maongezi meengi hadi baada ya muda fulani akaniambia "kuna sehemu nataka niende nimeagizwa ma mama ntakutafuta tena jioni" nikamwambia poa haina shida.

Baada ya yeye kuondoka pale huku nikiwa nimeacha data on kwenye simu yake, meseji zikaendelea kuingia. Nikaanza kufuatilia chati zake zote.
Kibaya zaidi alivyokua mjinga alikua hazifuti.

Nilishikwa na mshangao kidogo nilipokua nikiperuzi kwani kuna tetesi nilishawai kusikia kua kuna jamaa anatoka nae ila sikuwai kumuuliza. Na hata nilivyoona ile namba imeingia text imeseviwa my husband nikahisi labda ndo huyo jamaa ambae wanasema anatembea nae, na jamaa nilikua namjua kwa jina na sura na mda mwingine tulikua tunapiga nae story kimtindo japo hakua rafiki yangu. Nilivyokua nashuka na ile chati akili ikanijia kwamba niiangalie chati ya yule mtu aliyemsave my husband.

Nikasoma mwanzo hadi mwisho meseji zao, yes ni kweli alikua anatoka na huyu jamaa aliyemsave my husband na picha iliyokuwa display profile kwa jamaa ni nyingine yofauti na sura ya mtu ambae me namjua na nilikua nikiskia anatoka nae.

Nikaangalia chati za chini. Nikaona jina la yule jamaa ambaye ndio nilikua nasikia na nilihisi anatoka nae.
Meseji hazikudanganya ziliongea yote hadi siku ambayo demu anaenda geto kwa mchizi. Hadi alipofika anamuomba jamaa amfungulie ili aingie. Kilichoendelea humo jiongeze ukiwa kama mtu mzima.

Orodha ya wanaume kwa haraka haraka ni zaidi kama kumi ambao yupo nao kwenye uhusiano. Nisingeshangaa kama hao wanaume wangekua ndiyo wapo kwenye process za kumtongoza, ila ni kwamba hao wanaume tayari yupo nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwanzo nilipoona demu anaweza kua ananicheat kwa mtu mmoja niliumia. Nikahisi labda kuna vitu nilikua simridhishi hadi akaamua kutafta mtu mwingine.

Ila nilipojua tupo wengi kwenye foleni aisee sijui hata nilitoa wapi ile furaha hata yale maumivu ya kuumia roho yakapotea. Sikujua ni kwanini.

Ila nikawa naenjoy kuangalia anavyofanya na alivyokua akitupanga. Idadi ilikua ni kubwa mno.

Nikawa naangalia kila kitu anachofanya. Mwingine ambae hataki kuchati nae, anamwambia anaumwa huku anaendelea kuchat na mwanaume mwingine huyu anamwambia usiku mwema mwingine ndo anaanzisha nae story.

Hapo ndipo nilipojua kwanini meseji zangu za wasap zilikua zinasomwa lakini hazijibiwi.

Nilishangaa zaidi kuona akituma video za nusu uchi kwa mwanaume mwingine huku akikata viuno. Nilizidownload zile video kama ushahidi.

Nilishangaa kwakua hakuwahi kunitumia video kama zile wala picha za vile, na hata baada ya mambo kuanza kusuasua akawa hataki kabisa kusikia yale maneno ya kupandishana genye kama ilivyokua mwanzo kutoka kwangu.

Kuna rafiki zake wawili ndio walikia wanaiva sana sana nikaanza kusoma meseji za hao rafiki zake. Nikakuta rafiki yake mmoja alituma picha ya mwanaume kwa demu wangu. Iyo picha haikua mara ya kwanza kuiona.

First time iyo picha niliiona kwenye status ya demu wangu aliipost, nikamuuliza uyo nani akanambia "my bro mtoto wa mamkubwa" nikaguna akaniuliza "mbona unaguna?" sikujibu chochote.

Alivyotumiwa iyo picha demu wangu, akamwomba rafiki yake namba ya uyo mchizi, alafu akamtumia picha zake ili uyo rafiki yake amtumie mchizi na akamwambia "mtumie izo picha zangu kama na ye amenielewa tufanye mambo"

Yani kiufupi manzi alijirahisisha kwa jamaa na ndio huyo ambaye alimsave my husband.

Nikazirecord chati zote na namba zote ambazo alikua anawasiliana nazo, yani zile za wanaume ikiwa kama ushahidi.

Sasa nikaanza kufikiria niachane nae kwa style ipi. Je nimtumie huu ushahidi wote niliyouona? lakini nikajiuliza mara mbili mbili kwamba kudukua ni kosa kisheria vipi kama akiamua kunishtaki.

Nikaendelea nae bila kumwambia chochote wala kuonesha, dalili kwamba najua anayoyafanya.

Nilikua nikimtafutia sababu ya kuachana nae, ila asijue kwamba najua mambo yake yote hata yale ambayo hakutegemea kuwa ningeweza kuyajua.
Vile vile sijazoea kuacha na ma ex wangu kwa njia ya shari.

Yani me tukitibuana tu napiga, mute hadi tunapotezeana jumla.

Ila kwa huyu, ningetaka kusepa kimya kimya bado angeendelea kujua namtaka.

Nikawa namtafuta mda mwingi namjali, yani nikaanza kumuigizia kama ye ndo yeye kwangu. Kifupi tunasema unamtengeneza kisaikolojia au unamjaza ili ajue kweli umekufa.

Na me nilikua nachati nae kulingana na situation ninayoiona kwenye inbox yake.

Kuna siku jamaa mmoja nafahamiana nae akaniuliza "oya vipi uyo manzi naona upo nae karibu sana ni shemeji yetu nini"

Nilijua ananiuliza vile kwa kejeli, kwasababu alikua ni rafiki wa jamaa mmoja kati ya wanaotoka na yule demu.

Nikamjibu ndio. Jamaa akaguna mmh!! Afu akauliza oya ni kweli au unatania nkamwambia ni kweli. Akasema uyo demu mbona wa fulani kamtaja jamaa yake. Nikamwambia mbona nalijua ilo. Na sio uyo jamaa tu tupo wengine wengi nikamtajia orodha.

Ikabidi jamaa aniambie "oya mwanangu uyo demu kicheche achana nae, me nilikua najua kitambo ila sikutaka kukuambia mapema si unajua mapenzi"

Yani kiufupi washkaji walikua wanajua kuwa demu kiruka njia, ila walikua wanashindwa namna ya kuniface si unajua mapenzi. Unaweza kumwambia mtu hapo siyo afu nae akaenda kusemelea kwa baby wake mwisho wa siku unaonekana we mnafiki.

Jamaa akabaki ameduwaa tu kwamba nimewezaje kujua yote hayo afu still nipo kimya, yani kama sijui chochote. Nikamwambia tulia haya mambo hauhitaji kukurupuka.

Basi niliendelea na maigizo yangu ya kujidai sijui chochote.

Nikapata wazo la kumwambia face to face. Nikamtafuta kwenye simu nikamwambia kuna issue nataka niongee nae. Akashtuka ni issue gani iyo ambayo lazima tuonane ndio tuongee. Nikamwambia usijali ni yakawaida tu mpenzi wangu ila itapendeza kama tukionana ndio tuiongelee. Akaitikia poa.

Sasa ikawa kila tukipanga kuonana tunapishana mara sababu hii mara ile. Me nikaona uyu anazingua. Kuna siku tumepanga kuonana hakutokea. Nikampigia simu namwambia vipi mbona hujaja akanambia alikua na mambo mengi. Nikakata simu.

Niliona huyu tunapotezeana time tu hamna haja ya kuonana face to face. Nikamtumia sms fupi tu yenye ujumbe "its over between us"
Ilikua sio kawaida yake na wala hajawai kunipigia simu usiku alinipigia. Sikupokea, akaendelea tena na tena. Sikipokea.

Kesho yake asubuhi sana nayo haikua kawaida yake akapiga. Sikupokea. Akarudia na kurudia sikupokea nikaanza kukata.

Mida flani ya mchana akanitumia sms. "Sijakuelewa sababu gani imefanya umentumia meseji ya vile. Yani kunikosea ukosee wewe afu uwe wa kwanza kutaka tuachane. Kama hutaki kuwa na mimi si unifate uniambie kwa mdomo ntakuelewa"

Nikamjibu hamna sehemu ambayo me nimekosea. Na nilitafuta nafasi ya kukuambia kwa mdomo nikaikosa ndomana nimetuma meseji. Kiufupi mimi na wewe basi.
Akasema kwasababu ipi. Nikamwambia we jua tu ivyo me na wewe basi.

Akasema au nikufate ulipo uniambie sababu. Nikamjibu itakua vema. Akaniuliza nilipo nikamuelekeza akaja. Alikuja kwa ujasiri na kujiamini mno, hakujua kama me nipo serious akajua ni utani kwakua kuna wakati nilikua mtu wa utani sana.

Akanambia enhee sababu ni ipi mana hata salam hakutaka kuisikia. Nikamwangalia usoni nimemkazia macho afu nikamuuliza unataka kuijua sababu. Akasena ndio nikamjibu kwasababu wewe ni malaya. Na sio malaya tu yani we ni kahaba.

Punde ninavyomwambia hayo maneno hakuendelea tena kuniangalia usoni alikwepesha macho nikaona ujasiri aliokua nao umetoweka ghafla. Alikimbia na kuondoka pale nilipokuepo. Muda mfupi kidogo akanitumia meseji.
Unaweza kuniambia me malaya kivipi.
Nikamwambia njoo nikuambie kwa mdomo kama ulivyotaka. Akasema hawezi kuja. Akataka tuongee kwenye simu. Nikamwambia mauchafu yake anayoyafanya kwamba najua kila kitu kuhusu yeye.

Jambo lingine alilonishangaza ni jinsi alivyokua akibisha kua ye hayajui hayo mambo ninayoongelea. Akasema me namchekesha. Yani hadi nikashangaa anapata wapi ujasiri wa kubisha, nikataka kumtumia meseji zote za ushahidi ila nikaahirisha. Nikaamua kumpotezea kimya kimya.

Alinijibu kwa kejeli mno na akasema namfatilia kama nani kwani nimemlipia mali. Na akasema kwamba ndio umejua leo kua unatoka na kahaba. Nikasema ndio.

Maneno yake mengine akasema kua ye haumii hata kidogo yupo na amani tele. Nikamwambia sawa hata mimi lengo langu sio kukuumiza na ndio maana sikutaka kuyaongelea yote hayo.
Baada ya hapo akahamishia ligi kwenye status. Akaanza kunipiga madongo na vichambo. Nilichofanya nikafuta namba yake ili nisione chochote.

Baada ya wiki moja akaanza kunitumia meseji nikawa sijibu. Anatuma meseji eti hajaniona mda mrefu kanimiss na mengine kibao. Mara ananitumia meseji ananiambia ananipenda mara mimi ndo najua uhusiano umevunjika ila ye kwake halitambui hilo. Yani kiufupi ananisumbua.

Alivyoona kimya akaanza kumtumia mdogo wangu ili aniambie jinsi gani anaumia ila mimi siwezi kujirudi kwasababu nilishanawa mikono. Na nilishajiandaa kwamba huyu mtu mimi na yeye basi. Kwa ile team ya whatsapp angeweza hata kubeba world cup kwasababu ni kikosi kazi.

Tahadhari:

Kama unajua hauwezi kumuacha mpenzi wako usimchunguze.

Kudukua ni kosa kisheria.

Hata wanaume ni waongo ila dada zetu wamezidi.
 
Ahaaa nilimpaga mrembo mmoja hivi simu siku ya siku ikatokea nimeitia mkononi aisee madudu niliyoyakuta yalikuwa yakutisha.

Nilikuwa najua kwa jinsi alivyomrembo there is no way nitaweza mmiliki mwenyewe ila pia sikutegemea pia ningeweza mkuta ametupanga foleni wanaume wengi vile.
 
Ahaaa nilimpaga mrembo mmoja hivi simu siku ya siku ikatokea nimeitia mkononi aisee madudu niliyoyakuta yalikuwa yakutisha.

Nilikuwa najua kwa jinsi alivyomrembo there is no way nitaweza mmiliki mwenyewe ila pia sikutegemea pia ningeweza mkuta ametupanga foleni wanaume wengi vile.
Hhaha awa ndugu zetu inabidi tuishi nao kwa akili
 
[emoji23][emoji23] sema hamna feeling nzuri kma ukigundua mpo zaidi ya wawili yani hta yule anayeonekana anapendwa kumbe nae anachitiwa na wapo wengine. Ile inapunguza hasira zte ss unakua unajua una deal na Kahaba ss sio Mwanamke mwnye stara
Kweli kabisa kama ukijua mpo wengi haiumi, kwasababu unajua ni wengi mlichezewa akili
 
Huo muendelezo unafanana na ishu yangu hvyo hvyo yani.
Alafu wanawake hta ukimuelezea kila kitu na ushahidi wa uhuni wake bdo atang'ang'ani kubisha yani huwaga awakubali kma wanafanya umalaya
Wengine walikua wanalia lia tu inbox kwake aisee. Ila ukiwa unamchora mtu anachofanya bila yeye kujua raha sana. Unajiona kama ninja fulani ivi.
 
Daaah mapenzi ni ushezi sana,hivi kuna wadada waaminifu 100% hawa cheat kweli? Ndo maana vijana hawaoi maana unakuwa namsichana unamwamin ila.lazma makucha yajidhihirishe tu.
Lakin acha tuende nayo hivo hivo
 
Mwanamke muamini kwenye mambo mengine, sio mapenzi.

Kumuamini mwanamke kwenye mapenzi ni sawa na kucheza bahati nasibu. Unaweza kupata au ukakosa ila uwezekano wa kukosa ni mkubwa kuliko kupata.

Trust at your own peril.
I trust my inner voice. Once nikiona dalili mm hiwa najisogeza pembeni mapema.
 
Back
Top Bottom