Usimuazime simu yako mtu usiyemfaham vizuri, Itakugharimu

Usimuazime simu yako mtu usiyemfaham vizuri, Itakugharimu

Maeneo ya mijini yenye watu wengi na hata mitaani tu usimpe mtu simu hasa usiemjua hata kama amekuona unapiga sasa hivi,, mpe mtu simu ambae una uhakika nae tu maana majambazi, wezi, na wahalifu wengine hupenda sana kutumia iyo mbinu ya kuazima simu sababu wasipatikane kirahisi wakiwa wanatafutwa.
 
Ni kweli kabisaa.
 
Nakubaliana 100% kumuazima azima mtu smu yako ni risk japo kimtaa mtaa sometime mtu unaingiwa na huruma,
 
Tunapoelekea hata kusalimiana haitawezekana. Miaka michache nyuma tu hapo kuna vijiji uliweza kugonga mlango wa usiyemjua na akakupa chakula na malazi. Mambo yanaharibika sababu ya kuongezeka uhalifu.
 
Kabisa kabisa. Zaman mtu akikupita bila kukusalimia unamuuliza we vp mbna husalimii, lakn sku hz mtu akikusalimia unastuka, na sometime unaanza kujikagua kama smu yako bado ipo
 
Kabisa kabisa. Zaman mtu akikupita bila kukusalimia unamuuliza we vp mbna husalimii, lakn sku hz mtu akikusalimia unastuka, na sometime unaanza kujikagua kama smu yako bado ipo
Ndo maana mataifa ya walioendelea inapambana sana na mifumo ya utambuzi.
 
Iko hivii;
Hapa mtaan kuna office za kubeti kwa hyo mara nyingi huwa nashinda hapo. Sasa kuna jamaa imetokea tu tumezoeana kwa sababu kila sku tunakutana humo ndanin(simjui jina wala sina details zozote juu yake).

Sasa kuna siku akaazima smu yangu ampigie mtu nikasita nikamwambia mimi sina dakika. Sasa jana kaazima tena simu yangu ampigie mtu nikashindwa kukataa kwa sababu nilikua nmetoka kumpigia mtu muda huohuo kwa hyo alikua na uhakika kwamba nina dakika.

Mimi: Hallo mpigie mwnyewe mana mm nshaondoka pale

Namba ngeni: Mimi namba yake sina, nipatie nimpigie

Mimi: Kwan yule ni nani yako mpaka mnawasiliana afu huna namba yake?

Namba ngeni: Mimi ni askari polisi wa upelelezi nipo Kigambon namtafuta huyo ni mhalifu
Nikakata simu nkarudi kule kwenye kubeti nkamwambia jamaa hebu ongea na hii namba mana sielewi elewi. Nkampigia yule wa namba ngeni then wakaongea kidogo nikamwambia jamaa ampe namba zake ili ampigie kwenye smu yake

Jamaa akamtajia namba akampigia wakaongeaaa wakamaliza. Nkamuuliza huyu jamaa ambae nlimuazma smu kwani huyo anaepiga ni nan kwako? Akanambia ni kaka yangu yeye ni askari na ana miradi mingne lakini hanaga msaada kwangu. Nkashtuka mhhh inakuaje kaka yako akuite mhalifu? Jamaa akanielezea pale kwamba huyu kaka yao ni mtu wa kujimwambafai n.k

Sikuridhika na maelezo yake ikabidi niipige tena ile namba ngeni

Mimi; vp kwa hyo huyu jamaa sio mhalifu?

Namba ngeni; hapana huyo sio mhalifu ila nlitumia tu hiyo njia ili kuweza kuongea nae, huyo ni mdogo wangu.
MWISHO.

Ukiachana na scenario hyo pia

Kuna siku jamaa mwingine kaazma simu ya mtu atume sms mara moja, kumbe anachati na binti ambaye ni mwanafunzi. Baada ya kumaliza charting akamrudishia smu mwwnye nayo, asa kumbe yule mwanafunzi anatumia smu ya mamake na hakufuta msg alizokuwa anachat, basi yule mama kafatilia ile namba mdogo mdogo akaja kumdaka jamaa ambae ndo mmiliki wa simu sasa. Jamaa alijitetea sana kwamba sio yy aliekuwa anachat na mwanae lakn wapiiii,,, jamaa alilala kituoni sku mbili ndo mhusika alivopatikana jamaa akaachiwa.

Au sometime unajikuta upo kwenye basi afu abiria mwenzio anaazma simu ampigie mwenyeji wake,,

Au upo ofisini kwako anakuja mtu kabeba bag anaonekana kabisa huyu n mgen maeneo haya anakuambia smu yake haina chaji/hana smu/kapoteza smu kwa hyo anaazima smu ampigie mwenyeji wake,,,,, kumbuka watu hawa unakua hujui wana mipango gan labda ni majambazi/wauaji/ human trafficking /any other criminals wanawasiliana kwa hyo wakidakwa na ww unaunganishwa kwny kesi.

Swali langu ni je NAWEZAJE KUKWEPA KUWAAZIMA SIMU YANGU WATU AMBAO HATUFAHAMIANI VIZURI ILI KUEPUKA MATATIZO??
Kumbe mlikutana kwenye KAMARI
 
Back
Top Bottom