Usimuazime simu yako mtu usiyemfaham vizuri, Itakugharimu

Usimuazime simu yako mtu usiyemfaham vizuri, Itakugharimu

kwakipigo nilicho kutananacho sintasahau mtu mwenyewe humfahamu umeachiwa kesi usio ijuwa nilitolewa mkoani mpaka dar nilizungushwa jiji lote mitutu inakuangalia kuazima simu nimekoma bora nikununulie vocha ukapambane huko mbele
Bora ww una ushuhuda kamili mana Hance Mtanashati kasema hii ni chai!!!!

Vp uliemuazma smu alikuwa n mpita njia au mtu ambae angalau umemuona mara 2,3?
 
Wewe umeongelea mtu usiyemfahamu. Mimi naongezea. Hata mkeo unayelala nae kitanda kimoja uchi marufuku kugusa simu yako.
😀😀😀 Huyo kdogo kesi yake sio kama ya stranger,, mana n rahisi ku-trace back na kujua n nan alitumia smu kupiga
 
NDIO huyo ni mmoja wa watu usiowafahamu kwanini waguse Simu yako? SIO mkeo TU hata Mumeo na Mkweo
Kwa tulipofika naona kuna ulazma wa kufundisha somo la uaminifu mashuleni,, mana kwa sasa mtanzania wengi n tapeli kwanzia viongozi wa dini, raia, wafanyabiashara, boda boda, machinga, mkeo, mwabao, ukikaa vibaya tu unapigwa
 
Nakuongezea hii


Epuka kujifanya msamaria kutaka kupokea mizigo watu waliosimama kwenye daladala usiowafahamu. Kwa simu, kama anakwambia hana vocha wewe mpe jero akanunue vocha akikwambia simu yake imeisha chaji mpe jero akatafute pa kuchajia simu.

Wandugu, jifunzeni kuwa strict katika maisha yenu, usitake kuonekana mwema ukaja kulia kipumbavu
Hii ya daladala kuna jamaa kapanda na bag lake la mgongon kakuta daladala imejaa ikabidi asimame, akamwomba jamaa aliyekaa amsaidie kupakata bag lake, mbele kdogo police wanasimamisha daladala kumbe yule mwenye bag lake ashastukia mchezo akashuka

Katika searching wakamkuta jamaa aloombwa asaidie kupakata bag yuko na lile bag, kufungua ndani kumbe bag lina bangi, jamaa kujitetea bag sio langu anaambiwa tuoneshe mwenye nalo, kuangalia kulia na kushoto jamaa hayupo,,, ndo ikawa siku yake ya mwisho kuwa huru.
 
Kikubwa zaidi usije ukampa mwanafunzi wa kike lift hata Kama Ni jirani yako, mvua inanyesha na Giza linaingia. Utakuja kujuta hutopata wa kukutetea.
Mwisho kabisa usije ukamsifia mwanamke yoyote mbele ya mke wako au mke wako akajua, tafadhali MTU wa kusifiwa Ni mwanao na mke wako tu. Full stop.
Mambo mengi mda mchache,, tunajifunza daily
 
Back
Top Bottom