Usimwachie mkeo nyumba zaidi ya miaka 5 peke yake

Usimwachie mkeo nyumba zaidi ya miaka 5 peke yake

Me too

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,388
Reaction score
9,333
Wale mliozaa na kusomesha mpaka watoto wamepata kazi na kuoa /olewa.
Sasa baba akapata uhamisho wa kikazi akahama mkoa, mke akamwachia nyumba na mtoto mmoja labda ila wengine wameshaoa.

Kwa bahati mbaya baba kazi zake ni nyingi kiasi anashindwa kurudi weekend nyumbani, miaka imekata zaidi ya 5 na mke ameshazoea kukaa mwenyewe.

Ikumbukwe kabla hujahama kikazi mliishi wote na mmelea mpaka kuozesha / kuozeshwa watoto ndio ukahama. Sasa kwakuwa mke alishazoea kuwa underground no power na watoto wanalijua hilo,, kosa linakuja pale utakapo muacha mkeo ajitanue zaidi ya miaka 5 anakuwa keshajijengea power anasahau wajibu wake.

Madhara yatakuja kama hivi,,

1) mama atasikilizwa sana na watoto (hapo ndio mwanya wa kusemea kuwa baba enu kaniterekeza) kumbe anatafuta huruma, na kwakuwa mlikaa nae kipindi kabla hamjaoa / olewa mnakumbuka busara na jinsi alipokuwa mnyenyekevu kwa baba hivo hata atakachosema chochote kuhusu Baba kwenu watoto jiwe kibaya /kizuri lazima mkiamini.

2) kwa sababu ameshatanuka power atatawala na ndio ndugu zake watatawala nyumba yako kiasi kwamba hata kama Unataka kurudi kwako unahisi kama vile Unaenda ukweni. Unajikuta una ahirisha.

3)chuki baina ya baba na watoto,, kama kawaida mama ataanza kuwapa sumu ya maneno watoto ili tu wamtenge baba na pesa za kifuta jasho cha wazazi mama ndio awe anatumiwa,, hapo ndio muda mwingi watakaoutumia kuongea kwenye simu ya kumteta baba na namna ya kumuweka mbali na upendo wa watoto (wakati haya yote mtoto ataburuzwa kwa sababu aliondoka nyumbani kipindi baba na mama waliishi wote na mama alikuwa mnyenyekevu nyote mnajua,,) kumbe maisha baada ya watoto kuoa na baba kuhama kikazi yalibadirika.

3)Baba na mama hapa watafikia mda mama hata simu kupokea ya baba ni kazi vituko na ubabe mama atavionesha hadi kwa mawifi na mashemeji baba akijaribu tu kuwaambia watoto wake mama yao anacho Fanya ataambulia kununiwa na hata kumblock watatamani

4)kusambaa kwa ndugu wa mwanaume, kwa sababu mama ameshajijenga power amejaza ndugu zake kwa bahati mbaya amewajaza kiburi nao, sasa itokee tu Dada wa mwanaume amekuja kusalimia hapo nyumbani kama ilikuwa alale wiki ataenda guest na atageuza siku ifuatayo kijijini.

5)mwisho na la msingi itokee baba anastaafu anataka arudi nyumbani kwake hapa mke huwa hataki kabisa na anatamani utafte mahala ujifiche ila usirudi nyumbani,, kwanini?

Kwa sababu ameshajipower si kwa majirani, ndugu pande zote mpaka ukweni hivo kurudi kwako kutaleta msiba kwake airudie ile hali ya kukunyenyekea hatoweza,, kuwafukuza ndugu zake aliowajaza ndani huku wakimlamba miguu na yeye akiwaonesha ufalme atashindwa.

Sasa hapa mama huyu anafanyaje? Atafanya figisu baina yako (baba) na wanao kama alikuwa anaishi na mtoto wenu wa mwisho ( kwa bahati hajafanikiwa kimaisha bado yupoyupo tu) atamtumia huyo mtoto kukuonesha jeuri ili ushindwe kurudi nyumbani, ukijaribu kuwatafta watoto waliooa uwaambie hayo mauzauza wao hawatokuamini kwa sababu kabla hawajaoa picha walilo nalo la mama yao alikuwa mnyenyekevu, Mwisho wa siku baba anaambulia upweke hana msaada ndugu zake nao wamekimbizwa kipindi kaka yao alipokuwa nje kikazi, kiasi kwamba ukijaribu kuwatafta ndugu nao uwaelezee wakutatulie tatizo nao wanakukwepa wanamwogopa mkeo.

NB: ukihamishwa kikazi beba mkeo asipate mwanya wa kuujua ufalme (power).
 
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
 
Upo?
 
Mm nafikiri wakati mwingine tutofautishe hii kama umeona kwenye familia frani isimlie kama ilivo halafu utoeushauri mwanamke akiwanasababu yakukutenga nafamilia hata ukiwepo atafanya tu kwanza mtoto kama umemlea mpaka kuolewa hawezi kubadilika kilahisi hivo had kumchukia baba
 
Nijibu kama mtoto
Ni upumbavu na ulimbukeni wa hali ya juu kuamini maneno ya mzazi mmoja pekee , na ni ujinga usio na kipimo kumtenga mzazi mmoja kisa umejazwa maneno ma mzazi mwengine.

Mambo yao waachie wenyewe wewe focus kwenye kuwasaidia kadiri uwezavyo ili upate baraka zaidi kwa maana kama wewe ni wa kiume na umeoa jua ipo siku utaitwa baba pia na malipo si ni hapa hapa duniani?

Mwisho kabisa sisi kama watoto tuache kuingilia mambo yaliyotokea baina ya wazazi wawili kiasi cha kuwagawa kimakundi eti kisa baba alimtesa mama ,kisa mama alitelekezwa na baba? Utaaminije maneno ya upande mmoja WEWE KAMA MTOTO PLAY PART YAKO ACHA UJUAJI MWINGI , BLOOD FOOL!
 
Wamama si unawajua vizuri?
 
Mm nafikiri wakati mwingine tutofautishe hii kama umeona kwenye familia frani isimlie kama ilivo halafu utoeushauri mwanamke akiwanasababu yakukutenga nafamilia hata ukiwepo atafanya tu kwanza mtoto kama umemlea mpaka kuolewa hawezi kubadilika kilahisi hivo had kumchukia baba
Yote kwa yote mwisho baba hutengwa hasa uzeeni
 
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
Kuna wanawake hasa hasa wanaoringa ujanani wamevaa ringi tena hufikia hatua ya kuwatenga mashostio wasiovaa Ringo,

Yaani wananyenyekea ndoaa ili kuwaonesha jamii,, ngoja Mzazi mwenzie spate kilema au astaafu ndo utajua rangi zao.
 
Niwe tu mkwel wamama aanapenda kujikweza mbele ya watoto utasikia baba enu hajatoa pesa ya ada kumbe !!! Pesa kapewa anacheza tu mind game na watoto na baba akizubaa anaweka full mzigo kabisa "nawasomesha kwa pesa zangu bila aibu "
 
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
Inawahusu waliohamia Dodoma
Acha Niende Kondoa Sehemu Inaitwa Mauno
Nikakate Mauno Huko Huko
 
Kuna wanawake hasa hasa wanaoringa ujanani wamevaa ringi tena hufikia hatua ya kuwatenga mashostio wasiovaa Ringo,

Yaani wananyenyekea ndoaa ili kuwaonesha jamii,, ngoja Mzazi mwenzie spate kilema au astaafu ndo utajua rangi zao.
Ndo maana wanasemaga mke mwema hutoka kwa bwana
 
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
Kwann umesema hivi mkuu? Elezea vizuri nipate point yako huenda kuna funzo hapo.
 
Back
Top Bottom