Usimwachie mkeo nyumba zaidi ya miaka 5 peke yake

Usimwachie mkeo nyumba zaidi ya miaka 5 peke yake

Wale mliozaa na kusomesha mpaka watoto wamepata kazi na kuoa /olewa.
Sasa baba akapata uhamisho wa kikazi akahama mkoa, mke akamwachia nyumba na mtoto mmoja labda ila wengine wameshaoa.
Kwa bahati mbaya baba kazi zake ni nyingi kiasi anashindwa kurudi weekend nyumbani, miaka imekata zaidi ya 5 na mke ameshazoea kukaa mwenyewe.

Ikumbukwe kabla hujahama kikazi mliishi wote na mmelea mpaka kuozesha / kuozeshwa watoto ndio ukahama. Sasa kwakuwa mke alishazoea kuwa underground no power na watoto wanalijua hilo,, kosa linakuja pale utakapo muacha mkeo ajitanue zaidi ya miaka 5 anakuwa keshajijengea power anasahau wajibu wake.

Madhara yatakuja kama hivi,,

1) mama atasikilizwa sana na watoto (hapo ndio mwanya wa kusemea kuwa baba enu kaniterekeza) kumbe anatafuta huruma, na kwakuwa mlikaa nae kipindi kabla hamjaoa / olewa mnakumbuka busara na jinsi alipokuwa mnyenyekevu kwa baba hivo hata atakachosema chochote kuhusu Baba kwenu watoto jiwe kibaya /kizuri lazima mkiamini.

2) kwa sababu ameshatanuka power atatawala na ndio ndugu zake watatawala nyumba yako kiasi kwamba hata kama Unataka kurudi kwako unahisi kama vile Unaenda ukweni. Unajikuta una ahirisha.

3)chuki baina ya baba na watoto,, kama kawaida mama ataanza kuwapa sumu ya maneno watoto ili tu wamtenge baba na pesa za kifuta jasho cha wazazi mama ndio awe anatumiwa,, hapo ndio muda mwingi watakaoutumia kuongea kwenye simu ya kumteta baba na namna ya kumuweka mbali na upendo wa watoto (wakati haya yote mtoto ataburuzwa kwa sababu aliondoka nyumbani kipindi baba na mama waliishi wote na mama alikuwa mnyenyekevu nyote mnajua,,) kumbe maisha baada ya watoto kuoa na baba kuhama kikazi yalibadirika.

3)Baba na mama hapa watafikia mda mama hata simu kupokea ya baba ni kazi vituko na ubabe mama atavionesha hadi kwa mawifi na mashemeji baba akijaribu tu kuwaambia watoto wake mama yao anacho Fanya ataambulia kununiwa na hata kumblock watatamani

4)kusambaa kwa ndugu wa mwanaume, kwa sababu mama ameshajijenga power amejaza ndugu zake kwa bahati mbaya amewajaza kiburi nao, sasa itokee tu Dada wa mwanaume amekuja kusalimia hapo nyumbani kama ilikuwa alale wiki ataenda guest na atageuza siku ifuatayo kijijini.

5)mwisho na la msingi itokee baba anastaafu anataka arudi nyumbani kwake hapa mke huwa hataki kabisa na anatamani utafte mahala ujifiche ila usirudi nyumbani,, kwanini?

Kwa sababu ameshajipower si kwa majirani, ndugu pande zote mpaka ukweni hivo kurudi kwako kutaleta msiba kwake airudie ile hali ya kukunyenyekea hatoweza,, kuwafukuza ndugu zake aliowajaza ndani huku wakimlamba miguu na yeye akiwaonesha ufalme atashindwa.

Sasa hapa mama huyu anafanyaje? Atafanya figisu baina yako (baba) na wanao kama alikuwa anaishi na mtoto wenu wa mwisho ( kwa bahati hajafanikiwa kimaisha bado yupoyupo tu) atamtumia huyo mtoto kukuonesha jeuri ili ushindwe kurudi nyumbani, ukijaribu kuwatafta watoto waliooa uwaambie hayo mauzauza wao hawatokuamini kwa sababu kabla hawajaoa picha walilo nalo la mama yao alikuwa mnyenyekevu, Mwisho wa siku baba anaambulia upweke hana msaada ndugu zake nao wamekimbizwa kipindi kaka yao alipokuwa nje kikazi, kiasi kwamba ukijaribu kuwatafta ndugu nao uwaelezee wakutatulie tatizo nao wanakukwepa wanamwogopa mkeo.

NB: ukihamishwa kikazi beba mkeo asipate mwanya wa kuujua ufalme (power).
Kwa Mwanaume mwenye akili anajua haya, na lazıma ahakikishe anazaa watoto wachache unasomesha, mapema na una save pesa yako na unawekeza, ukifanya hivyo Mwanaume hufi mapema
 
Kuna wanawake hasa hasa wanaoringa ujanani wamevaa ringi tena hufikia hatua ya kuwatenga mashostio wasiovaa Ringo,

Yaani wananyenyekea ndoaa ili kuwaonesha jamii,, ngoja Mzazi mwenzie spate kilema au astaafu ndo utajua rangi zao.
Hasa hao wanawake wanaojionyesha ndio matatizo kabisa, yuko kwa mission ya kupata pesa akiona haifanikiwi au Mume pesa imeyumba utasikia alikua na malaya kibao, na kashakimbia. Wanaume kaeni nao kwa akili usiwekeze pesa yako yote kwa mwanamke.
 
Wanawake tuna tabia ya kushindana hasa mkiwa na uke wenza ndio inakuwa zaidi, haiwezekani wote mkamtelekeza Kuna atakaejipendekeza kwa mwanaume ili aonekane bora hivyo inakuwa ndo pona pona ya mwanaume husika, na ikiwa hivyo wengine nao wataiga tu hawatokubali kumuachia ushindi kizembe hivyo mwenzao
Ushindani upo sababu yupo kazini
 
Kuna mfano mmoja baba na mama wote ni MOD( Madawa ) sasa shida ni mmoja mwanaume baada ya kuona mke naye anapata pesa na nini aka acha kutoa ada. Timbili lake sio la kitoto.
Kwa uwelewa wangu mdogo pesa utayo pata mwanaume, hawa viumbe wanataka waione inavo tumika lakini pesa yake haikuhusu
Niwe tu mkwel wamama aanapenda kujikweza mbele ya watoto utasikia baba enu hajatoa pesa ya ada kumbe !!! Pesa kapewa anacheza tu mind game na watoto na baba akizubaa anaweka full mzigo kabisa "nawasomesha kwa pesa zangu bila aibu "
 
Pamoja na kuoa wake wengi

Kisanga kinabaki palepale tena itakuwa zaidi maana kila mwanamke anavuta mtoto kwake tena zile hasira za kwamba kaenda kulala kwa mke mdogo zinahamia kwa watoto na kuwajaza ujinga.

Vita inapamba moto mpaka unazeeka
Usinikumbushe babu yangu alipo fariki mke mdogo alikimbilia kuuza nyumba yaani kafa leo kesho kutwa yake nyumba inauzwa.
Na pia nakumbuka nilivo kuwa katoto kadogo nilienda jikoni kuomba samaki si unajua utoto tena yule bimdogo kafanya kusudi kuni nyima ila angekuwa mwanaye ange mpa. Dawa ya hawa viumbe ni kuishi nao kwa akili. Usikubali wakutawale
 
Kuna na watoto wachache sio sababu. Point ni moja tu Oa mwanamke mwenye hofu ya Mungu. Akiweza kukusikiliza baasi ushamteka huyo
Kwa Mwanaume mwenye akili anajua haya, na lazıma ahakikishe anazaa watoto wachache unasomesha, mapema na una save pesa yako na unawekeza, ukifanya hivyo Mwanaume hufi mapema
 
Kuna na watoto wachache sio sababu. Point ni moja tu Oa mwanamke mwenye hofu ya Mungu. Akiweza kukusikiliza baasi ushamteka huyo
Asilimia kubwa ya wanawake hawana hofu ya Mungu, wana holu ya kulinda maslahi yao, Ukiona mwanamke anakimbilia kwenye dini,wazazi,mafundisho ya dini, Ndugu,marafiki, wasimamizi wa ndoa, viongozi wa dini, anachotaka hapo ni agenda yake ya kumiliki mwanaume ikamilike. Mwanamke mwenye akili anahakikisha anaelewa malengo ya MUME wake ktk maisha, na anakua msaidizi wake ktk kuyafikia hayo malengo na kama malengo sio mazuri au ni madogo basi mwanamke anakua mshauri kwa Mwanaume ili kurekebisha, Ni kama ilivyo kwenye kazi huwezi mlazimisha Boss wako kufanya jambo ila ukiona ni Nzuri na linafaida unamshauri kwani unajua hasara ikitokea na wewe utaathirika kwani hata kazi utakosa na kipato kitakosekana
 
Wamama si unawajua vizuri?
Mkuu wanawake wana vitimbi na hivyo ndivyo walivyoumbwa hilo ni moja ya mapungufu yao , sasa kama umeshalijua hilo unatumia hekima tu msikilize halafu maamuzi fanya kwa hekima maana hata kama kweli mzee alimtenda(hapa wanaume huwa tunazingua kweli ) mtafute mzee kwa muda wako ongeeni malizeni huko huko yeye ni mzazi hata kama hatakuomba msamaha direct ila kwa reaction tu utaelewa.

Halafu saidia wote bila ubaguzi ,mama akisafiri sijui anakuja kukutembelea aje na mzee akishindwa tumia mzee nauli waje wote maanaa utaitwa baba pia na wewe yatakukuta tu simple kama hivyo na kwa wale wenye dini pia kuwasaidia wazazi ni moja ya njia ya kuongeza baraka na umri pia unapata thawabu.
 
Uko sahihi Kiongozi, hasa kwa watoto Wakiume kuna mtihani kwani wakina mama Wengi wanajitahidi kukuambia mabaya ya Baba tu, na la kwanza ni Baba yenu anaharibu pesa na malaya, ni mlevi nimewalea kwa shida, usijeingia kwenye huo mtego. Baba ni muhimu sana kwenye maisha na ukimfanya rafiki akakufundisha maisha utatoboa Baba wanajua na wanauzoefu mkubwa kwenye kutafuta maisha, Angalia ktk rafiki au Ndugu, wale ambao wako karibu na Baba zao wako vizuri kimaisha hawakosei target zao.
 
Huu ni ukweli mtupu mkuu , wanaokuwa violeted ni baba zetu sana ila kwa sababu hawei toka akatangaza basi jamii huwa haioni hilo.

Binafsi nina balance kila kitu hakuna sijui mama hiki mama kike sijui nini sina hiy kitu walikosana huwa namuambia tu hayo mtajadili nyie kama wazazi si hekima mimi kuingilia mambo yenu.

Tuwasikilize wazazi lakini tutumie hekima sana kwenye maamuzi aisee wazazi wa kiume wanateswa pia.
 
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
Naomba uongeze nyama kwenye hii comment...kuna kitu nataka kujifunza
 
Kwa Mwanaume mwenye akili anajua haya, na lazıma ahakikishe anazaa watoto wachache unasomesha, mapema na una save pesa yako na unawekeza, ukifanya hivyo Mwanaume hufi mapema
Mzee uko sahihi ndo wanavyofanya wenzetu ngozi nyeupe
 
  • Thanks
Reactions: Lob
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
Agiza chochote kwa mangi naja kulipa

Mkuu upate ulinzi harak iwezekanavyo!!
 
Na hii hali inawakumba wanaume wengi tu, mi ningekuwa mwanaume nisingewekeza nguvu zangu zote za ujana kwa mwanamke mmoja, hiyo Ni Kama kujichimbia kaburi, Kuna wanawake Ni mafia, ningeoa mmoja ila ningezaa na zaidi ya mmoja, ama ningeoa zaidi ya mmoja
Noelia, Noelia Noelia, nimekuita mara tatu😳😳😳
 
Back
Top Bottom