Usinunue iphone 13

Usinunue iphone 13

Hoja hapa sio kwa mwenye uwezo huyo aendelee.. ila mtu ni mkataufuta anaungaunga tu lisimu la bei ya mradi wa maana unaoleta fedha nyingi la nini si anunue simu simple tu hiyo fedha awekeze!?
Kwa mtu asiye na uwezo wa kununua iPhone, kama ananunua ili aonekane anayo wakati muda mwingi iko offline hana bundle au anatuma sms za please call me au kukopa salio huyo kwa kweli nakubaliana na wewe. Na anadhalilisha brand.
iPhone haitakiwi kuwa haina salio! Au haina Internet!
Sasa kama issue ni SMS na calls tu gharama kubwa ya nini, chukua kitorch.
 
Hebu tuache wenye hela zetu zipate matumizi dogo
Kwani kuna mahala nimesema hela za mtu zisitumike ama nimezuia watu kutumia hela zao?

Kwa ulichokiandika mimi na wewe nani dogo? Umedhihirisha wazi kwamba wewe ni dogo kiakili, hata kama ukiwa mkubwa kiumri basi ni kubwa jinga.
 
Hizo simu wapo watu wa aina nne..
1. Wale wanaojua kwanini inauzwa bei kubwa na wapo tayari kuilipia ili wapate kilichomo humo

2. Wale wanaojua kwanini inauzwa bei kubwa na hawapo tayari kulipia sababu hawana matumizi na kilichopo humo

3. Wale wasiojua kwann inauzwa bei kubwa ila ni watu wa mkumbo, fashion na wapo tayari kupoteza mengine ili awe nayo lakini hana matumizi ya msingi zaidi ya picha picha video na upuuzi unaofanana na hayo.

4. Wale wasiojua kwann inauzwa bei kubwa, wanashangaa kwann iuzwe hiyo bei.

Lifahamu kundi lako.
Sipo kwenye makundi yote mbona!
 
Watumiaji wa i phone ni wajinga wajinga sana
utasikia natumia i phone kwa ajili ya security
ukimuuliza anachoficha nini
hana zaidi za meseji za umalaya
ni wajinga tu
[emoji12][emoji12][emoji1787][emoji1787] Tatizo kuiga mkuu, kwenye maisha kama hujakaa chini na kuweka your own standards & guiding principles wewe utaishia kuruka ruka kama kitenesi to whichever you see...
 
Kwa mtu asiye na uwezo wa kununua iPhone, kama ananunua ili aonekane anayo wakati muda mwingi iko offline hana bundle au anatuma sms za please call me au kukopa salio huyo kwa kweli nakubaliana na wewe. Na anadhalilisha brand.
iPhone haitakiwi kuwa haina salio! Au haina Internet!
Sasa kama issue ni SMS na calls tu gharama kubwa ya nini, chukua kitorch.

Walisema wapi hayo maneno?
 
Aisee nyie ndo mnaojua kutumia simu, yaani hivyo vitu unavyovitaja sina hata kimoja ninachokizingatia. Hiyo camera yenyewe ninaweza kukaa mwezi sijajipiga picha, yaani mtu kama mimi kununua simu ya million ni kufuata mkumbo tu [emoji3]
Umeona hoja uliyoongea kiongozi yaani unaweza kuta hata hiyo high quality camera huna matumizi nayo kihivyo, sasa nini sasa linakuwa lengo la eti kununua simu ya milioni nne kwa kigezo cha camera? Kwani wewe ni muandishi wa habari? Kwani wewe ni professional photographer? Narudia tena tatizo ni kufuata mkumbo full stop.
 
Kaazi kweli,si bora nikununulie infinix na passo au vitz,au unaonaje hiyo
Hizo ndizo real priorities za maisha... Hapo una kausafiri kako hata kama unafuga kuku una uwezo wa kubeba kuku 20 ukampelekea mteja kwenye sherehe fasta, na hapo hapo simu ya kuwasiliana na wateja wako unayo. Siku umeshikwa na tumbo la kuhara na kutapika mpangaji mwenzio au rafiki yako fasta anatumia kigari chako kukukimbiza hospitali badala ya kuhangaika na boda boda au daladala...
 
Back
Top Bottom