Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Watu wengi hupenda kununua vitu vya thamani na kuishi navyo kwenye nyumba za kupanga (nyumba za wanaume wenzao, waliojinyima na kuweka mijengo).

Kufanya hivyo, kunawafanya watu wengi kuishi muda mrefu kwenye nyumba za kupanga, na kusahau kujenga nyumba zao.

Utakuta mtu ana kipato kizuri; lakini utashangaa atakimbilia kununua gari, music system ya gharama, tv kubwa ya gharama n.k, na hivyo vyote anavipaki kwenye mjengo wa mwanaume aliyejinyima na kutimiza ndoto zake.

Inapotokea kipato kimeyumba, na kushindwa kujikimu kwenye kodi ya pango; wanakosa sehemu ya kwenda kuvipaki vitu walivyovinunua kwenye nyumba ya kupanga; matokeo yake ni kuanza kuviuza kwa bei ya hasara.

Ushauri; kwenye nyumba za kupanga, weka godoro, kitanda na vitendea kazi vya kupikia tu.

Salio linalobaki; nenda katafute kiwanja ujenge
 
Hayo ni maoni yako.usitake kila mtu aishi maisha unayoishi.wengi waliishi maisha ya kupanga na vitu vyao vya dhamani na walipojenga wakahama navyo.inaonyesha umeishi maisha ya kulelewa.hujawai kupanga chumba
 
Back
Top Bottom