Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Watu wengi hupenda kununua vitu vya thamani na kuishi navyo kwenye nyumba za kupanga (nyumba za wanaume wenzao, waliojinyima na kuweka mijengo).

Kufanya hivyo, kunawafanya watu wengi kuishi muda mrefu kwenye nyumba za kupanga, na kusahau kujenga nyumba zao.

Utakuta mtu ana kipato kizuri; lakini utashangaa atakimbilia kununua gari, music system ya gharama, tv kubwa ya gharama n.k, na hivyo vyote anavipaki kwenye mjengo wa mwanaume aliyejinyima na kutimiza ndoto zake.

Inapotokea kipato kimeyumba, na kushindwa kujikimu kwenye kodi ya pango; wanakosa sehemu ya kwenda kuvipaki vitu walivyovinunua kwenye nyumba ya kupanga; matokeo yake ni kuanza kuviuza kwa bei ya hasara.

Ushauri; kwenye nyumba za kupanga, weka godoro, kitanda na vitendea kazi vya kupikia tu.

Salio linalobaki; nenda katafute kiwanja ujenge
Wee una akili Sana tunaweza kuwa washkaji

Alfu kingine umepanga alfu unaenda mliani cty kununua simu ya laki Tisa milioni. HV nmtu huna vya kufanya mpk kufanya hvyo
 
Watu wengi hupenda kununua vitu vya thamani na kuishi navyo kwenye nyumba za kupanga (nyumba za wanaume wenzao, waliojinyima na kuweka mijengo).

Kufanya hivyo, kunawafanya watu wengi kuishi muda mrefu kwenye nyumba za kupanga, na kusahau kujenga nyumba zao.

Utakuta mtu ana kipato kizuri; lakini utashangaa atakimbilia kununua gari, music system ya gharama, tv kubwa ya gharama n.k, na hivyo vyote anavipaki kwenye mjengo wa mwanaume aliyejinyima na kutimiza ndoto zake.

Inapotokea kipato kimeyumba, na kushindwa kujikimu kwenye kodi ya pango; wanakosa sehemu ya kwenda kuvipaki vitu walivyovinunua kwenye nyumba ya kupanga; matokeo yake ni kuanza kuviuza kwa bei ya hasara.

Ushauri; kwenye nyumba za kupanga, weka godoro, kitanda na vitendea kazi vya kupikia tu.

Salio linalobaki; nenda katafute kiwanja ujenge
Sasa mkuu haya maisha tunayoishi si tupo safarini? Sasa kwahiyo tujenge njiani???
 
Huyu jamaa ndio wale akiona mwenzake kanunua gari utaskia mi siwezi kumiliki gari kabla sijajenga unakuta anaacha kula vizuri kila siku anakula pembejeo (maharage) kwasababu hajajenga.
Kwa mtazamo wangu mdogo maisha yanahitaji akili na mipango na sio kujinyima au kuishi kimaskini.
Kuna wanaoishi kimaskini wanajibana na bado hawatoboi na kunawanao ishi kimkakati hawajibani wala nini na wametoboa wana majengo yao.
 
Msingi wa hoja yako umeegemea kwenye matumaimi "hope " kwamba kuna siku kila mtu atamiliki nyumba yake, je hujui kuwa watu hutofautiana vipato, malengo hats majkumu?Yaani niache kula vzuri mgahawani kwa matumaini kuwa nkifika kwangu nd nile vzuri? Wake up bro.
 
Paragraph ya mwisho inatosha kabisa kujua how bright you are... nimeipenda hiyooo
 
Huwa nawachora tu wanaokimbilia ardhi au viwanja
Dunia kubwa hii mazee.
Relax fanya maisha.
Unapata hela kidogo unawaza kujenga hahahaa.

Ishi kwanza halafu ujue ili ukamilishe kitu cha maana Kama nyumba Jenga kidogo kidogo utashangaa!

Muda huo unajenga hakikisha haupandi daladala kwenda site, unakitu ya kuingizA pesa daily na haujachakaa wewe mwenyewe
 
Msingi wa hoja yako umeegemea kwenye matumaimi "hope " kwamba kuna siku kila mtu atamiliki nyumba yake, je hujui kuwa watu hutofautiana vipato, malengo hats majkumu?Yaani niache kula vzuri mgahawani kwa matumaini kuwa nkifika kwangu nd nile vzuri? Wake up bro.
Ahahahah na unaweza kwako usifikie pia ukazima an...
 
Back
Top Bottom