Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Masikini wanaishi kitajiri ndiyo maana wanazidi kuwa masikini, na matajiri wanaishi kimasikini na ndiyo sababu wanazidi kuwa matajiri. Hapa hatupangiani maisha ila ukweli lazima usemwe. Follow the road less traveled. Mkuu Equation x umeeleweka vema. Mwenye masikio na asikie.
 
Ktk hili ouna mitazamo tofauti kulingana na familia tunazotokea.

Binafsi, kwa mazingira nikiyokulia nasapoti hoja ya mtoa mada. Familia zetu nyingi zimetokea ktk umaskini na upangaji wa kudumu kwa miaka mingi.

Sasa ili kuvunja hizi circle kuna haja kijana ukipata upenyo fikiria kujenga na si kuishi kwa extravagance.

Maana yake utawafanya wanaokuja ktk familia yako hata kama watakuwa na shida hawatorudia duara lako la shida na kudhalilika. Na hii ni kitu cha msingi.

Ninapotokea nina mifano mingi ambayo vijana wanapotoboa huwa wanawaza kukamata ardhi kwanza.

Kwa wale ambao wapo maeneo kama DSM wanaona jinsi wazaramo wanavyo vimba kwa ajili ya umiliki wao wa ardhi ya kurithi.

Katika suala hili majibu na mitazamo hailingani kulingana na mazingira, makuzi, changamoto, vipato au uzoefu tulionao.

Salaam Aleikhem
Waleikh Msalaaam
 
Wahindi na waarabu wanakaa upanga na masaki wanasomesha watoto ulaya na vacations za dubai kila mwezi huku benki salio limejaa ila bado wamepanga. Ni mtazamo tu wa kimaisha.

Ukisimamisha mambo yote kwenye maisha ikiwemo furaha yako ili upange matofali ni akili ya kimaskini. Pale ulipo kwa muda huo ishi vilivyo ipe raha familia. Jenga ukiwa comfortable ila usiache kuishi.
 
Back
Top Bottom