Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Usinunue vitu vya thamani kwenye nyumba ya kupanga, kabla hujajenga kwako

Hayo ni mawazo yako, kila mtu ana formula yake ya kuishi.

Nilianza kupanga nkanunua tv kali, na furniture za maana, nkaja nkanunua gari then nkajenga kama kawaida.

So usiwapangie watu maisha yao
 
Wee una akili Sana tunaweza kuwa washkaji

Alfu kingine umepanga alfu unaenda mliani cty kununua simu ya laki Tisa milioni. HV nmtu huna vya kufanya mpk kufanya hvyo
Weee nawe kwahiyo ambao hawajajenga hawapaswi kwenda (mliani city) mlimani city kununua simu ya laki Tisa? Watu wana vitu zaidi ya hivyo wanaishi vizuri kuzidi hata waliojenga
 
Hiyo dhana yako kwamba kila aliyejenga alijinyima, ni dhana potofu ya mrengo wa kimasikini. Kuna watu wamejenga/wanajenga huku wanaendelea kula bata. Kwahiyo unaweza ukaishi kifahari nyumba ya kupanga na bado ukajenga nyumba yako. Nadhani itakushangaza sana kusikia kuna mtu ana mjengo mkali tu maeneo ya Mbezi beach lakini yeye anaishi nyumba ya kupanga Sinza. Wapo wengi tu, ila wewe swala la kujenga na kupanga unalihusisha sana na umasikii wako. Wakati wa kutoa ushauri jaribu kuweka matatizo yako pembeni ndio utoe ushauri, utasaidia wengi.
 
Nyie ndo wale wenye nyumba mnaotegemea kodi kuishi, mnakuaga wanoko, wambea, wachunguzi,
Mnamchunguza Mpangaji wako kapika nini uombe au kanunua nini upandishe bili ya umeme,

Kama nyumba yako uliyojinyima ni kila kitu anza kula matofali msiwakere wapangaji.
kuna watu hapa bongo hudhan nyumba ukiwa nayo umemaliza kila kitu! Nyumba ukiwa nayo kama huna kijaza kipato shida ziko pale paleee,

Mm naamini katika mzunguko wa biashara na ujazo wa account baasi.
 
Mahali popote unatakiwa kuishi vizuri uwe anapanga au la .Kwa hiyo.ukipanga unatakiwa kulala kwenye mkeka?

Mleta mada huna akili wahindi ni matajiri tena mno watoto wanasomesha Ulaya na Marekani lakini Miaka yote wataishi nyumba za kupanga za National Housing

Una vimawazo vya kimaskini na pepo la umaskini
 
Watu wengi hupenda kununua vitu vya thamani na kuishi navyo kwenye nyumba za kupanga (nyumba za wanaume wenzao, waliojinyima na kuweka mijengo).

Kufanya hivyo, kunawafanya watu wengi kuishi muda mrefu kwenye nyumba za kupanga, na kusahau kujenga nyumba zao.

Utakuta mtu ana kipato kizuri; lakini utashangaa atakimbilia kununua gari, music system ya gharama, tv kubwa ya gharama n.k, na hivyo vyote anavipaki kwenye mjengo wa mwanaume aliyejinyima na kutimiza ndoto zake.

Inapotokea kipato kimeyumba, na kushindwa kujikimu kwenye kodi ya pango; wanakosa sehemu ya kwenda kuvipaki vitu walivyovinunua kwenye nyumba ya kupanga; matokeo yake ni kuanza kuviuza kwa bei ya hasara.

Ushauri; kwenye nyumba za kupanga, weka godoro, kitanda na vitendea kazi vya kupikia tu.

Salio linalobaki; nenda katafute kiwanja ujenge
Wazee WA ready made misifa[emoji2]
 
Bwanyenye aliyeweka mjengo pale Magogoni hakuondoka nao na alikufa, huo mjengo unachezewa na kina SSH & Mr born town, laiti angejua asingeujenga ili kuwajengea kina old CEO na wapambe wake 😄

Ni upuuzi kujenga nyumba ambayo hautaenda nayo kaburini, kupanga ndio habari ya mjini tunakula maisha bila kuwaza mijengo ambayo tukifa hatuta ondoka nayo.

Usitupangie bwashee!
 
Back
Top Bottom