Ktk hili ouna mitazamo tofauti kulingana na familia tunazotokea.
Binafsi, kwa mazingira nikiyokulia nasapoti hoja ya mtoa mada. Familia zetu nyingi zimetokea ktk umaskini na upangaji wa kudumu kwa miaka mingi.
Sasa ili kuvunja hizi circle kuna haja kijana ukipata upenyo fikiria kujenga na si kuishi kwa extravagance.
Maana yake utawafanya wanaokuja ktk familia yako hata kama watakuwa na shida hawatorudia duara lako la shida na kudhalilika. Na hii ni kitu cha msingi.
Ninapotokea nina mifano mingi ambayo vijana wanapotoboa huwa wanawaza kukamata ardhi kwanza.
Kwa wale ambao wapo maeneo kama DSM wanaona jinsi wazaramo wanavyo vimba kwa ajili ya umiliki wao wa ardhi ya kurithi.
Katika suala hili majibu na mitazamo hailingani kulingana na mazingira, makuzi, changamoto, vipato au uzoefu tulionao.
Salaam Aleikhem
Waleikh Msalaaam