Usiombe kuacha kazi kisa Forex. Nilivyofilisika na kukimbilia kijijini Tabora

Nilikuwa nimechoka na maisha ya kufanya kazi saa nane kwa siku katika ofisi flani hivi pale posta jijini Dar es Salaam. Ndoto yangu ilikuwa kubwa zaidi kuliko kiti changu cha ofisini na mshahara wangu wa kila mwezi. Nilikuwa na hamu kubwa ya kujaribu kitu kipya, kitu ambacho kingenipa uhuru wa kifedha na fursa za kutimiza ndoto zangu.

Nilitambua kwamba kwenye ulimwengu huu wa kisasa, forex ilikuwa njia inayopendelewa zaidi ya kuwekeza na kupata faida kubwa. Nilivutiwa na hadithi za watu waliojikomboa kutoka kwenye mikono ya ajira na kuwa mabosi wa maisha yao wenyewe kupitia biashara ya forex. Hivyo basi, niliamua kuwa mmoja wao.

Nilipofikiria juu ya kuacha kazi yangu na kujitosa kwenye ulimwengu wa forex, moyo wangu ulijaa msisimko na wasiwasi. Nilisoma vitabu vingi na kujiandaa kwa miezi kadhaa kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho. Nikaamua kuwa huu ndio wakati wangu wa kujaribu kitu kipya, wa kujiletea mabadiliko kwenye maisha yangu.

Kuacha kazi haikuwa uamuzi rahisi, lakini nilihisi kwamba huu ndio wakati sahihi wa kujitolea kwenye safari ya forex. Nilijiandaa kihisia na kifedha, nikiwa na matumaini kwamba ningeweza kugeuza ndoto zangu kuwa ukweli. Niliamua kufungua akaunti yangu ya forex na kutumia akiba yangu kama mtaji wa kuanzia. Safari yangu ya kuelekea uhuru wa kifedha ilikuwa imeanza.

Husikose sehemu inayofuata ...
adriz aliuza hadi kiwanja
 
Kuna kitu itakua ulikosea mkuu, ni PM nikuelekwze jinsi ya kuanza tena
 
tunaobet kuna kitu kinaitwa casino games. kwenye casino games kuna play for free (hii ni kama demo kwenye forex). kwenye play for free unapoplay unakula kirahis tu, unaona yes, kumbe simpo, nikiingia kwenye game yenyewe nakula tu. ingia sasa uone, utaliwa mpaka uchakae.

ndivyo ilivyo kwenye demo ya forex. kwenye demo mambo yanakuwa yanakuendea fresh tu, ingia kwenye account halisi sasa uone balaa lake. hizi biashara za trading ni pasua kichwa, asilimia kubwa zipo kwa ajili ya kunufaisha makampuni yanayoendesha hizi biashara. tupo tunatrade kwasababu tumeshaingia tumepoteza hela nyingi, tunaamini ipo siku tutarudisha hela zetu au kupata faida kubwa kwa mara moja.
 
Back
Top Bottom