Usiombe ukutane na mwanafunzi wa IT mwaka wa kwanza

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Aisee ikitokea umekutana na mwanafunzi wa IT mwaka wa kwanza wengi ni much know.
Niko na dogo hapa kamaliza mwaka wa kwanza anasoma masuala ya security yani yeye kila kitu anasema anaweza hack iwe gmail, wi-fi, mitandoa ya simu atumie net bure, anakwambia gmail haiko secure, instagram anaweza kuhack.
Basi mimi namchora tu na kumkubalia.
Kila anachoona kwenye computer anasema usitúmie hicho tumia hiki ananitajia softwares ambazo si maarufu ili mradi vurugu tu.
Hapa kaniambia nisitumie chatgpt haina performance nzuri nitumie sijui flick.
 
Mpe muda aki-graduate na GPA ya 1st Class afu asipate kazi ndo atajua Dunia hada walimwengu shujaa!
 
mwaka wa kwanza kila mwanafunzi anataka kutengeneza na kumilliki softwares kama Elon musk,Mwisho wa siku wakihitimu wakija mitaani hawawezi hata ku develop web-sites
 
Mpe muda aki-graduate na GPA ya 1st Class afu asipate kazi ndo atajua Dunia hada walimwengu shujaa!
Umeniwahi na hii comment. Amsubiri Makumbusho kwenye maduka ya iphone baada ya ku graduate.

Atamkuta kafuga ndevu zilizopakwa super black. kisuruali kimembana kinaishia juu ya kiwiko, maneno mengi ya kudalalia iphone. Hapo hatowaza hata ku hack account yake yeye mwenyewe.
 
mwaka wa kwanza kila mwanafunzi anataka kutengeneza na kumilliki softwares kama Elon musk,Mwisho wa siku wakihitimu wakija mitaani hawawezi hata ku develop web-sites
Ananiambia achana na gmail, namwambia mimi gmail hii email naitumia toka niko kidato cha 2 zaidi ya mika 15 iliyopita na niliipenda kwa sababu ya simple user UI nikaachana na Yahoo. Akaniambia mnaitumia kwa sababu ni maarufu ila hakuna kitu ni css tu hiyo. Mimi nacheka tu
 

🙂🙂🙂Mshikishe adabu mwambie ahack Instagram akaunti yoyote aibadili jina
 
🙂🙂🙂Mshikishe adabu mwambie ahack Instagram akaunti yoyote aibadili jina
Mkuu hata sibishani naye kila kitu mimi namkubalia. Maana yuko bsy anachapa code za python hapa anasema akimaliza anataka atengeneze file zake za kupenetrate mtandao wa voda sasa alikuwa hajaijulia vzuri python likizo hii ndipo ameamua kupambana nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…