Wakuu lazima tukubaliane kuwa maisha yamebadilika sana kuanzia vijijini hadi mijini. Na mabadiliko yametokea ghafla. Ujio wa bodaboda na mabadiliko makubwa ya teknolojia kama uwepo wa mitandao ya kijamii na mobile money umepunguza ugumu wa kazi nyingi. Urahisi wa kufanya kazi nyingi pia nao umekuja na changamoto za kiafya hasa unene na magonjwa yasiyoambukiza hali inayofanya tujikite kwenye mazoezi.
Zamani kutokana na kutokuwepo usafiri ilikuwa kawaida mtu wa Karatu mjini kutembea kwa mguu hadi kijiji cha Geykrum Lambo kufanya jambo lake kisha kurudi tena town. Hapo ni zaidi ya 10km. Mtu kama huyu hata ale chapati 8 kwa siku ilikuwa ngumu kunenepa kirahisi. Hata Arusha mtu alikuwa anatoka Kwa Mromboo hadi Mkonoo kwa mguu kutokana na kutokuwepo kwa usafiri. Kimsingi shuguli nyingi za siku zilikuwa sawa na kufanya mazoezi tena makali. Vibonge walikuwa wachache mno.
Kutokana na urahisi uliopo ninawasihi ndugu zangu tufanye sana mazoezi kutunza afya zetu. Vinginevyo tutakuwa misukule ya hawa wanaharakati uchwara mitandaoni wanaosema tusile ugali, wali, asali, matunda, wala kunywa maji ya bomba. Mazoezi ya kukimbia na gym ni muhimu sana ili uwe huru na maisha yako. Zoezi litalinda mwili wako na kukuweka fit pia mwonekano mzuri.