Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

Daaah! Huu ndiyo mchango wako kwenye thread hiii!!?
Huwa nawajibu ninavyotaka kama wanataka michango ya harusi sina labda michango ya minyoo,maana nachoka na simu,huku wanataka uwe mjumbe wa kamati,wengine michango tena asubuhi tu simu hizi.Nilishawaambia huwa sichangii michango ya harusi,nitachangia elimu na afya
 
Hii kero ilisababisha nikalimit wasap yangu kuungwa magroup bila ridhaa yangu ..haiwezekani mtu akurupuke tu mara kakuadd group la harusi watu wanaplij mule malaki huko badala yake unabaki kushangaa ukiulizwa unatoa sh ngapi.

Kiustaarbu nipe taarifa nijipange nione naweza support kiasi gan na aio niungwe kwa group la michango.
Kero nyingine mtu kukupigia siku akiwa anahitaji pesa yako kufanikisha jambo lake tena wasivyo na haya si ajabu hata katika harusi yako hakuchanga japo alijua kabisa.
 

KAMA MARAFIKI ZAKO ULIWAOMBA MICHANGO WAKUCHANGIE KATIKA HARUSI YAKO WAKAKUCHANGIA IMEFIKA ZAMU YAO HUTAKI KUWACHANGIA ..........UKISIKIA UCHAWI BASI HUU NDO UCHAWI
 
Weka settings ambayo hairuhusu kuungwa kwenye group bila ruhusa yako.. hiyo imenisaidia sana .. kwani hapo mwanzo nilikuwa najikuta tu tayari ndani ya group sasa hivi inakuja link ni accept au la
 
Na kuna watu wanadai kama Deni, sms mfululu mpaka unajisemea huyu mtu mzima kweli! Mbaya zaidi mtu anakuchangisha mchango wa harusi ya mtu hata usiyemjua!
 
Tatizo ni pale unachangishwa hadi michango ya harusi ya Mjomba wake na rafiki yako duh!
KAMA MARAFIKI ZAKO ULIWAOMBA MICHANGO WAKUCHANGIE KATIKA HARUSI YAKO WAKAKUCHANGIA IMEFIKA ZAMU YAO HUTAKI KUWACHANGIA ..........UKISIKIA UCHAWI BASI HUU NDO UCHAWI
 
Nzuri sana hii
Weka settings ambayo hairuhusu kuungwa kwenye group bila ruhusa yako.. hiyo imenisaidia sana .. kwani hapo mwanzo nilikuwa najikuta tu tayari ndani ya group sasa hivi inakuja link
 
Mimi mpaka muda huu yapo ma group ma 3 😊😊 mzee nakumbuka KAULI za wahenga """"KUTOA NI MOYO"" SI UTAJIRI..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…