Usipuuze Historia yake wengine bado wako vile vile bali, ni changamoto tu ndio zimefanya wapoe kidogo

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Usifanye kosa la kupuuza historia yake kwa muonekano wake mpya wa leo, wengine ni maji tu yaliyopoa yamerudi ubaridi ila kwenye moto yatarudia hali yake ya umoto.

Usijifanye kipofu kupuuza historia yake bali hakikisha kuwa unajua kipi kilikuwa nyuma ya historia yake hiyo na je kuna namna ya muendelezo endapo mazingira yaliyopelekea historia yake hiyo yatajirudia tena leo? Usiogope kujiridhisha na hayo kabla hujatoa kibali cha kuendelea naye kwenye hatua ya mbele.

Matokeo ya kupuuza historia ni matukio ya kushangaza tunayoona leo na ukifuatilia historia ya muhusika unakuta aliwahi kuwa hivyo miaka kadhaa nyuma au alikuwa na viashiria hivyo lakini harakati za maisha zikamfanya apoe kwa muda ila uhalisia wake ni ule ule.

Changamoto za maisha zinafanya wengi waigize maisha kwa kujipa taswira zisizo na hatia ila ukiingia tu kwenye mfumo taswira inavuliwa na kurudissha uhalisia wake sasa yawezekana utakuja kugundua hilo tayari muda umeenda na kakuharibia mambo mengi.

Sio wote ila kwenye majumba ya ibada huko pia wapo ambao Changamoto zimewapa taswira ya kimaigizo ili tu wanase ambaye atafuta Changamoto zao na kisha warudi kwenye uhalisia wao ,Hivyo usione umekutana naye Kanisani/ Msikitini ukadhani historia yake haina nguvu tena la hasha fuatllia kwa kina ujue nini kilikuwa nyuma yake na je si endelevu endapo mazingira yatajirudia?

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako.
 
Tukiwaambia thamani ya mwanamke ipo kwenye mwili wake, ya mwanaume ipo kwenye mali yake; hawaelewi.
Tuliwarahisishia zaidi waoe bikira, hawaelewi. Let them learn it the hard way.
Hawatabiriki hao! Nishawahi kuwa na bikira nikawa nae mazingira ya mbali kidogo.Ila kuja kugundua alikuwa analiwa sana asee, kikubwa mtu umkute tu ashajitambua yeye ni nani na thamani yake ni ipi kwako,ila kama utakutana na watoto hawa wa 2000 hata awe Bikira lazima utachapiwa tu, ulimwengu wa sasa ushaharibika.
 
Mbona kama umetunga tu kisa ili ujifariji?
 
Kuaminiana baina ya mwanaume na mwanamke imekuwa ni changamoto kuu kwa maisha ya nyakati hizi.Binadamu hawaaminiani?Waaminiane na viumbe gani sasa?🤔
 
Kashawahi kujiuliza Hawa ambao anawala sasa na kuwakuta hawana bikra walio watoa bikra wakowapi?
 
Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…