its MalekoGJ
Senior Member
- Aug 27, 2020
- 136
- 292
Kompyuta yako si kifaa kinachofanya kazi kimya kabisa. Ndani yake kuna fans, diski zinazozunguka, na sehemu za kielektroniki ambazo kwa kawaida hutoa sauti ndogo. Lakini pale sauti zinapobadilika ghafla kuwa kubwa zaidi, za ajabu, au zisizo za kawaida, hapo ndipo tatizo linaanza. Leo tutaeleza sauti 6 muhimu ambazo ukizisikia lazima uzingatie mara moja.
1. Kubofya au Kutick-Tick:
“Click of Death”
Ikiwa unaisikia kompyuta yako ikitoa sauti za kubofya kwa mpangilio (tick…tick…tick), mara nyingi chanzo ni hard disk drive (HDD) inayoanza kufeli.
HDD hutegemea platters zinazozunguka na heads ndogo zinazosomea data. Zikiharibika au zikishindwa kusoma kwa usahihi, unasikia “click of death.”
Hatua za kuchukua
1.Fanya backup ya data zako mara moja.
2.Badilisha HDD haraka iwezekanavyo.
3.Fikiria kutumia SSD ambazo ni za kasi, hazina kelele na ni salama zaidi.
Kuzipuuzia kunaweza kuleta madhara makubwa ikiwemo
faili kuharibika, vifaa kufeli, au hata motherboard kuungua kabisa.
2. Fans Zenye Kelele Kubwa au Zilizochakaa
Fans ndizo mara nyingi hutoa sauti kubwa zaidi kwenye PC, lakini haziwezi kulia kama grinder au injini ya ndege.
Sababu kuu za kelele
Sauti ya juu kama mluzi mdogo mara nyingi husababishwa na coil whine — vibration ndogo kwenye coils za graphics card (GPU) au power supply (PSU).
Kama PC yako bado ina optical drive, ni kawaida kusikia sauti kidogo wakati disc inasomwa. Lakini ikianza kulia kama blender:
Wakati PC inawashwa na kutoa beep zisizo za kawaida, hii ni Power-On Self-Test (POST) inayotolewa na BIOS.
Pattern ya beep hutofautiana kulingana na motherboard
Rattle ndogo inaweza kuonekana haina madhara, lakini mara nyingi inamaanisha kuna kitu kimelegea ndani ya case:
Fanyqa Hivii
Clicks, whines, rattles, au beeps sio sauti za kawaida ni ishara za failure.
Kwa kuchukua hatua mapema unaweza
Tunauza laptops original na tunarekebisha matatizo yote ya kompyuta — kuanzia hard drive clicks, overheating, mpaka system errors. Wasiliana nasi sasa: 0675031229.

- Vumbi limejaa kwenye blades au filters.
- Bearings za fan zimechakaa.
- Overheating – components zinapopata joto kupita kiasi, fans hulazimika kufanya kazi kwa nguvu
- Safisha vumbi mara kwa mara.
- Badilisha fans zilizoharibika.
- Hakikisha airflow inatosha,
Sauti ya juu kama mluzi mdogo mara nyingi husababishwa na coil whine — vibration ndogo kwenye coils za graphics card (GPU) au power supply (PSU).
- Kwa GPU: mara nyingi ni annoyance tu, siyo hatari.
- Kwa PSU: coil whine kubwa inaweza kuashiria capacitors zinazoshindwa. Na PSU ikifa, inaweza kuharibu motherboard, GPU na drives zako zote.
- Ikiwa sauti inatoka PSU → badilisha mara moja na uchague PSU yenye ubora.
- Ikiwa ni GPU na si kubwa sana → sio hatari, ila ni usumbufu wa sauti pekee.
Kama PC yako bado ina optical drive, ni kawaida kusikia sauti kidogo wakati disc inasomwa. Lakini ikianza kulia kama blender:
- Inaashiria drive imechakaa au imealign vibaya.
- Wakati mwingine inaweza kuspin bila disc ndani — ishara mbaya.
- Ikiwa hutumii optical drive → ondoa au disable.
- Ikiwa unatumia → badilisha mpya (ni rahisi na bei nafuu).
Wakati PC inawashwa na kutoa beep zisizo za kawaida, hii ni Power-On Self-Test (POST) inayotolewa na BIOS.
Pattern ya beep hutofautiana kulingana na motherboard
- Beep moja ndefu + mbili/3 fupi → mara nyingi tatizo la GPU.
- Beep zinazoendelea → tatizo la RAM au power.
- Hakuna beep kabisa → inaweza kuwa motherboard imekufa.
- Tambua aina ya BIOS (AMI, Award, Phoenix).
- Tazama manual ya motherboard yako au website ya mtengenezaji.
- Reseat au badilisha component husika (RAM, GPU, PSU).
Rattle ndogo inaweza kuonekana haina madhara, lakini mara nyingi inamaanisha kuna kitu kimelegea ndani ya case:
- Screw imeachia,
- Cable inagusa fan,
- Panel ya case inatetemeka.
Fanyqa Hivii
- Fungua case na kagua kila kitu.
- Tighten screws zote.
- Tumia cable ties kushika waya mbali na fans.
Clicks, whines, rattles, au beeps sio sauti za kawaida ni ishara za failure.
Kwa kuchukua hatua mapema unaweza
- Kuokoa data zako.
- Kudumu na PC yako kwa muda mrefu.
- Kuepuka gharama kubwa za matengenezo.
Tunauza laptops original na tunarekebisha matatizo yote ya kompyuta — kuanzia hard drive clicks, overheating, mpaka system errors. Wasiliana nasi sasa: 0675031229.