Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
USIPUUZE TAARIFA YOYOTE INAYOHUSU KUWA UMEBAMBIKIZIWA MTOTO.
Anaandika, Robert Heriel
Labda uwe unajua kuwa huyo mtoto sio wako, au labda uwe unajua huna nguvu za Kupata mtoto na huyo kwako ni stara yako.
Lakini ikiwa utamsikia MTU yeyote akikuambia au akisema kuwa huyo mtoto au mtoto Fulani sio wako basi usipuuzie hiyo taarifa. Kila taarifa hasa taarifa nyeti kama hizo zichukulie Kwa uzito kama zenyewe zilivyo.
Usije sema kuwa Kitanda hakizai haramu. Hiyo ni misemo ya Watu wajinga, wenye Giza kichwani, misemo ya Watu ambao aidha wanamatatizo ya kiakili, kimwili na Kiroho.
Ni akheri ujithibitishie yaani upate uhakika kuwa mtoto Fulani ni wako au sio wako.Kisha mengine yaendelee kama utaendelea na malezi Kwa Moyo upendo au utabwaga manyanga.
Kwa kizazi cha sasa ni muhimu kuwa makini Sana na kila kitu unachoambiwa. Usimdharau yeyote.
Usidharau taarifa yoyote hasa taarifa nyeti.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam