Usipuuze taarifa yoyote inayohusu kuwa umebambikiziwa Mtoto

Usipuuze taarifa yoyote inayohusu kuwa umebambikiziwa Mtoto

-et kitanda hakizai haramu.
-et mtoto akikuwa anaweza kuwa great person.
-mara mtoto wa kubambikizia anaweza kusaidia famila.
-et baba yako mzazi anaweza kuwa sio baba yako ila amevunga
-sijui mtoto wa kubambikiziwa anaweza epuka laana na mikosi kama hivyo vitu vikiachiliwa kwenye ukoo

hizo point juu zote haziko logic zote ni assumption na uoga juu ya kufanya maamuzi
kama alivosema mtoa mada mwanaume anaetetea huu ujinga anaweza kua na matatizo katika kufikiri kidhibitisho soma point hapo juu yani ni assumption na uoga haziko logic kabisa
yote hayo kisa kuogopa kuface ukweli na kutoa maamuzi hakuna kingine
et ndio hekima na busara ,hakuna hekima na busara kwenye kukimbia ukweli na kukimbia kufanya maamuzi
mtoto sio wako timua huyo ni alama ya usaliti ,mtu msaliti hata shetani hamtaki iweje wewe ambaye sio hanithi wala sio mgumba ukubali huu ujinga

Mkuu WANAUME wengi wanaosema kauli kama hizo ni wanaume wasiojiamini, na Upeo wao wa kufikiri huwaga ni mdogo.
Ndio wengi wao hufanya mauaji Kwa sababu hawakutaka kuutafuta ukweli mpaka pale ukweli ulipojidhihirisha
 
Mkuu WANAUME wengi wanaosema kauli kama hizo ni wanaume wasiojiamini, na Upeo wao wa kufikiri huwaga ni mdogo.
Ndio wengi wao hufanya mauaji Kwa sababu hawakutaka kuutafuta ukweli mpaka pale ukweli uulipojidhihiri
siko zote kweli ni adui adui kwa mtu mpumbavu na mwovu
 
Mtoto sio Mtoto.
Hiyo kauli hutolewa na watu wasioelewa Dunia inatoka wapi na wapi inaelekea.

Watu dhaifu wasioweza kuukabili ukweli na uhalisia.
Kisingizio kujitafutia kifo.

Ni vizuri kujua ukweli, kuhusu Kulea wote ni maamuzi, Kwani wangapi wanalea Watoto wasio wao Kwa mapenzi Yao.

Ila Kulea mtoto ambaye unajua ni wako WA kumzaa kumbe sio wako, hicho ni kizazi haramu, kizazi cha uongouongo, kizazi cha kitapeli.
Binafsi kwenye ndoa ninao wanne. Hapo kabla nilikua nae mmoja. Sifuatilii wala nini maana waja watakwambia mbona humfanani mtoto wako wa tatu😀😀 ili tu uvurugwe
 
Tanzania wanazingua Sana hawatoi majibu ya kweli



Kweli kabisa.

Hawazingatii ukweli na uadilifu.

Hawana code of ethics labda.

Eti wanauliza kati yenu wanaume nani anaishi na mwanamke na hiyo Mtoto ukisema mimi basi majibu yatatoka wewe ndiwe mwenye mtoto [emoji108]
 
USIPUUZE TAARIFA YOYOTE INAYOHUSU KUWA UMEBAMBIKIZIWA MTOTO.

Anaandika, Robert Heriel

Labda uwe unajua kuwa huyo mtoto sio wako, au labda uwe unajua huna nguvu za Kupata mtoto na huyo kwako ni stara yako.

Lakini ikiwa utamsikia MTU yeyote akikuambia au akisema kuwa huyo mtoto au mtoto Fulani sio wako basi usipuuzie hiyo taarifa. Kila taarifa hasa taarifa nyeti kama hizo zichukulie Kwa uzito kama zenyewe zilivyo.

Usije sema kuwa Kitanda hakizai haramu. Hiyo ni misemo ya Watu wajinga, wenye Giza kichwani, misemo ya Watu ambao aidha wanamatatizo ya kiakili, kimwili na Kiroho.

Ni akheri ujithibitishie yaani upate uhakika kuwa mtoto Fulani ni wako au sio wako.Kisha mengine yaendelee kama utaendelea na malezi Kwa Moyo upendo au utabwaga manyanga.

Kwa kizazi cha sasa ni muhimu kuwa makini Sana na kila kitu unachoambiwa. Usimdharau yeyote.
Usidharau taarifa yoyote hasa taarifa nyeti.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kwanini kushindwa kuwa na mtoto iwe ni tatizo kubwa hivi kwamba ubambikiziwe mtoto asiye wako kuwa wako nawe ukubali eti kama stara?? Hata vitabu vya dini vimesema kupata watoto ni majaliwa, haipaswi kuwa ni aibu isiyobebeka
 
Kwanini kushindwa kuwa na mtoto iwe ni tatizo kubwa hivi kwamba ubambikiziwe mtoto asiye wako kuwa wako nawe ukubali eti kama stara?? Hata vitabu vya dini vimesema kupata watoto ni majaliwa, haipaswi kuwa ni aibu isiyobebeka

Wengine wanaona Bora hivyo. Na wengine wanaweza kuwa na mashaka ya kwenda kupima ili kuondoa mashaka Yao.
 
Nawaangaliaaaaa, naishia kusema hiiiiiii!! Yaani ulimwengu wa sasa Yesu asingepata wa kumlea! Angepata changamoto mapema sana kutoka kwa baba! Kama ulipenda boga penda na ya lake! Sasa umemkuta mama ana mtoto au anazaliwa mkiwa mmeshaanza mapenzi sasa utamkataa ili aende wapi? Kwani ukimlea tu unapungukiwa na nini?
 
Kama umezaliwa Africa ardhi ya Mtu mweusi lazima utahasirika na tamaduni zetu maana tuko tayari kukupa hata taarifa za Uongo juu ya DNA ili kulinda haki za Watoto . Kwa ufupi Mtoto anayeaminika ni wetu ni aliyezaliwa na Dada maana Dada abambikiwi Mwana .

Hekima ya Afrika ni Pevu sana .Kitanda hakizai Haramu waliotoa huu Msemo walifikiri zaidi kuliko DNA.
Mungu aliishi afrika kabla hajapakwa vumbi na weupe na dini zao.
 
Kuna mtoto wa kike nimebambikwa hapa juzi tu, ikabidi nifike kumwona na watu wote nilioongozana nao wanashuhudia kanifanana.... cha ajabu hadi ndugu zangu na mjomba mmoja anaingia kingi eti alama za mikono ni zetu!

Mimi namba zooote zinagoma kuanzia mimba hadi kuzaliwa kwake, ndugu zangu wameshaingia kimiani... nimebaki nawachora tu ila sijafanya maamuzi.

Kuna nafsi inaniambia nimkubali tu huyu mtoto ili nimlee, haitonigharimu kitu.... ila ni hadi huyu mama yake anyooshe maelezo kuwa sio mtoto wangu ila anahitaji msaada wa malezi tu.

Akikubali, nitamlea huyu binti kama ndugu mwingine yeyote.
Dogo mkaldayo unaenda pupa sana. Subiri ukue kue.
 
Endelea kusikiliza maneno ya watu mitaani,..

Kwamba ukisikia mtoto sio wako basi umkatae.[emoji23][emoji23]


Kweli kuwa na bichwa kubwa kama siafu sio kuwa na akili.
Mkuu mwandende kuna uzi flani ulikoment nilicheka sana yani wee jamaa. Eti ikija kugegeda sijui kwa mashemeji, shangazi, mamdogo mamkubwa na binadamu huna huruma wewe unagonga tu.
 
Back
Top Bottom