Kuna mtoto wa kike nimebambikwa hapa juzi tu, ikabidi nifike kumwona na watu wote nilioongozana nao wanashuhudia kanifanana.... cha ajabu hadi ndugu zangu na mjomba mmoja anaingia kingi eti alama za mikono ni zetu!
Mimi namba zooote zinagoma kuanzia mimba hadi kuzaliwa kwake, ndugu zangu wameshaingia kimiani... nimebaki nawachora tu ila sijafanya maamuzi.
Kuna nafsi inaniambia nimkubali tu huyu mtoto ili nimlee, haitonigharimu kitu.... ila ni hadi huyu mama yake anyooshe maelezo kuwa sio mtoto wangu ila anahitaji msaada wa malezi tu.
Akikubali, nitamlea huyu binti kama ndugu mwingine yeyote.