Usisome kozi ya clinical medicine (clinical officer) kabla ya kusoma thread hii

Asante sana,japo sikio la kufa halisikii dawa.
Wapo wanaobeza uzi huu,ila ki ukweli mleta taarifa ameeleza anachokifahamu au kukipitia.

Sasa wewe mzazi au kijana unayejipanga kusoma ilimradi umesoma
ni heri ukaanza umachinga mapema bila kuhusisha bodi ya mikopo au mzazi kuingia mikopo kukusomesha
mwisho urudi nyumbani kuomba mtaji wa kufanya umachinga au kufuga kuku.
 
Ni hivi, hata wewe ni matunda ya sperm zaidi ya mil 100 zilizoshindana kuingia yai la mama yako ukazaliwa. Yani angetokea mhuni mmoja akaanza kuziambia mbegu ndani ya shaha.. za dingi yako kuwa ushindani hauna mfano na ni bora wasijisumbue, ni wazi usinhezaliwa βœŒοΈπŸ˜„
 
ADDO imefutwa?
Kama MD anaruhusiwa kuuza duka la dawa why not CO?
Hii imekaaje?
Hapana mkuu hata MD haruhusiwi kwa mujibu wa Pharmacy Act 2011, biashara ya pharmacy ni ya wafamasia(Assistant, technician na Pharmacist mwenyewe).
Mtu ambaye sio mfamasia kwa maana ya registered pharmacist(mwenye degree ya kwanza) akitaka kufanya biashara ya famasi lazima awe na mfamasia kama mwangalizi.
 
Vipi business administration???kwa hizo tafiti zako ukizifanya kwa kozi zingine na nafasi za ajira,utabakiwa na manyoya tuuuu!!!
 
Ujaweka na watakaokufaa wakati wa kusoma na waliopo makazini.....bro hii dunia ipo balanced hizo nazaria zako utafikiri watu wanaishi milele
Mimi ni clinical officer nmehitimu 2019 nashukuru mungu nmepata ajira serikalini mwaka 2023. Thread yangu haisemi watu wasisome clinical medicine bali imejikita kuelezea chungu na tamu za kada hiyo ili kila anekuja ajue kabisa ana malengo gani aidha kujiendeleza kielimu au kupata ajira na je njia anayotaka kupita kama itamfikisha? Mfano mm binafsi lengo langu la kwanza halikua ajira ilikua kuendelea na bachelor degree ya udaktari (MD) na nilipata GPA ya 4.5. na niliomba vyuo nikapata vya private lkn hata sikukanyanga kwa ajiri ya ukubwa wa adda zao, na kwa GPA hyo nmeshndwa kabisa kupata chuo cha serikali hvo nkasota mtaani, ajira kwenye private sector lkn mshahara kama nlivosema 200k (hii yote sababu tupo wengi mno) ni ushaur tu kwa vijana kila mtu ana hatma yake ... Nlkua nikiomba sana ajira za tamisemi since 2020 lkn hola Mwenyezi mungu akabariki nikapata kupitia utumishi ambapo unafanya interview kupata ajira na niliopata nao ajira wapo waliokua wamehitimu mwaka 2022 kwaio kila mtu na bahati yake na Lengo langu watu wawe na taarifa muhimu juu ya maswali wanajiuliza kuhusu kada hii kiujumla
 
Naomba kujuzwa ada ya chuo Cha makerere uganda.shahada ya medical Doctor.Mwanangu nimpeleke huko.
Kama unahitaji kumpeleka mwanao Makerere University "As We Build For The Future" njoo pm nikupe namba za Madaktari niliosoma nao Makerere (wao walisomea MD),wapo kazini Muhimbili,Mlongazila nk,nadhani wao watakuunganisha na classmate wao waliopo Uganda kwa msaada zaidi
 
Mzee vp koz ya dental kwa diploma ina soko?? Nina dogo amepata dv 1 form four nataka akasome
Dental au Radiology ziko poa...mimi ni CO ila nikiambiwa nirudishe miaka nyuma kuchagua cha kusoma nisingethibutu kusoma hii kitu.
Mzee vp koz ya dental kwa diploma ina soko?? Nina dogo amepata dv 1 form four nataka akasome
 

Vyuo vya serikali hata ukiwa na C kupata CO sio rahisi; wanaopata nafasi kusoma hizo Course ni walio na pass za A na B na wachache sana C. Nilifuatilia mdogo wangu alivyotaka kusoma na kuona waliopangwa hiyo course 85% walikuwa na DIV 1 tena kali
hiyo D uliyosema sijui ni ya somo gani ila Kimsingi kutokana na watu kufaulu sana miaka hii...wanachukua pass za juu.
 
Kwa aliyesoma akabahatika kutinga mamtoni .....kujiendeleza timamu mafanikio kwa kede.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…