Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance mpaka chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu, watoto wakimaliza chuo hawana ajira aua ajira zinakuwa za chini, kwa o yanageuka kuwa maumivu:

Nimekuwekea hapa mbinu za kumsombesha mtoto wako kwa gharama nafuu na kupata elimu sawa na wale wanaoenda private

SHULE YA MSINGI - Hapa lengo kuu la kupeleka watoto shule za private huwa ni mtoto ajifunze kiingreza, piga ua galagaza somesha mtoto wako shule za mitaala ya kiingereza kwa sababu akifika sekondari na chuo atatumia lugha ya kiingereza, kuna shule za english medium zinakidhi kila kitu kutekeleza hili, hakuna aja ya kulipia mamilioni kwenye shule za private, Mwanangu kamaliza darasa la tatu saizi anaweza kusoma / kusikia / kuongea / kuandika kiingereza kwa level nzuri tu, anaimba miziki ya kiingereza, anaweza kuelewa movies bila tafsiri, n.k. Hata nikimletea mitihani ya kiingereza ya shule kama st mary anabutua vizuri kabisa.

SHULE YA SEKONDARI - Hapa mtaji wa kujua lugha ya kiingereza unahitajika sanaili kumpiga jeki asome kwa urahisi, Hapa nasihi sana asome shule ya day, aidha iwe ni shule yenye walimu wa kutosha na inafanya vizuri mitihani ya taifa iwe ni shule ya serikali aliyochaguliwa au hizi shule za umoja wa wazazi ambazo mara nyingi hazizidi laki 4.

Binafsi enzi zangu wazazi wangu walinipeleka shule za boarding za gharama kwa sababu wazazi wenzao wengi walifanya hivyo (mkumbo) pia wakiamini kwamba ndio ntajifunza maisha na kuepukana na vishawishi, Mimi muhusika nilieenda huko nlikutana na hali tofauti kabisa, ukiwa mlegevu utaonewa, ukiwa mtu wa makundi utavuta bangi, kulikuwa na mashoga, n.k. watoto wa ma rpc, majaji, wabunge, wakurugenzi wa taasisi, n.k walikuwepo. Kuna ile dhana ya kwamba mtoto aende huku kwa lengo la kupata marafiki wazito, hii nayo siwezi kuipa uzito maana kuna watoto wa vigogo walikuwa wakikuona unawalamba lamba wananyanyasa sana wenzao na kuwafanya kuwa watumwa.

Kiufupi mambo ya boaring hayana sana umuhimu kwa sasa, baki na moto wako nyumbani, Siku hizi kuna vitabu vya maswali na majibu vya kumuandaa mwanafunzi kujua kuyajibu kwenye chumba cha mtihani, Tuition zipo kibao nyingi sana, mtoto anafeli vipi???

FORM 5 NI TAKATAKA PELEKA CHUO - Kuliko kujiminya kumsomesha mtoto shule ya milioni 2 ni heri umpeleke chuoni kwa milioni 1 aanze kujifunza taaluma yake mapema, hata serikali yenyewe huwa inatoa selection chache sana mithiri ya bahati nasibu kuwafadhili wanafunzi kwenda kusoma vyuoni, hii ni sababu tosha kwamba chuoni ndio kuna elimu bora kuzidi form 5.

Nakumbuka hata nilivyomaliza form 6 na kuingia chuo, wale watu waliosomea certificate na diploma badala ya kwenda form 5, kwao karibu kila kitu kilikuwa ni marudio, maisha ya uhuru wa chuoni walikuwa wameshayazoea, walikuwa tayari wameanza taaluma zao mapema huku sisi tunasomea kombi, walikuwa wameshafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo huko maoofisini kuvimbishia cv huku sisi ni weupe, vyeti vyao vilikuwa vina hadhi ya kuajiriwa serikalini wakati sisi na vyeti vyetu vya form 6 hata kiwe na division 1 hupati ajira, n.k. Pia nao wanapata mikopo kama waliomaliza form 6.

VITABU - Hakikisha mtoto wako anasoma vitabu kwajili ya elimu binafsi, kuna vitabu kama rich dad poor dad, How to make friends and influence people, n.k hakikisha anasoma hivi, Mwanangu napanga aanze kusoma hicho cha how to influence people mwakani. vitabu ni resource muhimu zaidi, ajabu ni kwamba kuna wahitimu wengi wa vyuoni hawajawahi hata kujisomea kitabu kimoja

Kwa mtinfdo huu utaweza kupunguza gharama
 
Kwakweli maisha yamebadilika sana, yaani kila sehemu ni conection kwanza.

Fikiria kijana wako uliyekomaa kumsomesha vyema unatamani hata aende polisi tu baada ya nafasi kutoka unaambiwa huyo hahitajiki kafaulu zaidi[emoji28][emoji28][emoji28].

Ujuzi wowote nje na vyeti hana, ukiwa unatafakari umtafutie mtaji afungue kakibanda stand ya daladala na tamkozzzz la machinga linatolewa daah,unaamia kumtafutia piki piki akachomekewe barabarani huko avunjike miguu[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24].
 
Kwakweli maisha yamebadilika sana,yaani kila sehemu ni conection kwanza.

Fikiria kijana wako uliyekomaa kumsomesha vyema unatamani hata aende polisi tu baada ya nafasi kutoka unaambiwa huyo hahitajiki kafaulu zaidi[emoji28][emoji28][emoji28].

Ujuzi wowote nje na vyeti hana,ukiwa unatafakari umtafutie mtaji afungue kakibanda stand ya daladala na tamkozzzz la machinga linatolewa daah,unaamia kumtafutia piki piki akachomekewe barabarani huko avunjike miguu[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24].
Ukiwaza zaidi mabaya lazima yakukumbe tu ...kwa bodaboda wote vilema au
 
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance na kuwalipia ada chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu.

Nakushauri umpeleke hizo shule kumuondolea tu changamoto kadhaa kama chakula, walimu, umeme, maji, n.k ila sio lengo liwe aje kuajiriwa.

Kwanza akifika form 4 hapo mpeleke tu chuo aanze taaluma yake mapema na sio kuhaha form 6 ambayo hawezi pata ajira kwa cheti hicho, aende chuo apate uzoefu, apanue uwanja wake wa ajira, cv yake ijae hata training 3, n.k.

Wazazi wengi walioanza somesha watoto wao kuanzia miaka ya elf 2 wanaugulia maumivu maana walichotegemea kimekuwa reverse.
Kama una pesa pekeka mtoto shule ya maana acha visingiziio
 
Shule ya Serikali, vitabu nyumbani ( textbooks masomo yote, solved questions masomo yote), usimamizi nyumbani, preparation kila siku saa mbili hadi saa tano maskani,tuition masomo yote mtaani... This way nimetengeneza genius Very cheaply...

Elimu ya private ni biashara tuu inayopambwa kwa vi school moto vya kijinga kuwavutia Wateja
 
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance na kuwalipia ada chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu.

Nakushauri umpeleke hizo shule kumuondolea tu changamoto kadhaa kama chakula, walimu, umeme, maji, n.k ila sio lengo liwe aje kuajiriwa.

Kwanza akifika form 4 hapo mpeleke tu chuo aanze taaluma yake mapema na sio kuhaha form 6 ambayo hawezi pata ajira kwa cheti hicho, aende chuo apate uzoefu, apanue uwanja wake wa ajira, cv yake ijae hata training 3, n.k.

Wazazi wengi walioanza somesha watoto wao kuanzia miaka ya elf 2 wanaugulia maumivu maana walichotegemea kimekuwa reverse.
Kule anakutana na watoto wa matajiri, wanasiasa na wa viongozi mbali mbali anapata future connections. Akisoma Kayumba kama mimi baba ake anakutana na kina Siyawezi, Avinitishi, Mwajuma ndala ndefu,mtoto wa mama Mudy muuza Kangala,Mtoto wa mzee Juma muuza genge etc.....

Sijutii kumpeleka mtoto wangu shule nzuri na zenye garama. Kama wewe kipato kidogo sawa mpeleke unapoweza ila usishauri wengine kufuata unavyofikiria.

Huu ni Umaskini ndo unaokusumbuwa na kukufanya uone hii ni sawa mtoto kwenda na fagio na dumu la maji shule
 
Wengi husomesha watoto shule za gharama kama njia ya kujionyesha wao wana maisha bora kuliko wengine.
Wala sio sababu! Kama nna hela why mtoto wangu akasome shule anayoenda na mifagio na vidumu vya maji kila siku?Why aende shule yenye huaba wa walimu wa sayansi na hisabati?? kisa nisionekane naringia pesa¿ haya ni mawazo ya kimaskini
 
Back
Top Bottom