Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

Wanasomesha huko ki ufahari na ulimbukeni tu waonekane wana hela na pia watoto wao wajue english, kumbe hakuna lolote huko. Kama mtoto ana akili, ana akili tu hata akisoma shule za kawaida atafaulu
Yaani nna Hela alafu nimpeleke mtoto wangu Shule ambayo aina walimu wa kutosha, Mtoto anabeba fagio na kidumu cha maji ya kumwagilia maua na anasoma na watoto ambao Baba zao makapuku no future connections. Acha hizo boss Tafuta Hela
 
Vijana wangu nawatafutia pesa tu maana ndo utithi wao wa uhakika TOKA kwangu,Urithi wa ajira na uongozi wamejitengenezea mabwana wakubwa utafikiri nchi ya kifalme hii
Mbaya zaidi hao wazee wakifika miaka 50 huanza kuwapachika watoto wao serikalini kabla ya kumaliza kustaafu kwao.mimi nilishangaa Prof analilia mkataba aongezewe.
 
Wala sio sababu! Kama nna hela why mtoto wangu akasome shule anayoenda na mifagio na vidumu vya maji kila siku?Why aende shule yenye huaba wa walimu wa sayansi na hisabati?? kisa nisionekane naringia pesa¿ haya ni mawazo ya kimaskini
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..
 
Kweli mkuu nimeona wengi, wengine naishi nao hapa
 
Mleta mada hata hujielewi elimu kazi yake kuamsha thinking mind elimu ikiwa Bora mtoto kichwa chake kinafanya kazi vizuri zaidi

Pili kwa Nini watu husomesha shule za gharama nitakupa mfano mdogo Nina Mama nitilie mtaani aliapa mwanawe wa kike hataki aoelewe na watoto wazazi maskini wa mtaani anataka aoelewe na mtoto wa tajiri akasema watoto wa matajiri wanapatikana shule za Bei mbaya akasema nitakopa popote mwanangu asome shule ya pesa nyingi akakutane nao huko huko.Alipomaliza form six tu akapata kijana wa ki Yemen sasa hivi kaolewa anaishi Dubai na mumewe . Wazazi wake kawajengea jumba la kifahari Mbezi beach aliwafungulia supermarket
Watu husomesha shule za gharama Wana malengo mengi

Tatu wasoma shule za gharama wengi Ni high class na middle class Wana uwezo na means kwenye society wengine watoto wa mawaziri,wamiliki makampuni makubwa , viongozi wakubwa serikalini nk kujenga urafiki nao kwaweza fungulia mtoto fursa nyingi mno mbeleni kuanzia ajira, connection za kibiashara ,tenda nk Ni Kama kujiunga group la WhatsApp la waheshimiwa shule za kimaskini utapata Nini Cha maana? Unaharibu mtoto humjengei connection strong ya future yake

Nne unawaza ajira tu za ndani ya nchi mleta mada .Ajira ziko kibao nje ya nchi lakini zinataka mtu mwenye very strong educational background .High quality education inatakiwa hawataki mtu aliyesoma kiubabaishaji

Tano kichwaCha mtoto kinabadilika anajitambua kuwa maisha aliyonayo Bado Sana sababu anakutana na waliomzidi uwezo wa kiuchumi wengine wanakuja na magari wakiendesha wenyewe lakini wanasoma kweli kweli sio utani.Inampa changamoto anaacha uvivu wa kusoma.Ndio maana shule za gharama watoto hufaulu Sana Kuna ushindani wa kusoma usio wa kawaida kuliko shule za kawaida za mitaani Ukienda huwezi amini Kama hizo shule wanasoma watoto wa watu Wenye uwezo mkubwa kiuchumi.Shule utakuta iko kimya Hakuna kelele lakini pita shule za kawaida watoto kelele mtindo mmoja wengine wanacheza na kupanda juu ya madawati na kuruka ruka huku na kule kusumbua wengine hata mtoto akiwepo aliye serious kusoma hawezi kusoma.Noise control iko zero shule nyingi za serikali waweza dhani Uko tamasha au sokoni kwa mikelele

Yako mengi ningeandika Kifupi acha ubahili somesha mtoto shule nzuri ya gharama
 
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..
Kufagia anajifunza nyumbani haya huko kulima shule za mjini anaenda kulima wapi?
 
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..

Tunawaona,mtoto kashakua mtu mzima hata kupiga ugali hawezi.ila muongeleshe kiingereza[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji602][emoji3512]
 
kule anakutana na watoto wa matajiri,wanasiasa na wa viongozi mbali mbali anapata future connections.Akisoma Kayumba kama mimi baba ake anakutana na kina Siyawezi,Avinitishi,Mwajuma ndala ndefu,mtoto wa mama Mudy muuza Kangala,Mtoto wa mzee Juma muuza genge etc.....Sijutii kumpeleka mtoto wangu shule nzuri na zenye garama. Kama wewe kipato kidogo sawa mpeleke unapoweza ila usishauri wengine kufuata unavyofikiria.Huu ni Umaskini ndo unaokusumbuwa na kukufanya uone hii ni sawa mtoto kwenda na fagio na dumu la maji shule
Duuu! Mbona umetaja majina mengi ya kiislam? Au wao nchi hii ndio wana hali duni?
NB: Mengi sio yote
 
Kweli mkuu nimeona wengi, wengine naishi nao hapa
Watoto ni kwenda nao utavyoweza,nna kijana mamaake alijifanya matawi shule ni hizo za gharama apelekwe.nikamuachia jukumu.

Mpk naonana na mtoto hawezi chochote hata kupika wali.
Na anasema kabisa mi nimetoka maisha ya kitajiri.

Sijawai kupika hata chai leo baba ananambia nipike.
Mi namwambia mamaako mi namjua kabla hujazaliwa ngoja tu.

Leo yupo mtoto na mimi ilikua makofi namfundisha hiki makofi namfundisha hiki.
Mpaka sasa anashkuru kwamba yani baba sijui nilikua wapi.

Anafanya kila kitu mwenyewe bila kuambiwa.
 
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..
Ugoigoi wa mtoto sio shule-Ni wazazi na malezi yao kwa watoto.
 
Wanasomesha huko ki ufahari na ulimbukeni tu waonekane wana hela na pia watoto wao wajue english, kumbe hakuna lolote huko. Kama mtoto ana akili, ana akili tu hata akisoma shule za kawaida atafaulu
Tafuta pesa mkuu utapunguza manung'uniko
 
tunawaona,mtoto kashakua mtu mzima hata kupiga ugali hawezi.ila muongeleshe kiingereza[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji602][emoji3512]
Uongo kupika mtoto anafunzwa nyumbani Mbona wakiwa likizo wanapika,wanafagia na kuosha vyombo na Kama una bustani wanasaidia kulima na kumwagilia? Toto gani Hilo lisilojua kupika wakati likizo linakuwa na wazazi?

Shule haiwezi kufanya kazi ya kufundisha mtoto kupika uongo hata mnaojitia vibabu na vibibi vya zamani mliosoma enzi za mkoloni na za Nyerere shuleni mtu alikuwa hafundiswi kupika unajifunza kwenu pale unapigwa shule sio kufundishwa kupika kande au ugali au supu ya kongolo

Nyie vizee vya zamani viongo Sana
Wewe mwalimu Nani alikufundisha kupika ugali shuleni? Acha uongo
 
Wala sio sababu! Kama nna hela why mtoto wangu akasome shule anayoenda na mifagio na vidumu vya maji kila siku?Why aende shule yenye huaba wa walimu wa sayansi na hisabati?? kisa nisionekane naringia pesa¿ haya ni mawazo ya kimaskini
Hii hujalazimishwa watu tunatofautiana vipato! Wewe kama una uwezo peleka feza international, IST au Atlas!

Ila dhumuni ni kuwa usisomeshe mtoto mashule ya gharama kiasi kwamba ukawe unateseka kulipa ma ada kwa kujitutumua eti mtoto aonekane mboga 7!
 
Yaani nna Hela alafu nimpeleke mtoto wangu Shule ambayo aina walimu wa kutosha,Mtoto anabeba fagio na kidumu cha maji ya kumwagilia maua na anasoma na watoto ambao Baba zao makapuku no future connections. Acha hizo boss Tafuta Hela
Sasa hivi Kuna kituko kimeingia mtu ana hela hataki mwanawe asome shule nzuri za Bei za private eti akisoma private za hela atanyimwa mkopo toka bodi ya mikopo akifika elimu ya juu!!! Yaani Kuna wazazi hawaelewi future cost kwa mtoto ya maamuzi yao

Anyway kila mtu na mwanae atajijua
 
Mwandishi umeingia chaka yaani umepotea njia. Naamini malengo ya wazazi siyo hayo uliyoyasema.
Wazazi tunataka kuwapatia watoto wetu kitu kilicho kizuri- yaani wasome shule nzuri. Hilo ndilo tunalotaka.
 
Back
Top Bottom