N:B Haya ninayaandika mimi ambae tayari wazazi wangu walishanisomesha shule za gharama sana, Mimi nimepitia hizo shule kwa hio najua system nzima za hizo shule za gharama, Mtoto wangu nmembadilishia system na atapata kitu kile kile nlichokipata.
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance na kuwalipia ada chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu.
Kwangu mimi shule za english medium za serikali ni nzuri tu, mtoto anafundishwa kwa kiingereza, na hiki ndicho ambacho huwafanya wazazi walipie mamilioni kwenye shule za private kama wazazi wang, Mimi hapa nimejiongeza nimempeleka mtoto shule za serikali za mitaala ya kiingereza, gharama ni nafuu, ada ni nafuu kabisa kama laki 2 hivi na mtoto Mwanangu kamaliza darasa la tatu saizi tunaweza kuongea kwa kiingereza, anaweza kusikiliza na kuimba miziki ya kiingereza, anaweza kuelewa movies za kiingereza bila tafsiri, n.k.
Akimaliza shule ya msingi hapo tayari ana mtaji wa kukijua kiingereza, kama hajachaguliwa shule nzuri ya serikali, nampeleka shule hizi za day za laki 4 zenye walimu na zinafanya vizuri, kumbuka hapo ana mtaji wa kuijua vema lugha ya kiingereza, hii ni rasilimali kubwa. namuongezea na tuition kwa juu anafeli vipi kwa mfano, wazazi wangu walinipeleka shule za boarding za gharama wakiamini kwamba ndio ntajifunza maisha na kuepukana na vishawishi, Mimi nilieenda huko nlikutana na hali tofauti kabisa, ukiwa mlegevu utaonewa, ukiwa mtu wa makundi utavuta bangi, ukipenda vya bure utageuzwa shoga, n.k kumbuka hapa mtoto yupo boarding haupo karibu nae, mimi sipo tayari kufanya hiki, Ntamsomesha shule za day na kumuongezea tuition.
Pia wazazi wengi kama wangu walinilea kwa ule mtindo wa "mimi sitaki mwanangu apitie shida nilizopitia" yani nilikuwa napigiwa kufuli nisicheze nje, niwe narudi na school bus, n.k mimi kama muhusika nasema haya malezi sikuyapenda, nlikosa uhuru kwa kuzuiwa kuishi maisha halisi ya mtoto wa kitz, kwa sasa mtoto wangu simlipii school bus na huko shuleni kwao wenzake wanatamani sana na wao wawe wanatembea kama yeye, pia simruhusu azurure mitaani ila simfungii geti asocheze na wenzake.
Wazazi wengi walioanza somesha watoto wao kuanzia miaka ya elf 2 wanaugulia maumivu maana walichotegemea kimekuwa reverse.