Usitafute pesa kwasababu ya mwanamke, iwe kwaajili maisha yako. Kilichomkuta huyu jamaa ni fundisho tosha!

Usitafute pesa kwasababu ya mwanamke, iwe kwaajili maisha yako. Kilichomkuta huyu jamaa ni fundisho tosha!

Vifuatavyo ni Marufuku kwa mchumba ...!

Apangishiwi nyumba,asomeshwi,ajengewi,
alipiwi vicoba,alipiwi ADA Wala hanunuliwi gari...!

Marufuku Kbs.

Vinavyoruhusiwa ni vitu kama Zawadi Za peni,mkebe au kompasi,calculator, laptop,kitambaa cha Leso,Saa Ya mkononi,viatu,madaftari,Vishikwambi n.k....!
Rafiki yako Mwambie atulize mshono ndo kashapigwa hapo..!
Mkuu kupenda kunamfanya mtu awe kipofu na ukizingatia jamaa alikuwa na pic ya yamaana
 
Kumekucha Tena😂😂😂
Asimilia kubwa ya Wanawake wanafiki Sana mtu kakutoa mbali kajitoa kwako the end of the day unampiga tukio kama umpendi siumwambie kuliko kula hela zake
 
Wajinga Kila cku wanazaliwa,unapokuwa na Dem kama mwanaume lazima uwe na uwezo wa kujitathmini huyo Dem Yuko na wewe Kwa ajili gani.lakini kama jamaa kaanza kumbaka Binti tangu akiwa form four then hayo ni malipo ya kuchezea utoto au kutoa bikra kama aliikuta maana angeweza kwenda jela.
 
Mpe rafiki yako pole.
Maisha mkuu ingawa hakuwa mimi ila iliniuma as if nimefanyiwa mimi wanawake wengine wa ovyo Sana alafu utakuta akija kufikisha 30+ ataanza kulamika Wanaume sio waoaji wakati alipata nafasi akaichezea
 
Peter alimpa fursa Lucy ya kuona upande mmoja tu wa Peter ambao ni ule wa fedha na huduma, akasahau mahitaji ya Lucy ya kihisia. Kwahiyo Lucy alijikuta akimfikiria Peter anafikiria upande wa huduma na fedha.

Boyfriend wa Chuo akaja kutatua tatizo la Peter la kihisia. Hisia ambazo ndo upande dhaifu zaidi wa mwanadamu haswa mwanamke. Kwa kawaida mwanamke ni mkweli sana haswa kwa vitendo linapokuja suala linalogusa hisia zao, hivyo kwa hapo walipofikia niseme tu Peter ameingia mtumbwi wa vibwengo.

Kumjali sana mwanamke ni kitu kizuri lakini ukivuka mipaka unakua huna jipya tena kwa mwanamke, na kawaida ya hawa wenzetu jinsia ya kike atahitaji zaidi pale utakapompa zaidi. Wanaridhika na vitu ambavyo hawana pekee.

Kuwajali sana ni kitu hatari mno, wanatakiwa wapewe hekaheka kidogo za kiakili ili wasikusahau, hawatakiwi kuona attention kutoka kwa mwanaume ni kitu rahisi sana kukipata, hawatakiwi kuwa na mwanaume anayetabirika, wanapenda kusumbuliwa akili. Na wanaume wengi wanaosumbua akili wanawake ndio wanaobakia kwenye kumbukumbu zao daima.

My take: Jali ila usipitilize.
 
Hakuna kitu kama hicho. Kwanza hayo majina ya Lucy wanakuwa wabovu sana. Labda useme anajua kujiremba ila siyo mzuri, nakataa. Ni mbovu tu.
Mkuu lucy nijina tu nimelitumia lakini jina halisi haitwi hivyo hii ni jamiiforum Unaweza kukuta yupo humu humu so sio vizuri kutumia jina halisi la mtu ni vizuri kulinda privacy ya mtu
 
Si mnaambizanaga humu demu mkali ni wa kupiga na kusepa asa mwenzenu ilikuaje?
Mwenzetu alikuwa mbishi jamaa alikuwa amekufa na ameoza kwa huyo manzi kiasi ambacho hata aambiwe nini kuhusu huyo manzi wake hakusikilizi anaona kama unamtaka demu wake
 
Jamaa hakuwa Makini Tu toka zamani....naamini kabisa huyo mwanamke hakumpenda jamaa Ila jamaa alikuwa anaamini akigharamia Sana huenda dem atampenda...

Pili wanaume wenzangu mwanamke hasomeshwi...anaesomeshwa ni mkeo tayar....huko vyuoni kuna changamoto Sana....mtaendelea kupigwa na vitu vizito kila siku!
 
Back
Top Bottom