Usitafute utajiri, utajiri ni matokeo. Tafuta kibali cha Mungu

Usitafute utajiri, utajiri ni matokeo. Tafuta kibali cha Mungu

Kitu muhimu ni kuomba Mungu akupe kibali au upendeleo.

Mengine yote ni matokeo ya kibali ulichopewa na Mungu.

Ukipewa kibali na cha uzima, hakuna mfumo au mtu wa kukunyang'anya haki ya kuishi.

Ukipewa kibali cha utajiri, unaweza kuwa mkulimq mkubwa kwenye ardhi isiyo na rutuba kama Isaka na Ibrahimu.

Ukipewa kibali unaweza kupita katikati ya maadui na wasikufanye chochote kama Yakobo.

Ukipewa kibali unaweza kuwa houseboy mwenye influence kuliko baba Mwenye nyumba. Diwani mwenye ushawishi kuliko Rais kama Yusufu.

Katika maombi yako usisahau kuomba kibali kutoka kwa Mungu.
Haya mawazo yametuchelewesha sana kufikia malengo. Yanadumaza uwezo wa kufikiri
 
Nilipita nje ya msikiti jion moja nikamsikia imam kwenye kipaza sauti anasema Kila mtu anazaliwa na rizki yake na jinsi atakavyo ipata na kiasi atakachotumia.
 
Unapowachapa watoto nyumbani huo sio upendo?
Kuwachapa watoto ni kwa vile wewe huna, uwezo wa kuwafanya wasitende hayo makosa,

Yani watoto wanatenda makosa pasipo wewe kutambua kwenye ufahamu wako kwamba, Watoto wako wanatarajia kufanya makosa, Ndio maana una wachapa kuwakanya wasirudie tena.

Laiti ya kwamba ungekuwa na uwezo wa kuwafanya watoto wako wasitende makosa ili usiwachape, Ungefanya hivyo.

Sasa Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kutenda mabaya na makosa ili asi waadhibu?

Yani kaumba binadamu wenye kuweza kutenda makosa na mabaya ili awa adhibu tena yeye mwenyewe?

Kama Mungu alikuwa hataki tufanye mabaya na makosa, Alishindwaje kutu umba binadamu wema tu, Tusio weza kutenda makosa na mabaya, Tuka mtii muda wote?

Maana yeye si ni muweza wa yote?
 
Kitu muhimu ni kuomba Mungu akupe kibali au upendeleo.

Mengine yote ni matokeo ya kibali ulichopewa na Mungu.

Ukipewa kibali na cha uzima, hakuna mfumo au mtu wa kukunyang'anya haki ya kuishi.

Ukipewa kibali cha utajiri, unaweza kuwa mkulimq mkubwa kwenye ardhi isiyo na rutuba kama Isaka na Ibrahimu.

Ukipewa kibali unaweza kupita katikati ya maadui na wasikufanye chochote kama Yakobo.

Ukipewa kibali unaweza kuwa houseboy mwenye influence kuliko baba Mwenye nyumba. Diwani mwenye ushawishi kuliko Rais kama Yusufu.

Katika maombi yako usisahau kuomba kibali kutoka kwa Mungu.
Maneno magumu, ya kilokole yasiyo na tija!
Eron musk, bill gates, Diamond, Dangote, hawa wametumia talanta zao, kufanya Mambo,
 
Back
Top Bottom