Usitake kumfunika boss wako, kilichomuondoa Makamba Wizara ya Mambo ya Nje

1. WMN ni Wizara ya kutelekezea Watu wakorofi
2. Ni Wizara yenye hype kubwa kuliko maokoto
3. Ni Wizara inayowafaa majobless, utaishia tu kua mzururaji
 
January alijua ameshamaliza kilakitu bado kupitishwa tu na kamati kuu kumbe🤣
 
January alitenguliwa na Magufuli 21/07/2019 Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, SSH amemtengua 21/07/2024 Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, je nyuma ya pazia huu mfanano wa tarehe mwaka mmoja kabla ya uchaguzi unamaanisha nini?

Je anapewa kazi maalum inayohusiana na uchaguzi? Au just coincidence?
 
Ni tarehe tu zimefanana lakini hakuna uhusiano wowote. Hayati JPM huko alipo hana taarifa yoyote kuwa Makamba alirudishwa serikalini.
 
..Maza uwezo wake ni mdogo.

..hajui nchi ilikotoka, na inatakiwa kwenda wapi.

..kwa kifupi yeye ndio anaharibu kuliko hata hao anaowabadilisha.

..yeye na chama chake wanatakiwa kuondolewa kupitia sanduku la kura.
Yaani uitoe ccm kwa kupiga kura?

Watanzania mnachekesha, ccm haito kaa itoke madaraka hata kwenye ndoto huwez kuota ndoto kama hyo..

Njia anayo pitia Makamba ndiyo njia aliyo kuwa anapitia Lowasa..
 
Yaani uitoe ccm kwa kupiga kura?

Watanzania mnachekesha, ccm haito kaa itoke madaraka hata kwenye ndoto huwez kuota ndoto kama hyo..

Njia anayo pitia Makamba ndiyo njia aliyo kuwa anapitia Lowasa..

..ndoto hufuatiwa na vitendo, halafu matokeo.

..kuna waliosema uhuru wa Tanganyika ni ndoto, mwaka 1961 ukapatikana.

..kuna waliosema mapinduzi ya Zanzibar ni ndoto, mwaka 1964 yakawezekana.

..kwa hiyo inawezekana kabisa kuiondoa CCM kupitia sanduku la kura.
 
..hajui hata anataka nini. Falsafa yake ya 4R imemshinda kutekeleza amebaki kupelekeshwa tu.
Umeme upo kila sehemu, viwanda vinafunguliwa kila kukicha, pato la taifa linaongezeka kila kukicha na miradi iliyokuwa imekwama inazidi kuifungua Tanzania.

Nyinyi wachache wa Dar mnaosumbuliwa na wivu wala hamuwanyimi watendaji wa serikali usingizi.
 
..mimi siikubali Ccm yote, lakini nadhani kuna watu huko mnamuona Makamba ni tishio ndio maana mnampiga vita.
tishio la nini? labda kama anakutisha wewe.
kwetu huyo ni mpuuzi, fisadi na mshirikina nothing more nothing less. In a fair competitive ground huyu empty set anaweza kushindana na nani akashinda? uwezo hana, akili hana ila watu wa kumbeba anao.
 
Samia kaona liwalo na liwe ngoja ampumzishe kwanza. Ataanzisha tu majungu na fitina ndio vitu anavyoviweza lakini haitamsaidia chochote.
 
Magufuli alimuacha nyie mkasema maneno kibao ya utetez juuu
 
Nape, mwigulu, makamba, kikwete, Hawa watu wamelidumaza sana Taifa hili, hawafai kabisa hawa.

..hata Maza asili yake ni genge hilohilo.

..Na kibaya zaidi ni kwamba ana uwezo mdogo kuliko hao uliowataja.
 
tishio la nini? labda kama anakutisha wewe.
kwetu huyo ni mpuuzi, fisadi na mshirikina nothing more nothing less. In a fair competitive ground huyu empty set anaweza kushindana na nani akashinda? uwezo hana, akili hana ila watu wa kumbeba anao.

..anaweza kushindana na watu wengi sana huko Ccm na kuwashinda. Huko Ccm nani sio mpuuzi, mnafiki, fisadi, chawa, ...? Nani ktk Ccm ana sifa nzuri na ni mfano wa kuigwa?
 
..hata Maza asili yake ni genge hilohilo.

..Na kibaya zaidi ni kwamba ana uwezo mdogo kuliko hao uliowataja.
Wewe unao uwezo mkubwa wa hiyo nafasi uliyonayo sasa hivi?. Punguzeni maneno negativity hayawasaidii chochote.

Hata JPM mlisema hivi hivi alipokuwa hai alipoaga dunia mkaanza kumpamba kinafiki.
 
Ndiyo tatizo ya hizi kazi za kupewa...kila ukisimama kwenye mkutano ama jukwaa lazima uanze na...mama oyeeee, mamaa anaupiga mwingi...nani kama mama...

Bora nife lofa aisee !!
 
Umeme upo kila sehemu, viwanda vinafunguliwa kila kukicha, pato la taifa linaongezeka kila kukicha na miradi iliyokuwa imekwama inazidi kuifungua Tanzania.

Nyinyi wachache wa Dar mnaosumbuliwa na wivu wala hamuwanyimi watendaji wa serikali usingizi.

..mbona wamachinga wanazidi kuongezeka kama viwanda vinafunguliwa na kuongeza ajira na uzalishaji?

..hakuna awamu ambayo haikujenga viwanda, miradi ya umeme, na miundombinu mingine.

..Tatizo ni kwamba waliyoufanya na yanayofanyika sasa hivi, yameshindwa kupambana na ongezeko la umasikini, na wanaotafuta ajira, hapa nchini.

..Kwa maneno mengine Ccm imeshindwa.
 
Makamba alidanganyika kwa kuwa msaidizi wa Kikwete akadhani anao uwezo wa kuwa rais tayari.

Mtazame anapoongea na wageni haswa wazungu vile anavyojiweka.

Ujuaji umemjaa akilini mwake na hana watu sahihi wenye kuweza kumwambia ukweli.

..tatizo Maza hajui Kiingereza, na hoja za kuongea na wazungu, na wageni wanaotutembelea, sasa hasira zenu mnazihamishia kwa bwana kipara.🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…