Usitumie hii mbinu kwenye mapenzi utakuja kufa!

Usitumie hii mbinu kwenye mapenzi utakuja kufa!

Sikuhizi nalipia delivery sina mambo ya kukabana na mtu nakula tunamalizana hapo hapo na uzuri wengi ninao kutana nao maelekezo ni hayo kula lipa tembea tusijuane sana ukihitaji tena siku ingine nichek kula lipa tembea

Nimeipenda hio mbwinu
Haya ndo maisha ya sasa hususani hapa Dar es salaam, ila kwa wageni wa jiji kina KENZY wanataka kugandana
 
😄😄😄😄😄


1733683581891-jpg.3173224
Nakubali kaka
 
Sawasawa bwana karungu yeye tumekusikia... Pole kwa masaibu yaliyokukuta ndugu
 
Waswahili wanasema "Kata mti panda mti!".
Huu msemo usiulete kwenye mapenzi utakuja kufa ulimi nje!.

Baada yakubwagana na mpenzi wangu chapchap kuuponya moyo,roho na nafsi yangu nikaamua kutafuta mpenzi harakaraka ili ku cover nafasi iliyoachwa wazi!.
alikuwa binti fulani hivi ndembendembe, kuanzia juu mpk chini mwili wake ulihubiri uzuri ama ufundi stadi wa muumbaji!.
muhuni wa watu nikatopea penzini hapo nikiwa na siku tatu tu toka nibwagane na mchuchu wa awali!.

Sasa penzi jipya likiwa na mwezi tu, nilikuwa siambiliki tayari nilikuwa nimezama nginjanginja mtoto alinidatisha na mwili wake laini halafu kitandani alikuwa na miondoko yakiufundi ukizubaa unaweza kupoteza uhai kitandani!!.
Siku isiyona jina sina hili wala lile nikafuma li sms la mahaba kwenye simu yake!!, nikaona isiwe tabu kabla sijapiga kelele wacha nifatilie.
walahi walahi katika kufatilia nikakuta kumbe kuna njemba linamfaidi na mbaya zaidi nilipata chati yao demu kanipondea kwa mshikaji ati wananiita mimi "Karungu yeye!" mara sijui mapenzi ati nampakampaka mate tu kama litoto linalojifunza kunyonya!.
wakati nayasoma hayo ye alikuwa amelala fofofo, machozi fulani hivi yakawa kama yanataka kunitoka lkn nikajikaza!. hawakuishia hapo kumbe walikuwa wanajua niliachwa na ndo nikamtafuta yeye sasa walivyokuwa wanahadithiana kuhusu mimi kuachwa kwangu ati
"ndo maana aliachwa akakonda kama ndama aliekosa lishe!"

hasira zilinipanda nikatamani hata niimeze simu yake ili akiamka hata asiione tena!. hii ndo hatua ilinifanya mpk nimkumbuke mpenzi wangu wa awali alivyokuwa mnyenyekevu,mcheshi na mzuri, nilitamani aje anitoe kwenye hii hali lkn isingewezekana maana nayeye alikuwa ashapata mpenzi mwengine!.

Niliamua kutoka kwenye hayo mahusiano na sikuamua kuanzisha tena mahusiano haraka haraka maana nilijiona kabisa kama huku nimeitwa karungu yeye huko niendako ningeitwa nani..??

Hivyo ndugu zangu kama utaachana na mtu usitumie haraka kupata mpenzi mwengine watu hawana adabu!, tulia jitafutie mpenzi wako taratibu.
Umevuna ulichopanda mwanangu. Mshaambwa hasira hasara na hasira za mkizi tijira ya mvuvi. Mkizi wewe umepata mvuvi wacha akuvue vilivyo.
 
bila shaka we utakuwa msukuma maana ndo mnaongoza kwa ushamba chai na maparachichi wapi na wapi..😂
Huyo pasina shaka ni mnyakyusa ama muhehe usukumani hayo maparachichi ya ghrama kuliko supu yoyote unayoijua. huku parachichi dogo jero kubwa buku hadi buku jero
 
Back
Top Bottom