Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa,uchumi na kijamii, Onesmo Mushi, amewasihi watanzania kutoshiriki kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwani itakuwa kama ni kuhalalisha upumbavu.
Mchambuzi huyo ameonesha kuwa tangu turejee kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa, wagombea wa Urais Kwa mwaka huu ni wa viwango vya chini haijawahi kutokea.
Mushi amesema chaguzi zilizopita wagombea Urais walikuwa ni kiashiria cha nchi kuwa makini kwenye kutafuta viongozi wake.
Mushi ametolea mfano jinsi Mwaka 1995 kulivyokuwa na ushindani mkubwa kati ya mgombea wa CCM wakati huo Benjamin William Mkapa na Augustine Lyatonga Mrema.
Mushi pia amekumbusha jinsi Mwaka 2000 Benjamin William Mkapa alivyotoana jasho na Ibrahim Haruna Lipumba, kwenye uchaguzi uliokuwa una ushindani mkubwa.
Ametolea pia mfano wa Jakaya Mrisho Kikwete na Freeman Aikaeli Mbowe, Jakaya Kikwete dhidi ya Willbroad Peter Slaa, na John Pombe Magufuli dhidi ya Edward Nyoyai Lowassa na John Magufuli dhidi ya Tundu Antipas Lissu.
Kwa mtazamo wake wagombea wa Urais mwaka huu, wanatoa taswira yenye tafsiri kuwa kama Taifa hatupo makini (Serious) kwenye kutafuta viongozi wetu.
Video.
👇