Usitumie Kura yako kuhalalisha upumbavu: Onesmo Mushi

Usitumie Kura yako kuhalalisha upumbavu: Onesmo Mushi

Kwa ivo hakuna suluhisho?
Suluhisho kwanza ni kufahamu tunataka nini..., Sababu hii Demokrasia ya Kuchaguliwa na wachache (wajumbe / vyama n.k.) wa kutuamulia na sio sisi kuamua na wala hatuna jinsi ya kuwawajibisha zaidi ya kusubiri miaka mitano nadhani SIO nguvu ya UMMA bali ni Oligarchy.., (He who Nominates.., Chooses)



Tukishamaliza hapo tujikitike kwenye UWAZI na kufuata Sheria na Mifumo as well as Kutumia Merits za kupata watendaji, na lazima tuwe na Muhimili mwingine ambao sio wa wanasiasa ambao utakuwa na nguvu ya kuibua madudu ya wanasiasa (sababu kinachoendelea wanasiasa wa sasa wote wapo kwa ajili ya maslahi yao mwananchi ni second); Na ukizingatia miaka mitano ni michache sana kufanya Big changes kwahio kila anachofanya kiongozi ni kujipatia ujiko short term bila kujali what happens long term,

 
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa,uchumi na kijamii, Onesmo Mushi, amewasihi watanzania kutoshiriki kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwani itakuwa kama ni kuhalalisha upumbavu.

Mchambuzi huyo ameonesha kuwa tangu turejee kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa, wagombea wa Urais Kwa mwaka huu ni wa viwango vya chini haijawahi kutokea.

Mushi amesema chaguzi zilizopita wagombea Urais walikuwa ni kiashiria cha nchi kuwa makini kwenye kutafuta viongozi wake.

Mushi ametolea mfano jinsi Mwaka 1995 kulivyokuwa na ushindani mkubwa kati ya mgombea wa CCM wakati huo Benjamin William Mkapa na Augustine Lyatonga Mrema.

Mushi pia amekumbusha jinsi Mwaka 2000 Benjamin William Mkapa alivyotoana jasho na Ibrahim Haruna Lipumba, kwenye uchaguzi uliokuwa una ushindani mkubwa.

Ametolea pia mfano wa Jakaya Mrisho Kikwete na Freeman Aikaeli Mbowe, Jakaya Kikwete dhidi ya Willbroad Peter Slaa, na John Pombe Magufuli dhidi ya Edward Nyoyai Lowassa na John Magufuli dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Kwa mtazamo wake wagombea wa Urais mwaka huu, wanatoa taswira yenye tafsiri kuwa kama Taifa hatupo makini (Serious) kwenye kutafuta viongozi wetu.

Video.
👇
View attachment 3436436
Wananchi wameshasema hawatiki
 
Waraka wa TEKI nao upo njiani. Kusomwa kila parokia, jimbo, kigango, jumuiya.
 
Shida kubwa ya Chadema ni kudhani wao tu ndio wana haki ya kuwa chama za upinzani wengine wote hawafai. Nyinyi mkisusia wengine wanakula. Mlitakiwa kuwa washindani na kupiga kampeni kali sio kususa. Hamtaki na mnataka wengine wakatae. Siku mkija kukubali kuwa hii nchi inaenda bila kuwa na wapinzani kama Chadema, badala ya kufanya siasa mmekuwa wanaharakati.
 
Amesha chukuwa form.
IMG_20250809_113357_551~2.jpg
 
Shida kubwa ya Chadema ni kudhani wao tu ndio wana haki ya kuwa chama za upinzani wengine wote hawafai. Nyinyi mkisusia wengine wanakula.
CHADEMA haidhani yenyewe tu ndiyo chama cha siasa (siyo chama cha upinzani) bali kinapigania haki yake ya kuwa chama cha siasa.

Simba inaposajili vizuri ili ichukue ubingwa, mtu yeyote atailinganisha na Yanga. Sasa siyo kwamba Yanga na Simba ndiyo timu pekee za Mpira wa miguu Tanganyika, Bali ukweli zenyewe ndizo timu kubwa Tanganyika.

Ukitaka kuipuuza CHADEMA, ifanye CCM iwe Imara. NA CCM iliacha kuwa imara mara tu baada ya uchaguzi wa mwaka 2000.
 
Back
Top Bottom