Usitumie Kura yako kuhalalisha upumbavu: Onesmo Mushi

Usitumie Kura yako kuhalalisha upumbavu: Onesmo Mushi

OCTOBER KWA UMOJA WETU TWENDENI TUKA ✔️ TUACHANE WALIOJICHOKEA KIAKILI?😄


Oktoba mashetani yote yaende kuwasimika watakaosimamia utekaji na mauji ya Watanzania. Yaende yakawasimike viongozi wao wa kupora rasilimali za nchi na kuwagawia wajomba wa kutoka uarabuni.

Watu wema, wanaoipenda nchi yetu, wanaojua thamani ya uhai wa mwanadamu, kwao uchaguzi wa October ni ushetani usiotakiwa kuusogelea, maana ni tendo la ibilisi. Tuyaachie mashetani na mawakala wao.
 
Na kweli, huwezi enda kupiga kura sura za akina salumu mara Mpina mara samia...tunaonekana hatuko serious na rasilimali zetu za nchi ..hakuna mzalendo na mtu aliye serious hapo...kwa mbali Mpina ila hao wote hakuna tusichezeane sharubu aisee
 
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa,uchumi na kijamii, Onesmo Mushi, amewasihi watanzania kutoshiriki kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwani itakuwa kama ni kuhalalisha upumbavu.

Mchambuzi huyo ameonesha kuwa tangu turejee kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa, wagombea wa Urais Kwa mwaka huu ni wa viwango vya chini haijawahi kutokea.

Mushi amesema chaguzi zilizopita wagombea Urais walikuwa ni kiashiria cha nchi kuwa makini kwenye kutafuta viongozi wake.

Mushi ametolea mfano jinsi Mwaka 1995 kulivyokuwa na ushindani mkubwa kati ya mgombea wa CCM wakati huo Benjamin William Mkapa na Augustine Lyatonga Mrema.

Mushi pia amekumbusha jinsi Mwaka 2000 Benjamin William Mkapa alivyotoana jasho na Ibrahim Haruna Lipumba, kwenye uchaguzi uliokuwa una ushindani mkubwa.

Ametolea pia mfano wa Jakaya Mrisho Kikwete na Freeman Aikaeli Mbowe, Jakaya Kikwete dhidi ya Willbroad Peter Slaa, na John Pombe Magufuli dhidi ya Edward Nyoyai Lowassa na John Magufuli dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Kwa mtazamo wake wagombea wa Urais mwaka huu, wanatoa taswira yenye tafsiri kuwa kama Taifa hatupo makini (Serious) kwenye kutafuta viongozi wetu.

Video.
👇
View attachment 3436436
Kabisa!!! Mimi sitafanya upuuuuuzi huuuuu!!!!!!!
 
..kwanza mfumo mbovu.

..pili wagombea wote mazuzu.

..siku ya uchaguzi ni bora kupumzika, au kufanya shughuli binafsi.
 
Oktoba mashetani yote yaende kuwasimika watakaosimamia utekaji na mauji ya Watanzania. Yaende yakawasimike viongozi wao wa kupora rasilimali za nchi na kuwagawia wajomba wa kutoka uarabuni.

Watu wema, wanaoipenda nchi yetu, wanaojua thamani ya uhai wa mwanadamu, kwao uchaguzi wa October ni ushetani usiotakiwa kuusogelea, maana ni tendo la ibilisi. Tuyaachie mashetani na mawakala wao.
Suala la utekaji,serekali sikivu imesha lichukuwa na kulifanyia kazi kwa kina,serekali ilichukizwa sana na utekaji wa mdude,na hapo ndipo ilipoongeza kasi za kupambana na maharamia hao,kwa sasa hakuna tena uchafu wa aina hiyo,ndani ya Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom