Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

Sasa mkuu asiuze na yeye hapaendelezi?

Hilo eneo la baba yako we mwenyewe umeandika mwamba alienunua alijenga makitu kibao, na yeye alikua miongoni wa wachangamshaji wa eneo kwa kiasi kikubwa kama sio chote kabisa.

Sasa mzee wako ulitaka asiuze nani aje apaendeleze sasa??

Hupaendelezi UZA.
 
Hela sio kitu mkuu, kuna watu wameuza Nyumba 500 Million wakamuomba waliemuuzia awape muda wa kuhama, jamaa bila hiyana akawapa Mwaka mzima wajipange wahame walivyo hawana akili wakaanza kuzitumia pesa bila mipangilio inayoeleweka kulipa madeni na ujinga mwingine wanakuja kushtuka mwaka umeisha hawajafanya muendelezo wa sehemu nyingine ya kuishi na hawana pa kwenda mwisho alienunua eneo ikabidi aje kuwaondoa kwa nguvu akiwa na polisi maana ilikua inaenda kua kesi eneo kanunua ila jamaa km walikua wanataka waendelee kukaa, leo hii wakipita pale wakipatazama roho zinawauma maana jamaa kafanya muendelezo mkubwa sana wa kujiingizia faida hata miaka 100 mbele, tumia akili usikurupuke
 
Sio la Baba yangu mkuu mimi katika kitu napenda kuongea na wazee zaidi maana kuna nondo nazipata zaidi kuliko kuongea na vijana wa ovyo ovyo kwa hio ninaposema mzee haina maana ni baba yangu usinitoe nje ya reli
 
Emu fafanua tena kidogo, mfano eneo lililokua linauzwa shillings 5000 mwaka 1980 leo bei yake ni hio hio Shs.5,000?
Mwaka 1980 mshahara ulikuwa Tsh 500/=
Kwahiyo ili upate 5000 hapo uweke mishahara 10 au 11.
Mwaka 2025 mshahara 1,000,000/=
Ukiweka mishahara 10 hapo ni milioni 10.
Thamani inakuwa Haina tofauti sana
 
kwa ardhi sikukatalii. mwaka 1996 tuliendaga pale tegeta kwa ndevu marehem babu alikataa eneo kubwa tukasema porini. leo je? ardhi mzee haina ubaya. si unaona walioshika beach plot kigambon wengine wameshakufa
 
Emu fafanua tena kidogo, mfano eneo lililokua linauzwa shillings 5000 mwaka 1980 leo bei yake ni hio hio Shs.5,000?
Nimesema thamani ya pesa huwa inaenda na muda,zamani tsh mia tano ilikuwa ina thamani mara 10 kuliko elfu kumi ya sasa, ukiwa na mia tano utanunua mbuzi watano,utanunua gunia la mahindi na chenchi inabaki, leo hii elfu kumi ya leo inaweza kufanya hivyo.
Tuna pesa nyingi lakini thamani yake ni ndogo ukilinganisha na miaka hiyo, kwa sasa ukiuza kiwanja let say m100 inaweza kulingana au iwe ndogo na mtu aliyeuza kiwanja kile kile mwaka 1990 kwa tsh milioni 5 tu. Umenielewa mkuu?
 
Huyo jamaa ana hoja nzuri, zingatia hilo.
 
Kuuza eneo sio tatizo.
Mimi nadhani kosa ambalo watu hua wanafanya ni kuuza eneo bila kuwa na mipango ya nini cha kufanyia hizo hela, hivyo kuishia kuzichezea.
 
kwa ardhi sikukatalii. mwaka 1996 tuliendaga pale tegeta kwa ndevu marehem babu alikataa eneo kubwa tukasema porini. leo je? ardhi mzee haina ubaya. si unaona walioshika beach plot kigambon wengine wameshakufa
Hawa nawaambia mimi hawanielewi bora uwaambie wewe kuna watu walidharau maeneo wakauza kisa waliona hapata endelea milele leo pameendelea wakipita palepale hawaamini wanachokiona
 
Uongo mkubwa thamani ya mwaka 1980 sio sawa na thamani ya 2025 na mbaya zaidi ukiwa umefaanya muendelezo sio kupaacha tu km kichaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…