Usiwasahau ndugu kisa una marafiki, tujifunze kuwapa nafasi wote

Usiwasahau ndugu kisa una marafiki, tujifunze kuwapa nafasi wote

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kuweka stori iwe fupi ni kwamba ndugu huyu alijiingiza kwenye kununua mali iliyotumika pasipo mkataba wala risiti, kanasa kwenye tundu hapo juzi na kiasi kilichohitajika ili achomoke ni milioni 1.

Ana marafiki wengi lakini kwenye hili tatizo wameingia mitini ni wawili tu ndio wamechangia cha maana, moja kaweka laki na tunamjua tangu zamani, mwengine elf 50, waliobaki watatu michango haivuki elf 50 (michamgo ya kuzugia) wengine wamepotea kama mvuke.

Ndipo tulipojulishwa sisi nduguze kwamba kijana yupo shimoni, harakati zilianza moja kwa moja bila kujali ratiba za shughuli zetu, ni sisi nduguze ndio tulikuwa tayari kumpelekea chakula na kumchangia na hata ingebidi tukope tungekopa.

Simaanishi kuwa tuendekeze sana ndugu ama tusiwe na marafiki bali tujue kubalance mambo !!

Pamoja na kuwepo marafiki wabaya wapo wazuri pia, ni ngumu sana binadamu kuishi bila marafiki hasa tunapokuwa sehem flan kwa muda mrefu (kazini, vyuoni, makanisani, mtaani, n.k)

Pia ndugu ndugu wapo wabaya sana na wapo wazuri zaidi maana kiasili ndio watu wa karibu, utaowajua mapema ma mtaendelea kukutana mara kwa mara kuliko marafiki, si wa kuwabeza.
 
Kwa kweli mimi sina na sijawahi kuwa na rafiki zaidi ya maisha ya shule, na yaliishia hukohuko...
Japo wengi tulikutana baadae na ushkaji ni wa tukikutana tena ni mambo wa vipi....end of story..
Wa karibu yangu ni watoto wangu, na ndugu wa familia yangu ya baba na mama mmoja....ambao tunategemeana kwa hali na mali....
 
Ndugu wachache mno nao haya mambo ni kubahatisha tu
 
Back
Top Bottom