Usiyoyajua kuhusu Daraja la Tanzanite. Kongole Rais Samia!

Usiyoyajua kuhusu Daraja la Tanzanite. Kongole Rais Samia!

Yaani kumekuwa na foleni ya hatarii
Duh...naona kila mtu anataka kupita huko
Acha wapite walizoee wakichoka watarudi la zamani,tanzanite wataendelea kutumia kwa wanao kwenda obay,masaki

Ova
 
Kura yetu kama mwanachama wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na ushawishi wa kisiasa na kidiplomasia Afrika imetupatia hilo daraja toka Korea Kusini. ( Ban Ki Moon kuweza pata nafasi ya ukatibu mkuu UN)

Hapa nguli Jakaya alicheza na diplomasia kuleta manufaa ya kiuchumi kwa nchi. Shukrani kwake.

Hongereni JPM na SAMiA kwa kusimamia ujenzi mpaka kuisha kwake.
 
Yeye anamalizia ya jpm yakwake mingapi ameanzisha?
Kwa vile hana vision inafaa anga'ang'ane na ile ya jpm japo akitoka 2025 aache sifa ya kukamilisha miradi ya jpm.
Mengine tunaona tu akimcritic jpm kwa vitendo. Bado tu kuruhusu ushoga😂.. maana mabeberu ndio anawahusudu sana.
Tulia mtoto wa kiume, wivu wa namna hiyo utaishia kubanduliwa!! Usijesema sikukwambia, wanaJF mashahidi
 
Kati ya hayo 10 ni la ngapi hili
Daraja limejengwa mita chache kutoka daraja la zamani la Salenda. Lina Urefu wa takribani Mita 1030, Upana wa Mita 20.3 na Urefu wa Barabara Unganishi yenye KM 5.2 zilizojengwa kwa kiwango cha lami. Daraja limekamilika kwa asilimia 100%.

Tofauti na madaraja mengi ya namna hii barani Afrika, Watumiaji hawatalipa tozo yoyote pindi watumiapo daraja hili (TOLL FREE). Pia, Daraja hili lenye uwezo wa kuhimili tani 180 za uzito litaweza kusafirisha watu wapatao 55,000 kwa siku.

Kwa Takwimu zilizopo, Daraja hili litakuwa kati ya madaraja 10 marefu zaidi barani Afrika likiwa nyuma ya Daraja la Wouri kutoka Cameroon lenye urefu wa takribani Mita 1800 likiwa katika nafasi ya nane kwa urefu Afrika.

Gharama za ujenzi zimetolewa kwa ushirika kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Korea. Ujenzi ulioanza rasmi mwaka 2018 umeigharimu serikali ya Tanzania kiasi cha takribani dola za kimarekani milioni 104.5.

Hadi kufikia mwaka 2017, Takwimu zilionyesha watumiaji wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kufikia kiasi cha magari 42,000 kwa siku. Barabara hii ni kati ya Barabara muhimu kiuchumi lakini pia ni kati ya Barabara zenye foleni, hivyo kukamilika wa Tanzanite Bridge ni mafanikio makubwa kiuchumi.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika mwaka 2021, wakazi wa Jiji la DSM wenye kipato cha TZS 90,000 hupoteza hadi kiasi cha 39% ya mapato yao kutokana na gharama zinazosababishwa na foleni. Daraja la Tanzanite ni kati ya mipango mingi madhubuti ya kukabiliana na foleni ndani ya Jiji.

Mwisho nimpongeze Rais Samia Suluhu kwa kutekeleza ahadi ya kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli inatekelezwa. Mh. Rais anazidi kuonyesha umahiri mkubwa katika uongozi wake. Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele tumebarikiwa kuwa na viongozi makini.

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
 
Tazara bado panahitaji kuboreshwa Mandela Road bado ina foleni ya kutisha
Tunaishukuru serikali ya korea kwa daraja zuri pamoja na barabara zake.

Pia tunaishukuru world bank kwa ubungo interchange.

Tunawashukuru japan kwa Tazara.

Tupate mtu mmoja ajitoe tumalize na pale mwenge kwa kuenga interchange. Watu hao ndio wanafanya sisiyemu tuvimbe kichwa
 
Akafie mbali, ameligawa Taifa vipande vipande. Na katuachia umaskini kwa kukopa hela nyingi na kujenga kiwanja cha ndege chato na kununua ndege zisizo zalisha. Ametuachia majanga.
Pia wewe utakufa fala wewe sijui mfanyiwe nini malalamiko kila sku mtoto wakiume au unataka bolo yang??!!
 
Akili zako.fupi mno , unahisi korea , Japan na World Bank wametoa pesa bure ? Ndio maana bado tunatawaliwa kamamboleo , bado tuna mabogasi mengi sana
wewe ndio zimekaa kwenye makalio, nimemjibu mwenzako aliyesema ni pesa za Mwendazake ndio ana akili km zako za Chato?
TANROAD kuwajengea uwanja wa Ndege na traffic lights ndio mmeona mmeula, pesa si zetu NI ufadhili hata km ni deni
 
Wale waliotuibia kupitia Richmond na wale waliokomba hela kutoka Escrow Account walifanya nini cha maana kupitia huo wizi? Afadhali aliyeiba akazipeleka Chato kwa Watanzania kuliko walioiba then wakaenda kuzificha pesa nje ya nchi halafu tunakopeshwa kwa riba
kwa akili zako kweli unaweza kwenda Chato kushangaa Kaburi au uwanja na taa za barabarani?
Mobutu alijenga Globetore Nani katika huko?
Mwendazake alishaipoteza Nchi hata daraja la Busisi linaishia kwa wakwe ningekua Mimi miradi yake hiyo ningezima km alivyoisahau kusini na Gesi yake na korosho mpaka mnyooke haturudii tena kuwapa nafasi za juu
 
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Nyeupee

Tunaserereka tu.
 
Na siyo Selander ni Seylander. Ndio alikuwa anaitwa John Einer Seylander 'y'baada ya e. Na hakuwa director of public works bali social climber enzi hizo za ukoloni na siyo 1929 bali 2019.

Acha kutupiga fiksi wewee
Acha uongo
Screenshot_20220202-200939.png
wewe ndio fixer mkubwa yangu lini Selander alikuwa mpanda milima?
 
kwa akili zako kweli unaweza kwenda Chato kushangaa Kaburi au uwanja na taa za barabarani?
Mobutu alijenga Globetore Nani katika huko?
Mwendazake alishaipoteza Nchi hata daraja la Busisi linaishia kwa wakwe ningekua Mimi miradi yake hiyo ningezima km alivyoisahau kusini na Gesi yake na korosho mpaka mnyooke haturudii tena kuwapa nafasi za juu
Ulishawahi kuvuka busisi wakati kivuko kimoja kibovu kati ya hivyo vitatu ukaona foleni ya hao unaowaita wakwe wa mwendazake.
 
Back
Top Bottom