Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

JPM alikuwa na msimamo gani kuhusu UN?

Umesoma kwa utulivu nilichokiandika? Nimeongelea JPM kuwa na misimamo, kwenye mambo yake, hapa tunasifia mtu kutaka kutumia kiswahili, yule alikua anakitumia, alifanya hivyo AU na EAC.
UN hakuwahi hudhuria hadi mauti inamfika.
 
Upuuzi mtupu! Tuna wizara husika, tuna ubalozi UN, kikao Cha UNGA Kiko kwenye calendar ya UN kila mwaka; walishindwaje kufanya maandalizi husika kupata mkalimani?! Wacha kutetea ujinga,

..kuzungumza Kiswahili UN inabidi ulipie.

..kuzungumza Kiingereza UN ni bure.

..pia kuna kitu kinaitwa " working language " ndani ya UN.

..working language maana yake ni lugha ambazo mtumishi wa UN anatakiwa kuzifahamu.

..sasa Kiswahili sio mojawapo ya lugha ambazo mtumishi wa UN anatakiwa kuzifahamu.

..Bahati mbaya Watanzania hatuambiani ukweli kuhusu suala hilo. Tumebakia kudanganyana tu viongozi wetu wanapohutubia kwa Kiswahili ktk mikutano mbalimbali.
 
Bado uko hai wewe, kabla ya kupost taarifa yako ipitie kwanza.
 
One of the best learned from Paskali ni ile kulike comments zenu hata kama zimeyumba (matusi) kiasi gani yeye ni kulike tu daa, 😂😂😂😂!.
 
Haya ndo matatizo ya watanzania! Hawana misimamo zaidi ya kujipendekeza! Nenda ukawanunulie wazee vikombe viwiliviwili vya kahawa!!!, nenda kawanunulie dumu la pombe washiriki uone sifa utakazomwagiwa!
Inasikitisha hata wasomi wetu wamekuwa watu wa kujipendwkeza! Hakuna weledi tena!
Nadhani hili linatokana na mifumo ya ELIMU YETU, haitutengenezi kuwa na CONFIDENCE kwenye maamuzi yetu!
 
Ile mida ya hongera hizi ndio imewadia, her this time Mama atahutubia UNGA kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, au tutaendeleza ile kasumba ya mkoloni aliotuachia?.
P
 
Watu wengine mnakaaga wapi, Yaani ufike katika Baraza la UN katika mkutano utumie lugha yako, si ungebaki nyumbani kwako

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mkuu Alvin Slain, wewe mwenzetu umewahi kufika UN kwenye kikao cha Baraza Kuu, ukasikia viongozi wa mataifa wanahutubia kwa lugha gani?. Lugha rasmi za UN ni 6, English, French, Spanish Arabic, Chinese na Russian, je mataifa wasio tumia lugha hizo, jee viongozi wao wanahutubia UNGA kwa lugha gani?

P
 
 
HBD Rais Samia!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…