Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Sasa mbona nimelitafuta ila sijaliona, nilitaka ni post huko!!
Kule mpka uombe kuunganishwa na mods haliko public km majukwaa mengine ndo maana!
.so ukiomba ukaingia huko ,mfano hii madam hapa Kwa ambao hawapo huko hawataiona!

Ndo shida ,ila walioko kule wanaliona hii .
So watakuja tu naamini
 
Roho Mtakatifu ndie hukupa tofauti na msisimko kwenye maandiko. Ukiongozwa nae kila siku utaona unavutiwa kusoma kitu kile kike lakini kwa msisimko tofauti na mafunuo tofauti. Otherwise utaona biblia ni kama gazeti tu.
Ahsante, nafikiri hapa ndipo napahitaji. How do i come to this point!?
 
  • Thanks
Reactions: 511
Inawezekana hapa si mahala pake lakini ningependa kusaidiwa na wahusika ambao najua wapo hapa.
Ni vile nimelitafuta jukwaa la dini katika forums zilizopo na sijaliona.

HIvi, mantiki ya kusoma Biblia iko wapi? Kwakifupi tu ni kwamba sisi wengine (kama walivyo wengi) tumezaliwa katika dini. Kanisani nakwemda toka sijitambui mpaka najielewa hivi.
Nikiwa mtoto mdogo kabisa nimeshashika tayar amri zoote kulingana na utaratibu wa kanisa ambalo nimekua nikisali (ambalo nimekuta wazaz wanasali nami nikafuata humo, though baada ya kuoa nikaamua kubadili mwelekeo na ninasali kanisa lenye mlengo mwingine, japo ni ukristo tu kama ambavyo nilizaliwa).

Sasa miaka yoote hii, tika sijui kusoma, nimekua nikisia mahubiri, maandiko ya biblia, mpaka nafikia kujua kusoma ,ujana na sasa utu uzima, nimekua nikisikia na kusoma habar za Mungu na Yesu na mitume wake na historia yao nzima katika maandika na hii imenifanya kuwa kama naijua biblia.

Sio yote in such na sijawahi kuisoma yoote kimfululizo nikaimaliza but ile kugusa hapa na pale na kusikiliza na kusikiliza, tena na tena all my life mpaka sasa third floor ya umri. Na hii imenifanya kwamba, 90% ya chochote utakacho au yeyote yule atakayezungumza kuhusu maandika ya Biblia, NAVIJUA.

Hali hii kiukwel, inanitaabisha sana.
Maana hata leo asubuh nilipochukua biblia nisome (maana niko kwenye maombi yangu tu binafsi) honestly,nimejikuta kuboreka kias flan na ndio likanijua swali hili nikajiuliza, NASOMA MAANDIKO HAYA ILI IWEJE?? ILI NIPATE NINI??MBONA SIONI KIPYA, I KNOW THESE STUFFS, AU KUNA NAMNA LABDA NAPASWA KUISOMA KIUTOFAUTI BUT HOW?
ndio namuomba Mungu kabla ya kusoma but MBONA NILICHOKIONA JANA NA JUZI NDIO HIKI HIKI AMBACHO TAYARI NAKIJUA???...

kuna ulazima gani wa kuendelea kusoma mambo ambayo tayar nimekua nikiyasikia na kusoma miaka mingi mpaka leo??...

Kuna kitu watu huwa nasikia wakisema na pia naamini inawezekana, kknaitwa REVELATION /UFUNUO(MAFUNUO). how do i come to this point.

Yan kwamfano leo nimeanza kusoma Mathew Chapter 2, ile kuanza tu habari kuzaliwa kwa Kristo, akilini tayari ufahamu wangu ukajawa na ile flow nzima ya matukio mpaka mpaka kufa kwake, sasa najiuliza, NIENDELEE KUSOMA ILI IWAJE??????..

Wakuu wenye dini na imani, naomba mawazo na kusaidiwa katika hili.

Natangukiza shukrani.
Rabbon Tayana-wog Carleen matunduizi na wengine wote

View attachment 3032379
Labda nikupe muongozo kidogo, Wakatoliki wote yani Roman, Anglican na Lutheran wana Liturujia, kwenye liturujia kuna injili ya mwaka mzima.

Wanachofanya wachungaji wenye bible knowledge ni kukufafanulia injiri ya siku husika kutokana na lugha ngumu ya kibiblia, kuna kiswahili cha zamani na kiswahili cha kisasa.

Kama kuna sehemu kanisa la Roman Catholic wameferi ni kwenye kuhubiri injiri, hapo ndipo kina Mwamposa walipowapiga bao achana na kuombea wagonjwa na miujiza, watu wa kariba ya Mwamposa akihubiri injiri anaeleweka vizuri.

Makanisa katoliki yamebase kwenye misa retuals, ndio maana Lutheran na Anglican wana wainjilist wao kazi yao ni kuhubiri injili tu kwenye misa, mchungaji au Padre afanye jukumu la kusalisha misa tu, huwezi kusinzia wakati Mwamposa anahubiri injili.

Biblia ya kujisomea mwenyewe tu bila wainjilishaji huwezi kuelewa kitu zaidi ya kuzaliwa kuteswa kufa na kufufuka kwa Yesu tu, itaielewa injili ya Luka labda na matendo ya mitume kwingine utatoka kapa.
 
Biblia huna haja ya kuisoma mara nyingi ikiwa tayari unaijua.
Kwakwel nimejiuliza sana kuhusu hili suala leo
Vinginevyo utaona uko bored ukifika Kanisani kwa sababu mambo mengi 99% ni marudio na unayajua
Hii naungana na wewe kwa 100%.
Very boring.
I only like prayer time binafsi maana hapa angalau unakua una agenda zaki kila siku mpya, ila mengine naonaga ni yale yale tu
 
Neno la Mungu ni lile linalokuwa moyoni mwako.

Biblia huna haja ya kuisoma mara nyingi ikiwa tayari unaijua.

Soma vitabu vingine hasa vile walivyovitoa, soma Quran, ongeza ujuzi na maarifa

Hata Kanisani sio pakwenda kama tayari umefika level fulani ya ufahamu.
Labda upeleke watoto nao wakajifunze.
Vinginevyo utaona uko bored ukifika Kanisani kwa sababu mambo mengi 99% ni marudio na unayajua
Kule tunaenda kukumbushwa jinsi ya kuyaishi hayo maandiko.unaporudia kusoma neno now and then unakifanya kichwa kukumbuka kiurahisi.
 
Jibu zuri kaka..
Na mimi nimesema hapo nikatoa mfano, leo i was about to read certain chapter in nee testament, lakin nikaboreka maana nikafikiri, mbona hiz bmhabar zote nishazisoma na kuzisikia, sasa nisome tena ili iweje????

Ndio maana naukiza, au kuna namna mpya ya kusoma napaswa kuifahamu?
Biblia ni kitabu kinachokufundisha historia ya dini yako. Baada ya kuisoma yote na KUIELEWA hakuna kipya utakachojifunza, kilichobakia ni kutekeleza/kufanya kwa vitendo vile ulivyojifunza katika biblia. Funga, fanya maombi, toa sadaka.

Unataka kusoma zaidi? Soma vitabu vya imani za dini nyingine, unaweza kusoma Quran. Itakuongezea kitu, unaweza kufanya kama unajiuliza swali hivi, vipi kama ningezaliwa katika familia ya Kiislamu? Ngoja nisome Quran nione ningekuwa mtu wa namna gani kiimani, pia nijifunze elimu gani ningeipata katika Quran.

Ni ushauri kutoka kwangu Mkristo mwenzio!​
 
Huwa inasema hii kila siku, na kwa namna flan naweza amini BUT,

ndio maana nikajiuliza leo ,inabid iweje ili mtu uwe unasoma katika namna isiyoitwa scanning?? Yan nisome vipi, kwamfano wewe how do you do it??

How this??? Maana binafs mpaka leo kufikia hatua hii ni kwamba am fed up!! Naona kabisa kuna kitu am missing katika usomaji probably maana mbona habar hiz ni zile zile, zinawezaje zikafanyika upya kunipatia ufaham mpya everytime??

How do you do it??
Kwanza naomba ujue hii hali Haikukuti pekee yako.. Ni rahisi mtu kuomba Lakini sio rahisi kusoma neno.. ni struggle.. inawezakana tunaongea kwa wepesi ila ni kitia nia kwamba nataka kusoma na kuelewa neno.. unapolisoma unakuwa na uhitaji wa kupata kitu kutoka kile unachokisoma.. pia neno hilo hilo unaweza ukalisoma Kwa sauti kama upo mwenyewe.. rudia rudia ule mstari utajikuta tu unapata insight katika kile unachoma..


Mfano mimi nilisoma hili neno la Yohana 3:16.
16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.



Kwa sauti na nilikuwa na wasomea watoto kadri nilivyo lisoma Kwa nguvu na kulirudia nikajikuta napokea kitu kingine tofauti na nilivyolizoea..

Yaani wakati nalisoma likajichambua.. Kwa namn hii.. Yaani Mungu (huyu aliyeumba mbingu na nchi na binadamu)alinipenda kiasi akamtoa Mwana wa pekee ili nisipotee bali niwe na uzima wa milele..


So nimetoa tu namna ambavyo ukilisoma tofauti na mazoea utakapokea pia kitu tofauti na ulivyoluwa unalichukulia.. na hapo ndipo neno linakiwa na maana kwako..
 
Mwakasege ni mwalimu mzuri sana,na anaweza kua na majib ya maswali yako yote, mimi hupenda kumfatilia.
Uko sahihi Ms R lakini hata mimi nilikua na mtazamo huu na pia sio kwamba yeye si mwalim mzuri hata sasa no, but nilipoanza kuwafuatilia watu wengine haswa wa nje mfano Dr. Myles Monroe, nikaja kuanza kuona kumbe hata hawa akina mwakasege pia wanajifunza vitu vingi toka hukoo so nimepunguza kidogo kumfuatilia maana vingi ambavyo nimekua nikimsikia, nikagundua bimeshaongelewa na watu miaka mingii sanaa, yan ni sio vipya japo kwa huku kibongo bongo vinaonekana vipya
 
Biblia ni kitabu kinachokufundisha historia ya dini yako. Baada ya kuisoma yote na KUIELEWA hakuna kipya utakachojifunza, kilichobakia ni kutekeleza/kufanya kwa vitendo vile ulivyojifunza katika biblia. Funga, fanya maombi, toa sadaka.

Unataka kusoma zaidi? Soma vitabu vya imani za dini nyingine, unaweza kusoma Quran. Itakuongezea kitu, unaweza kufanya kama unajiuliza swali hivi, vipi kama ningezaliwa katika familia ya Kiislamu? Ngoja nisome Quran nione ningekuwa mtu wa namna gani kiimani, pia nijifunze elimu gani ningeipata katika Quran.

Ni ushauri kutoka kwangu Mkristo mwenzio!​
Ukisoma ukimaliza hakuna jipya.. Narudia neno la Mungu ni jipya kila siku.. unaweza ukatumia warumi 8:11 leo mfano Kwa case ya uponyaji afu ukalitumia kesho wala lisikupe matunda unayo tarajia ukaona Mungu sio mtendaji.. Na ndio maana ni vyema ukajifunza kusoma neno kila siku
 
Nilishawahi kupata hii experience pia ila mimi nilienda mbali zaidi kuna kipindi hadi kanisani nilikua sioni jipya.

Saivi niko kwenye mzunguko wa pili (mwanzo mpaka mwisho, word by word), Ila mafunuo ni tofauti kabisa ni kama sikuwahi kusoma. Mwanzo nilipata tabu sana (nahisi ndipo ulipo wewe) ila nikaanza chagua vitabu vyepesi kama zaburi, mithali mpaka unamaliza yote. Na pia niligundua it always speaks to your current situation.
Sizani kama kuna namna maalumu ya kusoma, wewe endelea tu kusoma hivyo hvyo utakuja kupata mafunuo.
 
Utapata majibu sawa na Altar ( Lango ) unayojiunganisha.

Wajuzi watamalizia.
Mkuu naweza kubaliana na wewe na hapa pia nafikiri kuna tatizo kubwa sana, about the altar. Kuna mahala mimi nikitoa sadaka mambo yanakwenda vyema, na kuna mahala inakua kama mikosi.
Haya mambk siri yake ni nini, ndio maana i really want to know myself sio ku depend on people be telling me what to do? I believe in my heart kwamba kuna siri katika maandiko but hiw doni crack them?
 
Kuna watu wanasema soma na vitabu vingine.. usifanye hilo kosa.. wewe kama mkristo soma kile kinachohusiana moja Kwa moja na imani yako.. usije ukacorrupt imani yako
 
Nimekusoma chief, ila kwa hapa mimi nafikiri hii kitu nahitaji kujua zaidi.. level niliopo nimekaa na kugundua kwamba, i know the stories na histories but WHAT IS THE ESSENCE of all this stuffs???

Essence ya simulizi zote hizo ni power na authority ya kutawala nafsi na roho za watu.
 
Nilishawahi kupata hii experience pia ila mimi nilienda mbali zaidi kuna kipindi hadi kanisani nilikua sioni jipya.
Yah niko kwenye situation hiyo pia na hata kanisan kwasasa niwe mkwel naemda kwa manat sana ili tu watoto wasipate confusion
Saivi niko kwenye mzunguko wa pili (mwanzo mpaka mwisho, word by word), Ila mafunuo ni tofauti kabisa ni kama sikuwahi kusoma. Mwanzo nilipata tabu sana (nahisi ndipo ulipo wewe) ila nikaanza chagua vitabu vyepesi kama zaburi, mithali mpaka unamaliza yote. Na pia niligua it always speaks to your current situation.
Sizani kama kuna namna maalumu ya kusoma, wewe endelea tu kusoma hivyo hvyo utakuja kupata mafunuo.
Ahsante sana
 
  • Thanks
Reactions: I M
Me sina hata majibu ya kukupa ila mwamba mmoja hivi huwa mafundisho yake ni ya kitofauti kabisa ngoja nikikumbuka jina lake ntalikupa upate mwanga
Fanya hivyo tajiri angu
 
Ahsante, nafikiri hapa ndipo napahitaji. How do i come to this point!?
Matendo ya Mitume 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁷ Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? (how do i came to this point?)
³⁸ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
 
Back
Top Bottom