Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Sasa hicho kifungu kimoja tu cha Yohana, muinjirishaji anaweza akatumia masaa mawili kwenye crusade kukifafanuwa bila wasikilizaji kuboreka, au Mwakasege kifungu hicho tu kimoja kinaweza kuwa ndio somo lake kwa siku hiyo.Kwanza naomba ujue hii hali Haikukuti pekee yako.. Ni rahisi mtu kuomba Lakini sio rahisi kusoma neno.. ni struggle.. inawezakana tunaongea kwa wepesi ila ni kitia nia kwamba nataka kusoma na kuelewa neno.. unapolisoma unakuwa na uhitaji wa kupata kitu kutoka kile unachokisoma.. pia neno hilo hilo unaweza ukalisoma Kwa sauti kama upo mwenyewe.. rudia rudia ule mstari utajikuta tu unapata insight katika kile unachoma..
Mfano mimi nilisoma hili neno la Yohana 3:16.
16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Kwa sauti na nilikuwa na wasomea watoto kadri nilivyo lisoma Kwa nguvu na kulirudia nikajikuta napokea kitu kingine tofauti na nilivyolizoea..
Yaani wakati nalisoma likajichambua.. Kwa namn hii.. Yaani Mungu (huyu aliyeumba mbingu na nchi na binadamu)alinipenda kiasi akamtoa Mwana wa pekee ili nisipotee bali niwe na uzima wa milele..
So nimetoa tu namna ambavyo ukilisoma tofauti na mazoea utakapokea pia kitu tofauti na ulivyoluwa unalichukulia.. na hapo ndipo neno linakiwa na maana kwako..
Sasa mtu anasoma vitabu kadhaa ndani ya biblia kwa masaa tu unategemea ataelewa nini zaidi ya maluweluwe.
Biblia inasema ukiwa na imani unaweza kuamuru mlima uhame na ukahama, sasa kwa akili zako timamu unadhani kuna imani ya kuhamisha mlima kilimanjaro?
Sasa hapo ndio kazi ya Wainjiristi mlima ni mfano tu lakini ukiwa na imani unaweza kufanya abcd.