Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Kuna tofauti ya kusoma Biblia na kusoma kitabu cha historia. Kusoma Biblia kunahitaji kutafakari, kusoma kitabu cha historia kunahitaji kuweka kumbukumbu (kama unavyosema Biblia kwa sasa).
Acheni kuipa dini ugumu hivi. Mungu hajafanya dini kuwa ngumu kiasi hiki mnachoaminisha watu. Haihitaji tafakari yoyote kuisoma biblia, zingine ni mbwembwe tu za hapa na pale!
 
Ongera umeingia ktk hatua nzuri ya kuanza kutumia akili, hata sisi tulianza kama wewe kutilia shaka hata maandiko na mashaka haya yanaambatana na kuanza kuhoji uhalali na undani wa hizi dini na maandiko yake, ukishaanza kuhoji utatukanwa sana na hawa makondoo waliofungwa na hizi dini, bila kusahau wapo watakao kuhukumu kwa kukuita wewe mpinga kristo sijui nani ilimladi kukutisha na kukustopisha usiendelee kuhoji, wanaamini eti hizo biblia hazitakiwi kuhojiwa.

Ukweli ni kuwa tuko ktk zama za tofauti na hizo ambazo baba na babu zetu waliaminishwa upumbavu bila ya kuhoji wala kutumia akili,

Dini zote ni uzushi zimetungwa kwa kuiba historia za waafrika walioishi maelfu ya miaka kabla hata hao wazungu na waarabu hawajaja hapa dunian.

Asikudanganye mtu kuwa biblia ili uelewe lazima uongozwe na huyo Roho mtakatifu wa kutungwa huo ni uongo wa kukufunga ili usihoji mikanganyiko ya hizo stories zao za kishenzi za biblia na quran.

Biblia na hizo takataka zingine ili uelewe lazima utumie akili timamu wala haihitaji Roho wala usaidizi wa hayo maMiungu/mamizimu ya Wazungu ili uelewe.

Ni suala la muda tu miaka 10 na kuendelea baadae hizi dini zenu zitakosa mvuto na wafuasi hivyo zitabaki kama makumbusho ya utalii jinsi gani hizo dini zilivyopumbaza wengi, Ushahidi ni huu wa watu kuanza kuamka na kuondoa uoga kwa kuhoji hizo biblia, bila kusahau watoto wa kizazi hiki wameshaachana na hizo dini wamebaki kulazimishwa na wazazi, so baada ya miaka kadha ya hawa wazazi wao wanaowalazimisha kupotea dunian, hapa ndipo akili na uhuru wa hiki kizazi utaonekana waziwazi kuzipoteza hizo dini zenu za kishetani.

Amkeni nyie watumwa wa mila za wageni, Muumba wa kweli haitaji hizo takataka za biblia na Quran ili umjue, haitaji dini ili umjue wala haitaji mila za wageni ili umjue, mnapoteza muda wenu bure kuamini hayo maujinga ya bible.
 

Attachments

  • 1651591598606.jpg
    1651591598606.jpg
    183 KB · Views: 2
  • 1650890440636.jpg
    1650890440636.jpg
    427.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20230226-141254.png
    Screenshot_20230226-141254.png
    360.7 KB · Views: 2
Hakuna dhambi mpya dhambi zote Kristu alishazifia pale Msalabana kwa hio wewe ni kiumbe kipya kisicho na dhambi na kisichotenda dhambi
Kwahiyo ukila malaya saa hii hiyo sio dhambi?
 
Inawezekana hapa si mahala pake lakini ningependa kusaidiwa na wahusika ambao najua wapo hapa.
Ni vile nimelitafuta jukwaa la dini katika forums zilizopo na sijaliona.

HIvi, mantiki ya kusoma Biblia iko wapi? Kwakifupi tu ni kwamba sisi wengine (kama walivyo wengi) tumezaliwa katika dini. Kanisani nakwemda toka sijitambui mpaka najielewa hivi.
Nikiwa mtoto mdogo kabisa nimeshashika tayar amri zoote kulingana na utaratibu wa kanisa ambalo nimekua nikisali (ambalo nimekuta wazaz wanasali nami nikafuata humo, though baada ya kuoa nikaamua kubadili mwelekeo na ninasali kanisa lenye mlengo mwingine, japo ni ukristo tu kama ambavyo nilizaliwa).

Sasa miaka yoote hii, tika sijui kusoma, nimekua nikisia mahubiri, maandiko ya biblia, mpaka nafikia kujua kusoma ,ujana na sasa utu uzima, nimekua nikisikia na kusoma habar za Mungu na Yesu na mitume wake na historia yao nzima katika maandika na hii imenifanya kuwa kama naijua biblia.

Sio yote in such na sijawahi kuisoma yoote kimfululizo nikaimaliza but ile kugusa hapa na pale na kusikiliza na kusikiliza, tena na tena all my life mpaka sasa third floor ya umri. Na hii imenifanya kwamba, 90% ya chochote utakacho au yeyote yule atakayezungumza kuhusu maandika ya Biblia, NAVIJUA.

Hali hii kiukwel, inanitaabisha sana.
Maana hata leo asubuh nilipochukua biblia nisome (maana niko kwenye maombi yangu tu binafsi) honestly,nimejikuta kuboreka kias flan na ndio likanijua swali hili nikajiuliza, NASOMA MAANDIKO HAYA ILI IWEJE?? ILI NIPATE NINI??MBONA SIONI KIPYA, I KNOW THESE STUFFS, AU KUNA NAMNA LABDA NAPASWA KUISOMA KIUTOFAUTI BUT HOW?
ndio namuomba Mungu kabla ya kusoma but MBONA NILICHOKIONA JANA NA JUZI NDIO HIKI HIKI AMBACHO TAYARI NAKIJUA???...

kuna ulazima gani wa kuendelea kusoma mambo ambayo tayar nimekua nikiyasikia na kusoma miaka mingi mpaka leo??...

Kuna kitu watu huwa nasikia wakisema na pia naamini inawezekana, kknaitwa REVELATION /UFUNUO(MAFUNUO). how do i come to this point.

Yan kwamfano leo nimeanza kusoma Mathew Chapter 2, ile kuanza tu habari kuzaliwa kwa Kristo, akilini tayari ufahamu wangu ukajawa na ile flow nzima ya matukio mpaka mpaka kufa kwake, sasa najiuliza, NIENDELEE KUSOMA ILI IWAJE??????..

Wakuu wenye dini na imani, naomba mawazo na kusaidiwa katika hili.

Natangukiza shukrani.
Rabbon Tayana-wog Carleen matunduizi na wengine wote

View attachment 3032379
Unatakiwa usome Ili ujue kuwa Yesu alisema Ili update uzima wa milele lazima uamini kuwa Mungu ni mmoja na yeye Yesu ni nabii tu aliyetumwa na huyo Mungu mmoja

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Pia unatakiwa ujue kuwa Yesu mwenyewe alikuwa anamuomba na kumsujudia huyo Mungu mmoja

Mathayo 26:39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Ila jambo la kushangaza hapo ukiamini hayo Maneno ya Yesu ya Yohana 17:3

Na ukifanya vitendo alivuovifamya Yesu katika hiyo Mathayo 26:39
alipokuwa anamuomba na kumsujudia Mungu wake automatically unageuka kuwa Muislam
 
Kwahiyo ukila malaya saa hii hiyo sio dhambi?
Sio dhambi Ila km ulikuepo enzi Musa na Torati kabla ujio wa Yesu hio ni dhambi kwa mujibu wa Amri za Torati ya Musa

Yesu alizifia dhambi hizo pale Msalabana akatutakasa kuanzia hapo hakuna dhambi
 
Acheni kuipa dini ugumu hivi. Mungu hajafanya dini kuwa ngumu kiasi hiki mnachoaminisha watu. Haihitaji tafakari yoyote kuisoma biblia, zingine ni mbwembwe tu za hapa na pale!
Acheni pia ku'simplify' dini to the extent ya kufanya dini isiwe/ikose maana. To make religion too simple to have any meaning in your life. Acheni kufanya hivyo pia.
 
Matendo ya Mitume 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁷ Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? (how do i came to this point?)
³⁸ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Sawa sawa chief..
Ngoma inakuja sasa tayar ushatubu ,mbona bado kasheshe zinakua nyingi??
 
  • Thanks
Reactions: 511
Acheni kuipa dini ugumu hivi. Mungu hajafanya dini kuwa ngumu kiasi hiki mnachoaminisha watu. Haihitaji tafakari yoyote kuisoma biblia, zingine ni mbwembwe tu za hapa na pale!
Kwa Mungu hakuna Dini Dini ni creation ya mwanadamu km ilivyo kwamba mbinguni kwa Mungu hakuna usiku hakuna Mchana hakuna majira hakuna saa kuna Nuru ya Uzima tu kwa hio suala Dini halimuhusu Mungu linamuhusu mwanadamu mwanadamu ndie alietengeneza Dini
 
Sawa sawa chief..
Ngoma inakuja sasa tayar ushatubu ,mbona bado kasheshe zinakua nyingi??
Unatubu nini wakati huna dhambi? Dhambi zako Yesu mwenyewe Yesu alishatubu kwa ajili yako pale Msalabana "Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo" sasa wewe unatubu nini wakati Yesu alishamaliza kila kitu pale Msalabana au Wewe ni Mkristu Jina?
 
Ila jambo la kushangaza hapo ukiamini hayo Maneno ya Yesu ya Yohana 17:3

Na ukifanya vitendo alivuovifamya Yesu katika hiyo Mathayo 26:39
alipokuwa anamuomba na kumsujudia Mungu wake automatically unageuka kuwa Muislam
Sasa hapa chief, hii inaweza kunivuruga zaid, kwamba unageuka muislam?
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Sio dhambi Ila km ulikuepo enzi Musa na Torati kabla ujio wa Yesu hio ni dhambi kwa mujibu wa Amri za Torati ya Musa

Yesu alizifia dhambi hizo pale Msalabana akatutakasa kuanzia hapo hakuna dhambi
Lakin Maandika hayo hayo yanam quite Yesu akisema "hakuja kubadilo wa kutengea torati wala manabii". Kwamba kila kitu kakiacha kama alivyokikuta, hii imekaaje??
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Uko sahihi Ms R lakini hata mimi nilikua na mtazamo huu na pia sio kwamba yeye si mwalim mzuri hata sasa no, but nilipoanza kuwafuatilia watu wengine haswa wa nje mfano Dr. Myles Monroe, nikaja kuanza kuona kumbe hata hawa akina mwakasege pia wanajifunza vitu vingi toka hukoo so nimepunguza kidogo kumfuatilia maana vingi ambavyo nimekua nikimsikia, nikagundua bimeshaongelewa na watu miaka mingii sanaa, yan ni sio vipya japo kwa huku kibongo bongo vinaonekana vipya
Hata walimu wazuri wa mashuleni walifundishwa na walimu wa zaman hata wafanyakaz pia,,mimi mwakasege hua namwelewa sana.
 
Unatubu nini wakati huna dhambi? Dhambi zako Yesu mwenyewe Yesu alishatubu kwa ajili yako pale Msalabana "Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo" sasa wewe unatubu nini wakati Yesu alishamaliza kila kitu pale Msalabana au Wewe ni Mkristu Jina?
😁😁
 
Back
Top Bottom