Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Enendeni huku mkijitafakari.

Mwana wa adamu atachoka kurudia maandiko matakatifu,
Naye hatochoka kurudia dhambi afanyayo kila siku.

Amin amin maandiko matakatifu hayana mwisho na hayakuwa na mwanzo,
Kwani siku zote yatokayo ndani mwake ni makumbusho na ni ufunguo,

Enyi mliokwisha kukalili yote basi nanyi mkayaaishi yote yaliyoandikwa, haijalishi ni Quran au Biblia.

Ameen 🙏
 
Kwa hiyo, umeandika nini sasa? Kusema wewe ni Mkristo ina mchango/maana gani kuhusiana na swali alilouliza aliyeanzisha uzi huu? Kama ukisoma bila kutafakari ina maana unasoma bila kupata maana ya kile unachokisoma - yaani kusoma kama kasuku. Kusoma kwa kutafakari ni kusoma kwa kutumia akili/intelligent reading au reflection. Sasa wewe unasema tusome Biblia bila kutumia akili, siyo? Mimi siwezi kufanya hivyo na wala siwezi kumshauri mtu anahitaji ushauri namna hiyo. Kukosoma Biblia bila kutafakari ni kama kutafuta kitu mchangani huku umefumba macho. Kwa Kiingereza ningeweza kusema unintelligent reading of the Bible na hakuna kitu kibaya kama kufanya hivyo. Mungu amekupa rational facultities na inabidi tuzitumie na siyo kusoma blindly.
Acha porojo bhana!!!

Unauliza nimeandika nini kwakuwa umesoma andiko langu bila kutumia akili.

Mtu ameweza kutumia akili kuweka uzi JF useme anashindwa kutumia akili hiyohiyo kuisoma Biblia, acha dharau!
Kuandika huu uzi tu ametumia nguvu kubwa kuliko nguvu anayotakiwa kuitumia kuisoma Biblia.
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Acha porojo bhana!!!
Mtu ameweza kutumia akili kuweka uzi JF useme anashindwa kutumia akili hiyohiyo kuisoma Biblia, acha dharau!
Kuandika huu uzi tu ametumia nguvu kubwa kuliko nguvu anayotakiwa kuitumia kuisoma Biblia.
Si ndivyo unavyotaka wewe? Sasa unaposema tusome Biblia bila kutafakari maana yake ni nini? Hebu eleza hapa. Nasubiri.
 
Si ndivyo unavyotaka wewe? Sasa unaposema tusome Biblia bila kutafakari maana yake ni nini? Hebu eleza hapa. Nasubiri.
Soma kama unavyosoma masimulizi/hadith zingine, unataka kutafakari nini sasa na kitu umekisoma zaidi ya mara 10?
 
Labda nikupe muongozo kidogo, Wakatoliki wote yani Roman, Anglican na Lutheran wana Liturujia, kwenye liturujia kuna injili ya mwaka mzima.

Wanachofanya wachungaji wenye bible knowledge ni kukufafanulia injiri ya siku husika kutokana na lugha ngumu ya kibiblia, kuna kiswahili cha zamani na kiswahili cha kisasa.

Kama kuna sehemu kanisa la Roman Catholic wameferi ni kwenye kuhubiri injiri, hapo ndipo kina Mwamposa walipowapiga bao achana na kuombea wagonjwa na miujiza, watu wa kariba ya Mwamposa akihubiri injiri anaeleweka vizuri.

Makanisa katoliki yamebase kwenye misa retuals, ndio maana Lutheran na Anglican wana wainjilist wao kazi yao ni kuhubiri injili tu kwenye misa, mchungaji au Padre afanye jukumu la kusalisha misa tu, huwezi kusinzia wakati Mwamposa anahubiri injili.

Biblia ya kujisomea mwenyewe tu bila wainjilishaji huwezi kuelewa kitu zaidi ya kuzaliwa kuteswa kufa na kufufuka kwa Yesu tu, itaielewa injili ya Luka labda na matendo ya mitume kwingine utatoka kapa.
Injiri❌
Injili✅
Kuferi❌
Kufeli✅
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana humu ndani!
Watu wanataka tusome Biblia kama tunajiandaa na UE, tena huu sio upotoshaji tu ni roho mbaya kabisa.​
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Inawezekana hapa si mahala pake lakini ningependa kusaidiwa na wahusika ambao najua wapo hapa.
Ni vile nimelitafuta jukwaa la dini katika forums zilizopo na sijaliona.

HIvi, mantiki ya kusoma Biblia iko wapi? Kwakifupi tu ni kwamba sisi wengine (kama walivyo wengi) tumezaliwa katika dini. Kanisani nakwemda toka sijitambui mpaka najielewa hivi.
Nikiwa mtoto mdogo kabisa nimeshashika tayar amri zoote kulingana na utaratibu wa kanisa ambalo nimekua nikisali (ambalo nimekuta wazaz wanasali nami nikafuata humo, though baada ya kuoa nikaamua kubadili mwelekeo na ninasali kanisa lenye mlengo mwingine, japo ni ukristo tu kama ambavyo nilizaliwa).

Sasa miaka yoote hii, tika sijui kusoma, nimekua nikisia mahubiri, maandiko ya biblia, mpaka nafikia kujua kusoma ,ujana na sasa utu uzima, nimekua nikisikia na kusoma habar za Mungu na Yesu na mitume wake na historia yao nzima katika maandika na hii imenifanya kuwa kama naijua biblia.

Sio yote in such na sijawahi kuisoma yoote kimfululizo nikaimaliza but ile kugusa hapa na pale na kusikiliza na kusikiliza, tena na tena all my life mpaka sasa third floor ya umri. Na hii imenifanya kwamba, 90% ya chochote utakacho au yeyote yule atakayezungumza kuhusu maandika ya Biblia, NAVIJUA.

Hali hii kiukwel, inanitaabisha sana.
Maana hata leo asubuh nilipochukua biblia nisome (maana niko kwenye maombi yangu tu binafsi) honestly,nimejikuta kuboreka kias flan na ndio likanijua swali hili nikajiuliza, NASOMA MAANDIKO HAYA ILI IWEJE?? ILI NIPATE NINI??MBONA SIONI KIPYA, I KNOW THESE STUFFS, AU KUNA NAMNA LABDA NAPASWA KUISOMA KIUTOFAUTI BUT HOW?
ndio namuomba Mungu kabla ya kusoma but MBONA NILICHOKIONA JANA NA JUZI NDIO HIKI HIKI AMBACHO TAYARI NAKIJUA???...

kuna ulazima gani wa kuendelea kusoma mambo ambayo tayar nimekua nikiyasikia na kusoma miaka mingi mpaka leo??...

Kuna kitu watu huwa nasikia wakisema na pia naamini inawezekana, kknaitwa REVELATION /UFUNUO(MAFUNUO). how do i come to this point.

Yan kwamfano leo nimeanza kusoma Mathew Chapter 2, ile kuanza tu habari kuzaliwa kwa Kristo, akilini tayari ufahamu wangu ukajawa na ile flow nzima ya matukio mpaka mpaka kufa kwake, sasa najiuliza, NIENDELEE KUSOMA ILI IWAJE??????..

Wakuu wenye dini na imani, naomba mawazo na kusaidiwa katika hili.

Natangukiza shukrani.
Rabbon Tayana-wog Carleen matunduizi na wengine wote

View attachment 3032379
Kwa kawaida, Kila mwaka unatakiwa usome BIBLIA mwanzo Hadi ufunuo na kuimaliza,

Ukimaliza kuisoma, nunua mpya uanze kuisoma tena January Hadi December Mwanzo Hadi ufunuo umalize.

BIBLIA Si kitabu kama vitabu vingine,

BIBLIA ni Neno la Mungu, ni Pumzi ya Mungu, BIBLIA ni kuongea na Mungu na kuisikia sauti yake kupitia Neno lake. Hivyo huwezi kumuelewa Mungu siku moja au mwaka mmoja, ni lifetime process, ni milele na milele

Katika BIBLIA, unaweza kusoma mstari mmoja pekee na ukajikuta unapata mafunuo yanayoweza kujaa kwenye kitabu kizima.

Kusoma BIBLIA ni kuongea na Mungu kupitia Roho mtakatifu, hivyo ujisoma Kwa Roho, sahau kuchoka au kuizoea.


BIBLIA, Neno la Mungu ni chakula Cha Roho ambayo ndio wewe mwenyewe.
Sasa kusema kuwa umesoma na kuimaliza na hujisikii kusoma tena na tena, ni sawa na kusema kuwa nimekula vyakula vyote duniani na sijusikii kula tena kesho, Hilo Haiwezekani. Kula chakula Cha mwili na Roho ni suala la Kila siku,

Kumeditate, kutafakari neno la Mungu ni mchana na usiku 24/7.

Omba Mungu akupe kusoma Kwa Roho, kamwe hutotamani kuacha kusoma BIBLIA.

Mungu akubariki. Amen
 
Nimesoma full Biblia mara nne, sasa almost namalizia kuisoma kwa mara ya tano.

Japo kwa mara ya kwanza mpaka ya tatu nilikuwa sielewi, sasa ndivyo ninazidi kuielewa.

Bible ni ngumu sana kusoma, sometimes unasinzia unalala unaamka unaendelea kusoma tena.

Ayubu 22: 21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
 
Mathayo 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
¹⁸ Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.


Naomba kuuliza.
Nikiua sasa hivi sihesabiwi dhambi?
Inabidi upate ufahamu sahihi wa nini maana ya mwanadamu kua ndani ya Kristo na Kristo kua ndani ya mwanadamu(Kuokoka),ufahamu wa dhambi kwake,ufahamu wa haki nk(yaani mafundisho ya Kristo na kumfanania yeye maana ametuita tufanane nae)
Sikiliza hizi audio chache,ya 3 ina jibu la huo mstari hapo uliouandika.


 
Ili uweze kusoma kitabu (biblia) na kuelewa au kupata ufahamu wa juu zaidi lazima uyajue yafuatayo:-

1.Majira saba za kanisa na manabii waliongoza majira hizo.

2.Hatua kumi za uumbaji.

3.Vizazi vinne vya kanisa toka kiuno cha Ibrahimu na walioongoza hivyo vizazi.

4.Nyota 12 zilikatika ufunuo 12:1.

Sababu kila kilichoandikwa katika biblia kiliandikwa kitimie maana Muumba anafanya kazi kwa majira au wakati.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Zekaria 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
 
Carleen umeitwa huku, mama mchungaji wangu.
Nimeitikia wito baba mchungaji wangu,

Ivan,
Nimesoma comments, wengi wamekushauri vyema kabisa..!! Neno la Mungu wetu ni jipya kila iitwapo Leo, Neno la Mungu halizoeleki, halichuji, wala haliboi kabisa..!!

Unaiona tofauti sababu unalisoma Neno la Mungu kama unasoma hizi makala nyingine, huwa unasoma Neno mpaka unahisi 'mtetemo' flani hivi kwenye moyo wako..? Unaona kabisa hichi hasa ndiyo hasa ulitamani kukisikia kwa wakati huo..? Ama unasoma Neno kana kwamba unasoma Jibu la kilichokuwa kinakutatiza hasa kwenye maisha yako..?

Kama jibu lako ni Hapana, basi itafute hasa kuijua nguvu iliyopo kwenye Neno la Mungu, Biblia inasema Neno la Mungu ni Pumzi ya Mungu, maana yake siyo maneno tu Hapana, ila ni maneno yenye 'uhai' ndani yake..!!

Hivyo basi ili uielewe Biblia vizuri inakubidi ukae darasani kwa Roho Mtakatifu na umruhusu akufundishe vile apendavyo yeye mwenyewe. Muombe Roho wa Mungu akufundishe, kabla ya kuanza kusoma mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe na kukuongoza,

Natumaini unafahamu Roho Mtakatifu ndiye msaidizi na muangalizi wetu tuliyeachiwa baada ya Bwana wetu Yesu kurudi Mbinguni, na Biblia inatusisitiza kabisa kuwa Roho Mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikotamkika..!! Hivyo jitahidi kabla hujaanza kusoma Biblia, Omba kwanza usaidizi wa Roho, ili kufahamu hasa hekima na ufunuo uliopo kwenye Neno..!!

1 Wakorintho 2 : 10-11
10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila Roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
 
Back
Top Bottom