Nilitegemea aliyeleta hoja angetuambia kuwa ametafiti kama hivyo vyuo alivyosoma Dr wa ukweli akakikosa, au akagundua kuwa hakuna graduate kama huyo (Dr Slaa) kwenye hivyo vyuo; au hicho chuo hakitambuliki. Sasa anakuja kwa kutaka eti Dr Slaa atueleze, sasa hata kama atakueleza utaamini wakati hizi ulizopresent ndo yeye kawasilisha? Kama hujui exploration kamconsult Msemakweli jinsi ya kutafiti waliosoma vyuo feki, atakusaidia japo methodology, ili uje na tuhuma zilizojitosheleza. La sivyo hizi itakuwa ni zile mlizozoea siasa za majitaka.
Any way majina ya viwango kama vya elimu kama vile: Bsc (BA) au Msc (MA), siyo uniform saana duniani kote. Na hii haimanishi kuwa hizi nchi ndo wana elimu za chini. Kwa mfano, Ujerumani mpaka recently hawakuwa na Msc wala MA. Walikuwa na Diploma (wenyewe wanaita Diplom) na hii inaheshimika zaidi ya Masters. Baada ya hapa mhitimu hujiunga na PhD moja kwa moja. PhD za ujerumani huwa zina classification kama vile summa cum laude, magna cum laude, and cum laude. Suma cum laude ni kwa wale wanaopata disticntions (yaani ufaulu wa juu sana), wakifatiwa na magna cum laude, na mwisho cum laude. Kwa maelezo uliyotoa hapo juaú, ina maana Dr Slaa alipata first class katika PhD yake. Kwa maana hiyo yeye ni kichwa.
Ukiacha hilo suala la muda wa kusoma sio issue, maana qualification za mtu inategemea units alizocover, na mara nyingi kwa nchi za wenzetu huwa inategemea pia na bidii ya mtu kukamilisha Units anazotakiwa kwa qualification. Unashangaa hilo mbona wanafunzi huku huwa wanaweza kusoma huku wakifanya kazi na bado wanamaliza muda ule ule wakati kwa mazingira yetu ya Bongo kitu kama hicho ni ndoto na ukicheza wanaweza kula kichwa?
Lakini pia, elimu kwako ni nini? Je ni vyeti? Nyinyi ndo mnasababisha watu kila siku wanaforge mitihani bila ya kuelimika kisa wanataka vyeti (Oh ana masters, ana MBA, MPH, Phd nk) lakini ukiangalia quality yake ni chini almost to zero. Any way Kigwangala, watanzania hatuhitaji hivyo, tunahitaji ni mtu kudeliver. Tutawapima kwa matendo yao. Hakuna asiyejua deliverance ya Dr Slaa, si tu alipokuwa jimboni kwake Karatu, Bungeni, na kamati alizoongoza, lakini hata kwenye chama chake. Jamaa ni kichwa. Na ukitaka kuamini mwulize JK, siku hizi amekuwa ni mtekelezaji tu (copy and paste) wa yale jamaa aliyopropose through CHADEMA.