Utabiri: Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Sugu atavunja record kwa kupata kura ambazo hakuna mgombea mwingine aliwahi kupata

Utabiri: Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Sugu atavunja record kwa kupata kura ambazo hakuna mgombea mwingine aliwahi kupata

Una utani na jadi na Lucas mwashambwa? Akiamka usingizini atakuja na thread ndefu hadi utashangae.
Kwani Lucas mwashambwa yeye si CCM?
Sasa haya mambo ya Sugu kupitishwa na chama chake kugombea uraisi yeye yanamhusu nini mkuu?

Au unamaanisha kuwa yeye ataona bora apitishwe Lisu kupambana na mgombea wa CCM kuliko kupitishwa Sugu?
 
Kwani Sugu alivyoshinda uchaguzi wa ubunge jimbo la Mbeya mjini, tume ya uchaguzi ilikuwa ipi?Mkishinda all is allright mkishindwa tume ya uchaguzi haitendi haki!!!
You cannnot have both ways.You cannot have your cake and eat it too.
😂😂😂
 
Ulichoandika kina ukweli, hata mimi nitakuwa mmoja wa wachangiaji wa ticket yake ya urais.

Wana mbeya, iringa na songwe tupambane kuhakikisha sugu anakua mgombea urais wa chadema mwaka 2025, maana lisu ushawishi wake umeshuka sana na pia hana jipya la kushawishi watu wampigie kura.
Kumbe na wewe ni team Sugu!!
 
Ungepitia kwanza Sheria inayoelezea sifa na vigezo vya mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Utagundua kuwa Sugu anakosa baadhi ya Sifa na Vigezo vya kisheria na kikatiba.
Kumbe baadhi yenu mnamchukulia Sugu poa kuhusu elimu aisee...
 
Kwani Lucas mwashambwa yeye si CCM?
Sasa haya mambo ya Sugu kupitishwa na chama chake kugombea uraisi yeye yanamhusu nini mkuu?

Au unamaanisha kuwa yeye ataona bora apitishwe Lisu kupambana na mgombea wa CCM kuliko kupitishwa Sugu?
Hataki kusikia kuna kitu kinaitwa Sugu nchi hii, iwe Mbeya au popote pale. Iwe udiwani au ubunge Leo iwe Urais?!
 
Mkuu Pascal Mayalla hili swala litaenda kushangaza wengi wakiwemo Chadema wenyewe.
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Cdm kama Chama wanaweza kushiriki, lakini sisi watanzania tunaojitambua hatutajitokeza kushiriki hizi chaguzi za kishenzi. Kama mnategemea tena Yale mafuriko ya wapiga kura, mjiandae kisaikolojia kujotokeza wachache kushiriki huo uhayawani.
 
Usisahau kwa Chama Cha Majambazi/Majizi hakishindi uchaguzi kwa sanduku la kura.Zingatia hilo.
 
Hilo la kushindwa uchaguzi kutokana na sababu ulizozieleza hapo juu linaeleweka, lkn sasa Chadema ni lazima watashiriki ili kupata ruzuku ya kukisadia chama na viongozi wa chama.
 
Usisahau kwa Chama Cha Majambazi/Majizi hakishindi uchaguzi kwa sanduku la kura.Zingatia hilo.
Yani Sugu hatoshinda uchaguzi na kuwa raisi kutokana na sababu ulizozieleza, ila atashinda katika kinyanganyiro cha kumchagua mgombea atakaepeperusha bendera ya chama kwa ajili ya uraisi.

Na pia atapata kura nyingi zaidi ya walizowahi kupata wagombea wengine wa upinzani, plus atakisaidia chama chake kupata wabunge wengi kuliko mgombea yoyote wa upinzani aliewahi kugombea kabla yake.

I think umenielewa nilichomaanisha.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Hilo la kushindwa uchaguzi kutokana na sababu ulizozieleza hapo juu linaeleweka, lkn sasa Chadema ni lazima watashiriki ili kupata ruzuku ya kukisadia chama na viongozi wa chama.
Kungekuwa na uchaguzi wa kushindana hapa tungesema Kuna ushindani, sio kwa upuuzi ule unaojitokeza kwenye chaguzi zetu. Kama cdm wanatafuta ruzuku hiyo ni haki Yao, lakini kwa uhayawani ule wa kwenye chaguzi, msitegemee tena wanaojitambua kushiriki. Machafuko au mapinduzi ya kijeshi pekee ndio yataleta mabadiliko ya kweli.
 
Hapa nimekuelewa vizuri mkuu Tindo
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Kwanza naomba niwaandae kisaikolojia, wale wote ambao wanafikiri kuwa Chadema haitoshiriki katika uchaguzi mkuu wa uraisi, na ubunge.

Utabiri wangu unaonesha kuwa Chadema itashiriki katika chaguzi zote mbili. Yani uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani, na ule wa raisi na wabunge utakaofanyika mwaka 2025.

Sasa basi baada ya kukujulisha kuhusu ushiriki wa Chadema katika chaguzi zijazo, naomba nianze sasa kukufafanulia kuhusu utabiri unaoonesha kuwa ndugu Joseph Mbilinyi aka "Sugu" atapata kura nyingi kuliko wagombea wengine wa upinzani ambao waliwahi kugombea huko nyuma kabla yake.

Ni hivi utabiri unaonesha kwamba ndugu Sugu ana nyota kali ya kiuongozi na kukubalika, hivyo nyota hiyo inamsaidia kupata uungwaji mkono kutoka maeneo mbali mbali ya dunia (kama tulivyoona akitembelewa na mabalozi wa nchi zenye uchumi mkubwa duniani), na pia anaheshimiwa na kukubaliwa hata kwenye chama chake, including viongozi wakubwa wa chama (ukimtoa makamu mwenyekiti) ambae ana ubinafsi.

Hivyo utabiri unaonesha kuwa ndugu Sugu ndio atakaepitishwa na chama chake kikiongozwa na mwenyekiti wao kuwa mgombea uraisi wa chama hicho ambacho kilianguka vibaya katika uchaguzi mkuu uliyopita kutokana na sababu ambazo hapa sio mahala pake pa kuzitaja.

Nafikiri wengi mnataka kujua kwamba Sugu atagombeaje uraisi kupitia Chadema na wakati nafasi hiyo inaonekana kudhibitiwa na makamu mwenyekiti wa chama ndugu Lisu, na pia wengine wanajiuliza kwamba utabiri unasemaje Sugu atapeperusha bendera ya chama ambacho kimesema hakitasimamisha wagombea kutokana na hitilafu ya katiba na tume ya uchaguzi. Sasa utabiri unaonesha mazingira ya Sugu kugombea yatakuaje.

Utabiri unaonesha kuwa kutakuwa na msuguano mkali kati ya makamu huyo, na viongozi wenzake wa chama kuhusu chama hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu. Mwisho utabiri unaonesha kuwa makamu atashindwa na hivyo chama kitadhamiria kusimamisha wagombea wote kuanzia serikali za mitaa na hapo baadae uraisi.

Utabiri unaonesha kuwa katika swala la uraisi makamu hatoshiriki tena kwa hoja ya kujifanya anasimamia kile anachokiamini na kwamba hayuko tayari kuyumbishwa juu ya misimamo yake. Hapo sasa litatokea kundi la wana Mbeya likiongozwa na vijana na wazee waseme kuwa sasa uraisi ni zamu ya nyanda za juu kusini, watamchukulia Sugu tiketi ya kugombea uraisi, Sugu atakubali na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda katika kinyang'anyiro cha kupitishwa na chama.

Utabiri unaonesha kuwa, japo kuna wagombea wengine kadhaa watajitokeza kupambana nae katika kinyang'anyiro hicho, lkn Sugu atapita kwa ushindi mnono na hivyo kuwa mgombea uraisi kwa mara ya kwanza kupitia chama chake Chadema.

Katika uchaguzi huo, Sugu atakuwa mgombea wa kwanza uraisi kutoka upinzani kupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine wote waliowahi kugombea tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe. Na hii ni kwa sababu ya nyota yake ambayo inamfanya akubalike kwa vijana, wazee, kina mama, kina baba, kina mjomba, kina shangazi, kina babu, kina bibi nk.

Pia atakuwa mgombea wa kwanza kukipa chama chake wabunge wengi zaidi katika uchaguzi huo. Ukiona wazungu wanaingia na kutoka katika ofisi ya mtu, basi ujue kuna kitu fulani wanakiona kinakuja, kama sio sasa hivi basi baadae.

Kwa wale wanaompenda Sugu na kuhitaji awe raisi wao wa Jamhuri (sio Mbeya pekee) basi waongeze maombi ili aje kushinda katika uchaguzi mkuu ujao, maana utabiri haujaonesha kama atamshinda wa chama tawala, bali umeonesha namna atashinda kinyang'anyiro cha kupeperusha bendera ya chama chake na pia kupata kura nyingi zaidi ya wagombea wa upinzani waliopita.

Team Lissu wajiandae kisaikolojia, kwani mgombea wa Chadema ashajulikana kupitia utabiri huu.
Pumba 🚮🚮
 
Back
Top Bottom