Utabiri: Mungu tunaileta mbele yako kamati itakayopitisha jina la Rais wa Tanzania 2025

Utabiri: Mungu tunaileta mbele yako kamati itakayopitisha jina la Rais wa Tanzania 2025

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Mungu ulie chanzo cha Taifa la Tanzania watu wako tunakuja mbele yako kwa sala na maombi maalumu juu ya Taifa letu Tanzania.

Mungu Baba tunasema Asante kwa kila kiongozi ulie tupa ktk jamuhuri yetu ya Tanzania. Mungu Baba tuna sema Asante kwa kutupa Mashujaa walio lipigania Taifa hili kwa dam na Uhai wao na Leo hatuna tena.

Tuna Kushukuru kwa viongozi shupavu na wali kuwa na uthubutu kulivusha Taifa hili ktk nyakati nzito na ngumu na kamwe hawakukata tamaa Asante kwa wakuu wamajeshi Asante kwa wakuu wa usalama wa Taifa Asante kwa wakuu wa Vyombo vya ulinzi shupavu walio sema we will die ila Taifa litasimama.

Mungu tunasema Asante kwa viongozi wakuu wakitaifa ambao leo hatunao tena Asante kwakuwa wao ndio chanzo cha Taifa hili leo. Asante kwa ajili ya Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Asante kwa ajili ya Mzee Abeid Karume, Asante kwa Haya Moringe Sokoine Asante Mungu maana yote haya ni kwa utukufu wako ili Wewe uogopwe na uheshimiwe. Baba Asante kwa wamajeshi wetu walio fia vitani hasa ile vita ya uganda.

Mungu Asante kwa ajili ya Mageneral wote wa jeshi la ulinzi wa Taifa la Tanzania ambao leo hatunao tena Mungu usiwasahau hawa walimwaga dam kwa ajili ya Taifa hili kwenye most softcated operation na Leo tuna Taifa la Tanzania.

Asante kwa kutupa Jemedari Hayati John Pombe Magufuli. Asante kwakuwa hakumaliza kazi lakini yote nikwa utukufu wa Mungu.

Mungu tuna kuomba 2025 ikawe yakipeke hasa tuna elekea uchaguzi 2025 tunakuomba Mungu. Ukawalinde wale watakao ktk ku vet Rais wa Tanzania. Mungu hii shughuli itakuwa nzito sana hasa ukizingatia nyakati tulizopo na ujasusi wakidola Africa. Mungu tuna hitaji watu wenye hofu na Mungu ndio wakamchaguwe Rais wa Tanzania.

Mungu tuna kataaa madaraka yakupeana either kwa jinsia, urafiki, undugu, ukabila au udini. Mungu watanzania tuna hitaji Rais na sio jinsia awe mume au mke basi awe na misuli kuliongoza hili Taifa, Mungu tuna hitaji Rais mwenye roho ya uthubutu na anye juwa kero na mateso ya watanzania nakutupatia majibu.

Baba wapo watu muhimu sana lazima wafike 2025 japo ni wazee sana ila tunakuomba uwape pumzi ya Uhai watuchagulie Rais wa Saba ndipo uwapende zaidi. Haya majabali yalio Baki ukayalinde kwa ustawi wa Taifa hili.

Mungu tunawaombe wakuu wa ulinzi na usalama na vikosi vyote maalumu ktk kazi maalumu project 2025Q (Utabiri) wape akili uwezo wa ajabu kufanikisha kazi walizo NAZO na mwisho kulipatia Taifa Rais wa Saba.

Kuna watu wangetamani Taifa hili kuwa Mali yao na uzao wao Mungu wangu Hilo lisitokee chini ya uwepo wako. Macho yetu yapo kwako macho yetu yapo Mbinguni usitupite wana wako wa Tanzania. 🙏😭🙏🙏🙏
 
Mama sio muhuni Sana KULIKO waliomzunguka!

Kuna wahuni wamemzidi uhuni watamchomesha Sana na kuzua kambi mbili kali kama za msomali vs marope na yeye na wale jamaa wazito watampitisha asietarajiwa kati yao ambao ni Kati ya Ino wa Kaisho, Mabira, Kayanga, kaitambuzi n.k na mkono wa baunsa!!

Yote KHERI

Mfungo mwema!!
 
Mungu tuna kuomba 2025 ikawe yakipeke hasa tuna elekea uchaguzi 2025 Mungu tuna hitaji watu wenye hofu na Mungu
Samia ana hofu ya Mungu.
Mungu tuna kataaa madaraka yakupeana either kwa jinsia, urafiki, undugu, ukabila au udini.
Aliyemleta Samia ni Mungu na kama amempangia kuendelea, Samia ataendelea. Aliyeleta rais wa jinsia nyingine pia ni Mungu.
Mungu watanzania tuna hitaji Rais na sio jinsia awe mume au mke basi awe na misuli kuliongoza hili Taifa,
Hata Samia ni rais wa JMT na sio jinsia yake, msuli anao na sote tumeuona
Mungu tuna hitaji Rais mwenye roho ya uthubutu
Samia ameonyesha uthubutu mkubwa sana kupita hata marais wanaume
kero na mateso ya watanzania nakutupatia majibu.
Kazi inaendelea
Baba wapo watu muhimu sana lazima wafike 2025 japo ni wazee sana ila tunakuomba uwape pumzi ya Uhai watuchagulie Rais wa Saba ndipo uwapende zaidi.
Ndani ya CCM hakuna uchaguzi ni Samia tuu!, unless ile sauti ni ya YEYE. Hii ya kusema 2025 tunatafuta rais wa awamu ya 7 haijakaa poa unless wewe mwenzetu tayari umeisha ambiwa 2025 sio Samia!.
Haya majabali yalio Baki ukayalinde kwa ustawi wa Taifa hili.
Mungu tunawaombe wakuu wa ulinzi na usalama na vikosi vyote maalumu ktk kazi maalumu project 2025Q (Utabiri) wape akili uwezo wa ajabu kufanikisha kazi walizo NAZO na mwisho kulipatia Taifa Rais wa Saba.
Hii haijakaa poa. Kama umeambiwa sema...
Kuna watu wangetamani Taifa hili kuwa Mali yao na uzao wao Mungu wangu Hilo lisitokee chini ya uwepo wako. Macho yetu yapo kwako macho yetu yapo Mbinguni usitupite wana wako wa Tanzania. 🙏😭🙏🙏🙏
Mkuu nabii wetu TumainiEl , kwa sisi wasomaji wa jicho la tatu, hii sala yako haijakaa vizuri na haina nia Njema na Mama kwasababu kwa mujibu wa utaratibu wa ndani wa CCM, 2025 inatolewa fomu moja tuu ya urais kwa mtu mmoja tuu!. Hakuna kamati ya kumjadili bali ni procedures tuu za kumpitisha!, sasa hii kamati unayoiombea wewe ni kamati ya kufanya nini?.

Rais wa Tanzania kwa 2025 tayari aliishapangwa siku nyingi na Mungu mwenyewe ila sisi tuu ndio bado hatujaambiwa aliyepangiwa ni nani. Sasa kwa vile Mungu ametuletea Samia, kwa sasa twende na Samia mpaka pale Mungu atakapo tuonyesha vinginevyo kama nilivyo shauri hapa Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hii sauti niliyoisikia Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke ila sina uhakika sana ni sauti ya nani!, hivyo kama ni sauti ya kwake YEYE, then sio sauti ya kuipuuzia, na muda muafaka ukifika, hata Samia mwenyewe ataelezwa, kuwa ni wewe!. Naamini hata ile siku ya Wanawake Duniani ya Machi 8 mwaka 2017 tulipomshauri JPM, asigombee awamu take ya pili na badala yake ampishe VP wake Samia, naamini JPM alisoma Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” tulishauri
Wanabodi,
Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu.

Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa. Kwa jinsi alivyo na sauti safi, tamu na laini yenye lafudhi ya Kizanzibari, akiongea, utatamani asimalize kuongea, utatamani aendelee tuu kuongea, ukijumlisha na yale macho...!, sijui hata akitaka kugomba, atagomba kwa sauti gani na macho gani maana...!.

She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.

Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.

Paskali
lakini ndio hivyo tena!.

Mwezi April mwaka wa uchaguzi, 2020, tukashauri tena "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Wanabodi,

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.
.
Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?. Hili mnalionaje?.

Paskali
Rejea
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?! - JamiiForums

Wajue The Top Five Most Prominent Members wa Bunge Maalum la Katiba!. - JamiiForums

New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!. - JamiiForums

Makamu wa Rais, Samia Suluhu aweza kuendana na kauli za Rais Magufuli - JamiiForums
Naamini kabisa hata JPM mwenyewe atakuwa aliambiwa kitu lakini ndio hivyo tena!.
Hivyo kama hii sauti ni yake YEYE mwenyewe ambaye NDIYE, then Mama ataambiwa na ukiambiwa asipuuzie!!. Lakini kama sauti hii sio yake YEYE bali ni sauti ya yeye tuu, then Samia hataambiwa kitu na asipoambiwa kitu, 2025 tunakwenda na Samia na itakuwa ni Samia!.
P
 
Mungu ulie chanzo cha Taifa la Tanzania watu wako tunakuja mbele yako kwa sala na maombi maalumu juu ya Taifa letu Tanzania.
Hii ni RUBBISH!! Awamu ya Saba inatoka wapi? Mwaka 2025 ni Samia MITANO tena. Nyie watu wa Magufuli futeni mawazo, kizazi chenu au watu wenye itikadi ya UKATILI, UUAJI, WIZI na UWONGO hamna nafasi kwa Tanzania yetu kamwe.
 
Back
Top Bottom