Wabongo bwana kuna watu wanajidai wanaijua sana dini na wanamjua sana Yesu,mtu kaeleza ya kwake badala ya kumuuliza nini kimemsukuma aseme hivyo mtu anakimbilia kutukana mara ooh kwa Jina la Yesu..kwamba wewe ndiye una imani sana ?
Kuhusu rangi ya ndege na matukio mengine aliyosema itoshe tu kusema tukubali jamaa alitoa utabiri wake ambao ni ndege kuanguka.
Swala la kutafsiri kila kitu kwa ufasaha ni ngumu haijalishi utabiri wa mtabiri unatokana na nguvu ya Mungu au la !
Kwa Wakristu kuna kitabu kinaitwa UFUNUO, kila mmoja ana tafsri ya ufunuo ule,ukienda kwa Msabato atakuambia hivi,ukienda kwa Mpentekoste anakuambia vile,ukienda kwa Mkatoliki naye ana tafsri yake.
Hivyo hakuna haja ya kumbeza. Maana utabiri wake mkuu ni ajali ya ndege hayo mengine ni maelezo ya nyongeza ambayo pengine ameshindwa kuyatafsiri vizuri ili ili kuwa sawa na utabiri wake.
Kuna mtu utakuta anapinga kwa nguvu na kutukana lakini kanisani kwake katabiriwa mwaka huu ataolewa/atajenga nyumba/atapata kazi n.k yasipotokea ndani ya mwaka husika haendi kumkosoa kiongozi wake aliyemtabiria badala yake anaendeleza kuwa na imani. Lakini hapa kwa jamaa utakuta mtu yule yule anajidai mkali na kutukana ovyo.
Tujifunze kuheshimu watu,kama alichoongea kipo kinyume na uelewa/mtazamo wetu basi tuhoji na sio kutukana ovyo.