Utachukua hatua gani ukikutana na mtoto kwenye barabara isiyo na watu kama hivi?

Wee bwana Sio rahisi kivile mkuu. Kumhifadhi mtoto maana yake - ale, alale, akiugua umpeleke hospitali i.e Mustakabali mzima wa maisha yake unaubeba wewe lakini sio kwa hiari yako. Watu (hata kama ni mtoto) wana mambo mengi usiyoyajua bado na pengine huenda ni hatari kubwa kwako na familia yako. Tena uombe asikufie mikononi mwako. Utahangaishwa sana na Polisi, Ustawi wa Jamii, Dini na hata ndugu zako pia watakuhoji sana. Ni gharama ya kujitakia.
Ninafahamu huo ugumu wote unaosema, nina mtoto ana umri wa kama miaka 9 sasa, sijui ndugu yake hata mmoja, mtoto huyo alitelekezwa na mama yake wakiwa wanasafiri kwa miguu ambapo giza liliwakuta maeneo ya mashambani niliko na kibanda changu kilichokuwa kinakaliwa na mwangalizi (mume akiishi na mkewe na mtoto hapo) nikamwomba kwa usiku huo ampeleke kwa uongozi wa kijiji ambao uliridhia wajihifadhi hapo kwakuwa walidhoofu kwa njaa, kiu na uchovu, siku ya pili huyo mama aliondoka na kumtelekeza mtoto kwa huyo mwangalizi wa shamba na tangia hapo ikabidi niwe responsible for everything na mtoto alikuwa kama na mwaka mmoja na miezi kadhaa.
 
Kongole kwako mkuu. Huo ni ushujaa wa hali ya juu. Mungu na akubariki sana.
Ni kutokana na jinsi dunia ilivyoharibika - watu wanahofu kubwa kutenda kama ulivyofanya wewe kwani hawajui ni nini kitatokea akitenda lile analoona ni jema.
 
Back
Top Bottom