Ninafahamu huo ugumu wote unaosema, nina mtoto ana umri wa kama miaka 9 sasa, sijui ndugu yake hata mmoja, mtoto huyo alitelekezwa na mama yake wakiwa wanasafiri kwa miguu ambapo giza liliwakuta maeneo ya mashambani niliko na kibanda changu kilichokuwa kinakaliwa na mwangalizi (mume akiishi na mkewe na mtoto hapo) nikamwomba kwa usiku huo ampeleke kwa uongozi wa kijiji ambao uliridhia wajihifadhi hapo kwakuwa walidhoofu kwa njaa, kiu na uchovu, siku ya pili huyo mama aliondoka na kumtelekeza mtoto kwa huyo mwangalizi wa shamba na tangia hapo ikabidi niwe responsible for everything na mtoto alikuwa kama na mwaka mmoja na miezi kadhaa.