l
hata ukiwatosa, jua mtoto wako ambaye amezaliwa mama mmoja nao, hatawaacha, na atakuheshimu sana kama utawathamini watoto alionyonya nao ziwa moja. ugomvi ubaki wa wewe na mama, ila watoto wabaki na furaha na amani. pia, hata mama yao, kwa story hii, inaonyesha watoto hao walizaliwa kabla hawajaoana, ndoa ina miaka 12 wao wana miaka 15, hivyo walizaliwa kwenye kipindi ambacho walikuwa wachumba tu, hawakuwa kwenye ndoa. sihalalishi uzinzi ila nadhani ni busara kwake hao watoto aendelee kuwapenda kama alivyojenga upendo kwa miaka yote hiyo, ila baba yao apatikane ili wajue biological father, wanakujaga kuoana ndugu ukifanya mchezo.
pia, kwa mama, hilo ni kosa kabla ya commitment ya ndoa, asimhukumu kwa makosa ya kabla ya ndoa ambayo hata yeye si ukute ni kwasababu tu ni mwanaume angekuwa anashika mimba angeshakuwa na watoto wa nje kwasababu kama hakuwa anacheat huko aliko awe wa kwanza kurusha jiwe. ugumu unakuja tu pale mkeo uliyeishi naye miaka yote hiyo anapotakiwa akabiliane na aibu, ila linatakiw akuwa hivyo kwa muda mfupi na wakubaliane kuendelea na ndoa regardless of that. ni sawa na mtu umetenda dhambi, unatubu, na katika kutubu kuna aibu utaenda kukumbana nayo, hivyo unasema as long as nitasamehewa dhambi yangu, niko tayari kukabiliana na aibu hii. then maisha yataendelea.
mimi nilishakuwa mzinzi sana hata kwenye ndoa, kabla ya kukabidhi maisha yangu rasmi kwa Yesu. nilipokuja kuamua kusalenda, nilikubaliana na aibu zote, matusi yote hata kwa watu walioniheshimu as long as nimesamehewa dhambi zangu, na huwa naweka wazi tu ili iwe fundisho kwa wengine, nawaeleza madhara ya uzinzi kwenye ndoa na mengi mazito niliyopitia kutokana na dhambi.