Utachukua uamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako kumbe sio wako?

Utachukua uamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako kumbe sio wako?

Maisha yanasonga tu,ivi mfano unamwacha unaenda OA alonawatoto 4 wamijamaa! Unasolve au?

Kama ni mwazoni mwa Ndoa hapohapo nafukuza wote navuta chomboo mpya. Cha msingi nikuishi ukijua Sasa kwamba hauko na watu salama sana yaani mke na hao watoto.
Kwa kesi ya jamaa kusema unaendelea nae ni kujipunguzia siku za kuishi duniani, mwanamke alionesha kumdharau na drama nyingine nyingi.
 
Ni kuachana na mama yao waende kwa baba yao halisi, ni simple tu.

Na vile watoto washakua wakubwa basi hata wao itabidi waujue ukweli kua mama yao alicheza rafu.
 
Kazi ya kumsamehe mwanamke mzinzi ni ya Mungu si ya mwanaume.
Well said, huyu mwanamke na wengine wote wenye akili kama hii, ni wa kuwapiga chini tu mara moja. Ni muhimu sana kuoa mwanamke mwenye muelekeo wa maisha si kiruna njia kama hawa waśanii wetu wa Kibongo ama mke wa Jeremy. Kuweni makini sana na wanawake wanaojichubua na kufuga ndevu.
 
Kwann huwa hawashitaki mahakamani maana hapo kuna kesi ya kujibu mbona. Kwann huwa wanaume wanapotezea hizi issue, me nampeleka mahakamani atalipa kila senti niliyotoa na nitaleta ushahidi.
 
busara ni kufuata kile Roho Mtakatifu atakachokuongoza nacho, hata akisema umsamehe ubaki naye ila watoto wajue baba yao ili wasije kuoana na ndugu zao hapo baadaye, unatakiwa kukubaliana nalo. maamuzi mengi watu wanayachukua nje ya Mungu huwa hayana mwisho mwema. kuna kitu tu kizuri alichonacho huyo mwanamke ambacho hata kama alikuwa na makosa, ila kinamfaa huyo jamaa.

watoto wanaonekana walizaliwa miaka mingi, pengine kabla ya ndoa au baada ya ndoa, wakati ule ambao watu ambao hawajaokoka huwa wanakuwa hawana uhakika na mchumba waliye naye na wanakuwa na wachumba wengi, na si ukute huyo mwanamke hakujua kama mimba sio ya huyo jamaa, pengine alitembea nao wote siku za hatari, na ameishi akijua watoto ni wa jamaa. na baada ya kuoana amekuwa mke mwema, kwanini umtimue kwa makosa ya miaka 15 iliyopita?
Jinai haifi hata kama makosa yalifanyika miaka 15 iliopita, lazima mwanamke awajibike kwa makosa yake!!
 
l

hata ukiwatosa, jua mtoto wako ambaye amezaliwa mama mmoja nao, hatawaacha, na atakuheshimu sana kama utawathamini watoto alionyonya nao ziwa moja. ugomvi ubaki wa wewe na mama, ila watoto wabaki na furaha na amani. pia, hata mama yao, kwa story hii, inaonyesha watoto hao walizaliwa kabla hawajaoana, ndoa ina miaka 12 wao wana miaka 15, hivyo walizaliwa kwenye kipindi ambacho walikuwa wachumba tu, hawakuwa kwenye ndoa. sihalalishi uzinzi ila nadhani ni busara kwake hao watoto aendelee kuwapenda kama alivyojenga upendo kwa miaka yote hiyo, ila baba yao apatikane ili wajue biological father, wanakujaga kuoana ndugu ukifanya mchezo.

pia, kwa mama, hilo ni kosa kabla ya commitment ya ndoa, asimhukumu kwa makosa ya kabla ya ndoa ambayo hata yeye si ukute ni kwasababu tu ni mwanaume angekuwa anashika mimba angeshakuwa na watoto wa nje kwasababu kama hakuwa anacheat huko aliko awe wa kwanza kurusha jiwe. ugumu unakuja tu pale mkeo uliyeishi naye miaka yote hiyo anapotakiwa akabiliane na aibu, ila linatakiw akuwa hivyo kwa muda mfupi na wakubaliane kuendelea na ndoa regardless of that. ni sawa na mtu umetenda dhambi, unatubu, na katika kutubu kuna aibu utaenda kukumbana nayo, hivyo unasema as long as nitasamehewa dhambi yangu, niko tayari kukabiliana na aibu hii. then maisha yataendelea.

mimi nilishakuwa mzinzi sana hata kwenye ndoa, kabla ya kukabidhi maisha yangu rasmi kwa Yesu. nilipokuja kuamua kusalenda, nilikubaliana na aibu zote, matusi yote hata kwa watu walioniheshimu as long as nimesamehewa dhambi zangu, na huwa naweka wazi tu ili iwe fundisho kwa wengine, nawaeleza madhara ya uzinzi kwenye ndoa na mengi mazito niliyopitia kutokana na dhambi.
Weak mind
 
Kwann huwa hawashitaki mahakamani maana hapo kuna kesi ya kujibu mbona. Kwann huwa wanaume wanapotezea hizi issue, me nampeleka mahakamani atalipa kila senti niliyotoa na nitaleta ushahidi.
Lazima kuna fidia haiwezi tu kuisha bure bure labda mwanaume aamue.
 
Back
Top Bottom