Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,345
- 10,885
niletee ushahidi Yesu alikuwa mkristo au alileta ukristo.
Soma Mathayo 16: 13-20
"Yesu aliingia sehemu ya Kaisari Filipi. Akawauliza wafuasi wake, "watu wanasema Mwana wa Mtu ni nani?" Wakasema, "wengine Yohane Mbatizaji, wengine Eliya, tena wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii". Akawaambia, na "Ninyi mwasema kuwa mimi ni nani?" Simoni Petro akajibu, "Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu Mzima".
Yesu akamjibu, "Mwenye heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwili na damu vilivyokufunulia hayo, isipokuwa Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, wewe u Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, na milango ya Jehenamu haitalishinda. Na wewe nitakupa funguo za ufalme wa mbingu. Lolote utakalofunga duniani, litafungwa mbinguni pia; na lolote utakalofungua duniani, litafunguliwa mbinguni pia. Kisha akawaonya wafuasi wake wasimwambie mtu ya kuwa yeye ni Kristo".
Soma pia Marko 8: 27-29
"Toka huko Yesu na wafuasi wake walienda katika vijiji vya Kaisari Filipi. Njiani aliwauliza wafuasi wake, "Watu wanasema mimi kuwa nani?" Wakamjibu, "Yohane Mbatizaji, wengine Eliya, wengine mmojawapo wa manabii". Naye akawauliza, "Na ninyi mnasema mimi kuwa nani?" Petro akamjibu akisema, "Wewe ndiwe Kristo". Akawaonya wasimwambie mtu habari zake".
Soma pia Yohane 10: 22-29.
"Kulikuwa na Sikukuu ya Kutabaruku Hekalu iliyoadhimishwa Yerusalemu. Ilikuwa majira ya baridi. Yesu alitembea hekaluni, katika ukumbi wa Sulemani. Hapo Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, "Hadi lini utatuhangaisha? Kama wewe u Kristo, utuambie wazi wazi". Yesu akawajibu, "Niliwaambia, lakini hamsadiki. Matendo niyafanyayo kwa jina la Baba yangu, ndiyo yanayonishuhudia. Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu ninyi si kati ya kondoo wangu. Kondoo wangu husikia sauti yangu, nami nawajua, nao wananifuata. Nawapa uzima wa milele, hawataangamia milele. Hakuna awezaye kuwapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao, ni mkubwa kuliko wote, na hakuna awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.