Alifanya hivyo ili neno la unabii litimie kwa kuteswa, kusulubiwa na kufa msalabani. Kisha kufufuka. Kwamba, "Akasema, Lazima Mwana wa Mtu kupatwa na mateso mengi, kukataliwa na wazee, pia na makuhani wakuu na Waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka" (Luka 9: 22).
Hivyo wakati ulikuwa haujatimia! Ndiyo maana katika injili ya Mathayo 16: 21-23 inasema:
"Toka wakati huo, Yesu alianza kuwaonya wafuasi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu na kupatwa na mateso mengi kwa wazee, makuhani wakuu na Waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua upande, akaanza kumwonya na kusema, "Mungu akurehemu Bwana. Hayo hayatakupata hasha". Akageuka, akamwambia Petro, "Nenda nyuma yangu, Shetani! U kikwazo katika njia yangu, kwani maana mawazo yako si ua Mungu, bali ya kibinadamu".
Soma pia Marko 8: 31-33.
Some tena bandiko langu la saa 12:13 nililokujibu kuhusu ulipoanzia ukristo. Utapata jibu humo kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume.
Pia kwa kuongezea soma Mathayo 13: 54-58
"Akaenda nyumbani kwake. Huko akafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa na kusema, "Amepataje hekima hii na uwezo wa miujiza?" Je, huyu si mwana wa seremala? Na mama yake haitwi Maria? Na kaka zake si Yakobo, Yosefu, Simoni, na Yuda? Na dada zake wote hawakai nasi hapa petu? Basi, hayo yote ameyapata wapi? Wakakwazika kwake. Yesu akawaambia, "Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na nyumbani mwake". Huko hakufanya miujiza mingi kwa sababu ya ukosefu wao wa imani".
Pia injili ya Marko 6: 1-6 utapata majibu.